Akaunti ya Escrow yafichua mazito

Akaunti ya Escrow yafichua mazito

Aaah, kumbe unanusa tu? sasa sijui tunachobishana ni nini? ripoti hujaiona unaanza kutuhumu watu, huyo Mwenyekiti wa PAC ni wapi kamtuhumu mtu? wote tumemsikiliza na alichosema ni kuwa ripoti anayo na ipo tayari na wakati wowote akiambiwa ailete bungeni ataileta, na pia amesema ni vyema ikiletwa kwani matusi ya kila aina yamekuwa mengi.

Sasa wewe kunusa kwako hakukusaidii wala hakutusaidii kitu, tutakapoiona hiyo ripoti ndipo tutakuwa na uhakika kama kuna wezi au hakuna, lakini ukweli unabaki pale pale, fedha zilizowekwa escrow toka 2006 ni za malipo halali ya huduma walizotoa IPTL na PAP, na PAP wamesema na kutangaza kuanzia awali kuwa kama IPTL ilikuwa inadaiwa, madeni hayo yote sasa hivi ni yamehamia wao.

isitoshe, PAP bado wanatoa huduma, mitambo ipo Tanzania, mizima na inazalisha na sidhani kama issue hapa ni wizi.
Kwa mujibu wa habari tunazozisoma kila, nnachokiona kwa sasa ni kuna watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kuelekea uchaguzi, kuna wengine wamekasirishwa kukosa ulaji kwenye makesi yasioisha, kuna wengine wanaotaka PAP ifuge mitambo ili waweke ya wanaowakilisha ili waendeleze ulaji, kuna wengine wametofautiana kwa kukoseshwa udalali na wao wanachangia huu uonekane ni mgogoro.

Sijui unaelewa hayo?

Think.
FaizaFoxy nimekuelewa unasimamia ipande upi; bora wote tunyamaze hadi ripoti isomwe tujue inasema nini na wamebaini nini
 
Last edited by a moderator:
watanzania tunajazwa chuki ya ajabu ni hatari kilichoandikwa na majira ni sahihi kabisa kama inafikia fitina kwa ajiri ya kukosa kitu ni hatari au kwa kuwa kuna mtu anataka kugombea urais huyo anayefanya vitina hiyo ni kumuogopa kama ukoma huyo aliokosa gass ndie alieifirisi bank ya NBC mpaka ikauzwa chee.
kwanini mtu huyo asijadiliwe bungeni? nawaombeni wabunge msipandikizwe chuki ni hatari

Kama una ushahidi si uende kuwasaidia NBC ili walipwe kama hata hiyo kesi ipo.
 
Aaah, kumbe unanusa tu? sasa sijui tunachobishana ni nini? ripoti hujaiona unaanza kutuhumu watu, huyo Mwenyekiti wa PAC ni wapi kamtuhumu mtu? wote tumemsikiliza na alichosema ni kuwa ripoti anayo na ipo tayari na wakati wowote akiambiwa ailete bungeni ataileta, na pia amesema ni vyema ikiletwa kwani matusi ya kila aina yamekuwa mengi.

Sasa wewe kunusa kwako hakukusaidii wala hakutusaidii kitu, tutakapoiona hiyo ripoti ndipo tutakuwa na uhakika kama kuna wezi au hakuna, lakini ukweli unabaki pale pale, fedha zilizowekwa escrow toka 2006 ni za malipo halali ya huduma walizotoa IPTL na PAP, na PAP wamesema na kutangaza kuanzia awali kuwa kama IPTL ilikuwa inadaiwa, madeni hayo yote sasa hivi ni yamehamia kwao.

isitoshe, PAP bado wanatoa huduma, mitambo ipo Tanzania, mizima na inazalisha na sidhani kama issue hapa ni wizi.

Kwa mujibu wa habari tunazozisoma kila siku, nnachokiona kwa sasa ni kuwa kuna watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kuelekea uchaguzi, kuna wengine wamekasirishwa kukosa ulaji kwenye makesi yasioisha, kuna wengine wanaotaka PAP ifunge mitambo ili waweke ya wanaowawakilisha ili waendeleze ulaji, kuna wengine wametofautiana kwa kukoseshwa udalali na wao wanachangia huu uonekane ni mgogoro.

Sijui unaelewa hayo?

Think.

Ndugu yangu kama ulimsikia Mh Zito jana wakati anawasilisha mchango wake unaweza kabisa kujua nini kipo ndani ya ripoti nanukuu "Kwa mambo yaliyotokea usingetegemea kutokea katika nchi yenye utawala wenye udhibiti na ambao unafanya maamuzi kwa kila jambo kwa wakati haya mambo yaliyotokea ungetegemea kutokea kwenye nchi kama Somali, Congo, iraq, sudani kusini, afrika ya kati ambazo uongozi wake upo katika migogoro ya hapa na pale hivyo udhibiti ni mdogo" kwa maneno hayo unapata picha gani kwa yaliyotokea kwenye sakata hili la ESCROW. Lakini jambo la muhimu ni kuwa nasubira ukweli utajulikana walio chafuliwa watasafishwa outomatic. Watanzania tuwe na subira
 
WAKATI Bunge likijiandaa kusomewa ripoti ya uchunguzi wa Akaunti ya Escrow bungeni Mjini Dodoma, ripoti hiyo imezidi kuwapasua vichwa wabunge baadhi yao wakienda mbali zaidi na kudai wamebaini ukweli wa fedha hizo.

Hatua hiyo inatokana na taarifa zinazodai malipo ambayo yanalalamikiwa kufanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Kampuni ya Independet Power Supply Limited (IPTL), yalikuwa halali si ya fedha za umma.

Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya wabunge wanaodai kupata yaliyomo kwenye ripoti hiyo kuhusiana na malipo hayo, zinasema wabunge wengi wamefahamu ukweli na kinachofanyika ndani ya Bunge ni kupotosha ukweli kwa maslahi ya wachache.

Wakizungumza na gazeti hili, mmoja wa wabunge hao ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kinachoweza kufanyika sasa ndani ya Bunge ni uonevu kwa kuwa BoT ililipa malipo halali kwa IPTL na taarifa ziko wazi.

“Nimeipata ripoti ya CAG na taarifa zingine, nimezisoma kwa umakini mkubwa na kubaini kilichopo ni vita ya madaraka, kuna wakati tunafuatwa na watu ili tuwawajibishe viongozi hasa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,” alisema.

Alidai kuna baadhi ya wabunge ambao wamejiridhisha kuwa malipo hayo yalilipwa ili kutekeleza makubaliano kati ya IPTL na Serikali ambapo BoT ilichaguliwa kama wakala wa kutunza fedha.

Alisema hali hiyo ilitokana na uwepo wa mgogoro wa kimaslahi kati ya wabia wa IPTL ambao ni kampuni ya VIP (ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa) inayomilikiwa na James Rugemalila na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia (ilikuwa inamiliki asilimia 70).

Mbunge huyo alisema taarifa zinaonyesha kwamba Mahakama Kuu iliamua pande zote mbili VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano (MoU) juu ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi ya umeme, ambayo IPTL inauzia TANESCO.

Aliongeza kuwa, nyaraka zinaonesha mahakama ilielekeza malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti maalumu hadi mgogoro utakapoamriwa kati ya wabia hao ambao walikubaliana kufungua akaunti ya pamoja BoT na akaunti hiyo kuitwa Escrow.

“Ukitazama kwa umakini, kinachofanywa ni kumuonea Pinda kwa sababu ya upole wake, kuna watu wanaamini atagombea urais hivyo wanataka kumharibia,” alisema mbunge mmoja kutoka mkoani Morogoro.

Mbunge mwingine kutoka Dodoma, alisema ukisoma taarifa za Escrow, zinaonesha wazi kuwa BoT ilikuwa wakala wa kutunza fedha hizo ambapo TANESCO na Serikali walisaini hati kama sehemu ya wabia wakiwa walipaji wa umeme kwa IPTL.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ambazo gazeti hili iliziona zinaonesha makubaliano hayo yalifikiwa Julai 5, 2006 na kila upande uliwakilishwa na wahusika, kutia saini ambapo kwa upande wa Serikali alisaini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara wakati huo, Arthur Mwakapugi.

Taarifa hiyo ilionyesha kwa upande wa IPTL alisaini aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Datuk Baharuden Majid na upande wa BoT, alisaini aliyekuwa Gavana Mkuu, marehemu Daudi Balali kama wakala wa kuhifadhi fedha hizo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ikiwa ni maelekezo ya mahakama, ilielezwa kuwa mgogoro utakapoisha kati ya wabia, BoT itatoa fedha zote ilizokuwa inazihifadhi katika akaunti hiyo kwa mujibu wa hati husika ya makubaliano kwa ajili ya malipo ya uuzaji wa umeme kwa TANESCO.

Kwa upande wake, mbunge mwingine kutoka mkoani Tabora, ambaye alikuwa na mbunge mwenzake kutoka Mkoa wa Pwani, alisema ukilitazama Bunge kwa umakini limeanza kugawanyika.

“Kuna wafanyabiashara waliokosa vitalu vya gesi wamekuja na yao ndani ya Bunge ili wamwajibishe Waziri wa Nishati na madini kwa maslahi yao na wengine walikuwa wanatoa ushauri wa kisheria katika suala hili,” alisema mbunge huyo.

Aliongeza kuwa, Serikali inapaswa kuwa makini na kuhakikisha inasimama imara kuelezwa ukweli wa jambo hilo kwani anaamini kinachofanyika ndani ya bunge ni hasira za watu.

Chanzo:Majira

Tunashukuru kwa maelezo, sasa leteni basi hiyo ripoti bungeni ili mambo yaishe basi sio mnaishia kujinyeanyea.
 
Licha ya Juhudi za Mh.Kafulila a.k.a Tumbili kutaka kuzimwa hatimae zimezaa matunda.Nahisi ni Ushindi kwa Tumbili.Maswi na Werema mtambue ya kuwa Tumbili ni mjanja kuliko fisi.
 
Dah!
Nimefungua TV... ESCROW,
Nimefungua Redio... ESCROW,
Nimefungua Facebook... ESCROW,
Nimefungua Twitter... ESCROW
Eeh! naogopa hata kufungua Friji....!

Mamamamaaaaaeeeeeee nimecheka hadi basi....ukifungua friji nae escrowwwww
 
Too Late....majira.....haisaidii tena hii backup

Last edited by a moderator:
Sikumaliza kusoma habari hii, kwa haraka niliruka mpaka chini kwenda kuangalia chanzo. Nilipoona ni gazeti la Majira, nikavutiwa kurudi juu ili nimalize habari halafu nikae nifanye tathmini yangu mwenyewe. AKILI ZA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKOOOO!!!
 
mleta uzi ananishanganza anapoamua ku base upande mmoja katika kujenga hoja zake kwakuhoji wabunge wanaomtetea PM badala ya kubalansi stori, huu kwa kifupi ni uandshi wa kimasilahi kama sio uandishi kanjanja. Kama nia ya mwandishi ingekua njema angefurahia sana ripotiya escrow isomwe bungeni hadharani ili kukata mzizi wa fitina na ukweli ukajulikana. pia tufahamu kuwa kuweka wazi taarifa nzima ya escrow kutamsidia zaidi pinda katika mbio zake a urais kuliko ilivyo sasa.kma ni msafi anaogopa nini na kuhisi anaonewa hadi kusingizia kuwa eti kujadili suala hili ni kuingilia uhuru wa mahakama. uandishi wa namna hii ni dhahiri kuwa ni uandishi wa kimaslahi na hauwezi kumsaidia mtu yeyote
 
Ningekuwa mmiliki wa gazeti la Majira ningemfukuza Mhariri wake Mkuu leo na kuwaomba radhi watanzania. Unasoma public mood katika mambo serious, halafu unakurupuka na habari ya kijinga kiwango hiki. Nayo unadai umetumia uhuru wa habari. Ujinga mtupu.
 
Donatila ingawaje chanzo cha habari si wewe lakini kuiweka hii habari haiwezi kubadili upepo. Watanzania sasa hivi wanataka kuona wezi walitajwa kwenye hiyo ripoti wanafukuzwa kazi na kupandishwa mahakamani kujibu mashtaka ya wizi.

Habari hii ya majira inakinzana kabisa na maelezo ya mwenyekiti wa kamati ya PAC ambayo yanaashiria kabisa kuwa kuna "suspects" kwenye taarifa za uchunguzi wa ESCROW account

kwan wezi washatajwa mkuu? nisaidie kwahilo plzzzz
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha ha ha ha ha majiraaaaaaa on work, hata mfanyeje majira hamwezi kurudisha akili za Watanzania nyuma juu ya hili, kwani kama ni mbio za urais si tutajua nani mshiriki na nani hahusiki wasi wasi wenu nini bwana. Kwa bahati nzuri sijui kama nilishawahi kununua gazeti la Majira kwani kwangu mimi halina kitu cha kuongeza kwenye ubongo wangu. Unajua kuna level ya elimu ukisha ifikia huwezi soma gazeti la majira amini usiamini ndio hivo. Kwa maslahi ya Taifa langu naunga mkono kila anayeonyesha kuwajibisha wahusika wote. SHAME ON YOU ALL WHO ARE AGAINST WITH THE PUBLIC INTEREST ON THIS SCANDAL
 
WAKATI Bunge likijiandaa kusomewa ripoti ya uchunguzi wa Akaunti ya Escrow bungeni Mjini Dodoma, ripoti hiyo imezidi kuwapasua vichwa wabunge baadhi yao wakienda mbali zaidi na kudai wamebaini ukweli wa fedha hizo.

Hatua hiyo inatokana na taarifa zinazodai malipo ambayo yanalalamikiwa kufanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Kampuni ya Independet Power Supply Limited (IPTL), yalikuwa halali si ya fedha za umma.

Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya wabunge wanaodai kupata yaliyomo kwenye ripoti hiyo kuhusiana na malipo hayo, zinasema wabunge wengi wamefahamu ukweli na kinachofanyika ndani ya Bunge ni kupotosha ukweli kwa maslahi ya wachache.

Wakizungumza na gazeti hili, mmoja wa wabunge hao ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kinachoweza kufanyika sasa ndani ya Bunge ni uonevu kwa kuwa BoT ililipa malipo halali kwa IPTL na taarifa ziko wazi.

“Nimeipata ripoti ya CAG na taarifa zingine, nimezisoma kwa umakini mkubwa na kubaini kilichopo ni vita ya madaraka, kuna wakati tunafuatwa na watu ili tuwawajibishe viongozi hasa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,” alisema.

Alidai kuna baadhi ya wabunge ambao wamejiridhisha kuwa malipo hayo yalilipwa ili kutekeleza makubaliano kati ya IPTL na Serikali ambapo BoT ilichaguliwa kama wakala wa kutunza fedha.

Alisema hali hiyo ilitokana na uwepo wa mgogoro wa kimaslahi kati ya wabia wa IPTL ambao ni kampuni ya VIP (ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa) inayomilikiwa na James Rugemalila na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia (ilikuwa inamiliki asilimia 70).

Mbunge huyo alisema taarifa zinaonyesha kwamba Mahakama Kuu iliamua pande zote mbili VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano (MoU) juu ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi ya umeme, ambayo IPTL inauzia TANESCO.

Aliongeza kuwa, nyaraka zinaonesha mahakama ilielekeza malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti maalumu hadi mgogoro utakapoamriwa kati ya wabia hao ambao walikubaliana kufungua akaunti ya pamoja BoT na akaunti hiyo kuitwa Escrow.

“Ukitazama kwa umakini, kinachofanywa ni kumuonea Pinda kwa sababu ya upole wake, kuna watu wanaamini atagombea urais hivyo wanataka kumharibia,” alisema mbunge mmoja kutoka mkoani Morogoro.

Mbunge mwingine kutoka Dodoma, alisema ukisoma taarifa za Escrow, zinaonesha wazi kuwa BoT ilikuwa wakala wa kutunza fedha hizo ambapo TANESCO na Serikali walisaini hati kama sehemu ya wabia wakiwa walipaji wa umeme kwa IPTL.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ambazo gazeti hili iliziona zinaonesha makubaliano hayo yalifikiwa Julai 5, 2006 na kila upande uliwakilishwa na wahusika, kutia saini ambapo kwa upande wa Serikali alisaini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara wakati huo, Arthur Mwakapugi.

Taarifa hiyo ilionyesha kwa upande wa IPTL alisaini aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Datuk Baharuden Majid na upande wa BoT, alisaini aliyekuwa Gavana Mkuu, marehemu Daudi Balali kama wakala wa kuhifadhi fedha hizo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ikiwa ni maelekezo ya mahakama, ilielezwa kuwa mgogoro utakapoisha kati ya wabia, BoT itatoa fedha zote ilizokuwa inazihifadhi katika akaunti hiyo kwa mujibu wa hati husika ya makubaliano kwa ajili ya malipo ya uuzaji wa umeme kwa TANESCO.

Kwa upande wake, mbunge mwingine kutoka mkoani Tabora, ambaye alikuwa na mbunge mwenzake kutoka Mkoa wa Pwani, alisema ukilitazama Bunge kwa umakini limeanza kugawanyika.

“Kuna wafanyabiashara waliokosa vitalu vya gesi wamekuja na yao ndani ya Bunge ili wamwajibishe Waziri wa Nishati na madini kwa maslahi yao na wengine walikuwa wanatoa ushauri wa kisheria katika suala hili,” alisema mbunge huyo.

Aliongeza kuwa, Serikali inapaswa kuwa makini na kuhakikisha inasimama imara kuelezwa ukweli wa jambo hilo kwani anaamini kinachofanyika ndani ya bunge ni hasira za watu.

Chanzo:Majira

Nati za masaburi yako zimekufyatuka sasa unahara tu! Na huo mgawo wa hela toka akaunti ya Rugemalira ile ya libenki la mkomboti ni uzushi pia! Ma.vi ya.ko mb.wa wewe!
 
Back
Top Bottom