Akaunti ya Escrow yafichua mazito

Akaunti ya Escrow yafichua mazito

Majira tena hiyo habari....bora Majira ya kupanga uzazi...bring back our money
 
watanzania tunajazwa chuki ya ajabu ni hatari kilichoandikwa na majira ni sahihi kabisa kama inafikia fitina kwa ajiri ya kukosa kitu ni hatari au kwa kuwa kuna mtu anataka kugombea urais huyo anayefanya vitina hiyo ni kumuogopa kama ukoma huyo aliokosa gass ndie alieifirisi bank ya NBC mpaka ikauzwa chee.
kwanini mtu huyo asijadiliwe bungeni? nawaombeni wabunge msipandikizwe chuki ni hatari

Si bure! huo mtonyo wa escrow umekupitia
 
Matumaini yangu yapo kwako kaka Zitto na team yako ya PAC. Nyie ndio mtakaotutoa katika mtihani huu unaotaka kufunikwa kwa dhulma kabisa.

Kumtegemea Zitto ni kupoteza muda tu, ninakuhakikishia katika hili suala Zitto hatakuja na kitu unachokitarahia ba ishara ziliisha anza kuonekana tangu juzi na jana kwani kauli zake zilionyesha wazi mwisho waje utakuwa upi na ndio maana wakati anaongea pale bungeni Werema alikuwa anafurahi na kutikisa kichwa kwa ishara ya kukubali anachoongea Zitto
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru kwa maelezo, sasa leteni basi hiyo ripoti bungeni ili mambo yaishe basi sio mnaishia kujinyeanyea.

Kwa kweli kama tunao wabunge wenye uelewa mdogo kama hao waliotoa maoni yao kwenye hilo gazeti la nipashe ni lazima nikubaliane na mch. Msigwa kuwa haitatokea akili ndogo kuongoza akili kubwa. Na hili linachangiwa na ccm yenyewe kutuwekea wabunge wa madarasa ya saba na chini ya hapo bungeni. Hwa bado wanaamini haipo hela ya serikali iliyopotea. Pia hadi sasa wanaamini alielipwa hayo mabillion ni Iptl sio PAP. Hata hawaelewi acc. ya escrow huko b.o.t iliendelea kuwekwa na hela za malipo ya umeme uliouzwa kwa tanesco badala ya kufungua separate acc. Na hili lilifanyika makusudi. Pia hawaelewi PAP walinunua hisa pamoja na madeni. Hivyo hivyo tanesco waliwafungulia kesi ya madai Iptl mahakama ya kimataifa kwa kuwa ilikujagundulika walikuwa wanatozwa zaidi kwenye capacity charges. Hawaelewi pia hata b.o.t hawakuwa na haki ya kuruhusu fedha hizo kuchukuliwa wakielewa hukumu ya kesi ya tanesco iliyokuwa marekani haijaamuliwa. Hivyo hivyo kwa mwanasheria mkuu,Waziri wa nishati na katibu mkuu wake. Kwa waziri mkuu ni kushindwa kuzuia wizi huo na taifa kupata hasara.Ripoti itatolewa 26/11 bungeni na wote kujadiliwa na mtaelewa uwezo wa hao wabunge wenu na wachangiaji wa aina yao humu jukwaani.
 
huyo mbunge ni yai viza! analalamika nini sasa? nani anafanyiwa uonevu hata kabla ya mjadala? so asubiri mjadala aende bbungeni aseme anachokijua? kwa nini hataki jana lake litajwe wakati wenzake wanaongea hadharani? hii habari kama ya mshiko vileee! Nani sijui alikuwa zamu majira
 
Hili gazeti la majira nisha acha kitambo kulisoma...hii habari imekaa kiudaku, kwanini wanaficha majina kama wanajiamini na wanalokisema!...bringbackourmonies...full stop!!!
 
Ndio maana kwenye katiba tulitaka wabunge wawe na level fulani ya elimu tofauti na ilvyo sasa kwa sababu kama nikweli huyo aliyenukuliwa ni mbunge basi atakuwa ni wale wa darasa la nne
 
Unadhani Benki Kuu na kwenye madarakamakubwa ya maamuzi wanakaa watu waliokimbia shule na kukimbilia madufu.

Baada ya kushuhudia wahusika wengi wa EPA akina Maranda na pacha mwenzake tena wasiokuwa na elimu yoyote zaidi ua UKADA wa chama walivyochota Mabilioni kwa nini na wao tena Wasomi wasioneshe Usomi wao??

Jibu hoja wewe kinyago? Watu wenyewe ufauru wenu ni wa kuiba mitihan, kwani nani ajui. Ndio maana Hamna competency wala integrity. Vibaka wakubwa. Precidents za takataka zenu ziko wazi, miramba, yoona, etc
 
Kumtegemea Zitto ni kupoteza muda tu, ninakuhakikishia katika hili suala Zitto hatakuja na kitu unachokitarahia ba ishara ziliisha anza kuonekana tangu juzi na jana kwani kauli zake zilionyesha wazi mwisho waje utakuwa upi na ndio maana wakati anaongea pale bungeni Werema alikuwa anafurahi na kutikisa kichwa kwa ishara ya kukubali anachoongea Zitto

Acha chuki za kichadema dhidi ya mh zitto wewe, kile ni kichwa an huw hakikosei. Subiri uone matokeo ndo utajua yeye ni nani
 

WAKATI Bunge likijiandaa kusomewa ripoti ya uchunguzi wa Akaunti ya Escrow bungeni Mjini Dodoma, ripoti hiyo imezidi kuwapasua vichwa wabunge baadhi yao wakienda mbali zaidi na kudai wamebaini ukweli wa fedha hizo.

Hatua hiyo inatokana na taarifa zinazodai malipo ambayo yanalalamikiwa kufanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Kampuni ya Independet Power Supply Limited (IPTL), yalikuwa halali si ya fedha za umma.

Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya wabunge wanaodai kupata yaliyomo kwenye ripoti hiyo kuhusiana na malipo hayo, zinasema wabunge wengi wamefahamu ukweli na kinachofanyika ndani ya Bunge ni kupotosha ukweli kwa maslahi ya wachache.

Wakizungumza na gazeti hili, mmoja wa wabunge hao ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kinachoweza kufanyika sasa ndani ya Bunge ni uonevu kwa kuwa BoT ililipa malipo halali kwa IPTL na taarifa ziko wazi.

“Nimeipata ripoti ya CAG na taarifa zingine, nimezisoma kwa umakini mkubwa na kubaini kilichopo ni vita ya madaraka, kuna wakati tunafuatwa na watu ili tuwawajibishe viongozi hasa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,” alisema.

Alidai kuna baadhi ya wabunge ambao wamejiridhisha kuwa malipo hayo yalilipwa ili kutekeleza makubaliano kati ya IPTL na Serikali ambapo BoT ilichaguliwa kama wakala wa kutunza fedha.

Alisema hali hiyo ilitokana na uwepo wa mgogoro wa kimaslahi kati ya wabia wa IPTL ambao ni kampuni ya VIP (ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa) inayomilikiwa na James Rugemalila na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia (ilikuwa inamiliki asilimia 70).

Mbunge huyo alisema taarifa zinaonyesha kwamba Mahakama Kuu iliamua pande zote mbili VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano (MoU) juu ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi ya umeme, ambayo IPTL inauzia TANESCO.

Aliongeza kuwa, nyaraka zinaonesha mahakama ilielekeza malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti maalumu hadi mgogoro utakapoamriwa kati ya wabia hao ambao walikubaliana kufungua akaunti ya pamoja BoT na akaunti hiyo kuitwa Escrow.

“Ukitazama kwa umakini, kinachofanywa ni kumuonea Pinda kwa sababu ya upole wake, kuna watu wanaamini atagombea urais hivyo wanataka kumharibia,” alisema mbunge mmoja kutoka mkoani Morogoro.

Mbunge mwingine kutoka Dodoma, alisema ukisoma taarifa za Escrow, zinaonesha wazi kuwa BoT ilikuwa wakala wa kutunza fedha hizo ambapo TANESCO na Serikali walisaini hati kama sehemu ya wabia wakiwa walipaji wa umeme kwa IPTL.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ambazo gazeti hili iliziona zinaonesha makubaliano hayo yalifikiwa Julai 5, 2006 na kila upande uliwakilishwa na wahusika, kutia saini ambapo kwa upande wa Serikali alisaini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara wakati huo, Arthur Mwakapugi.

Taarifa hiyo ilionyesha kwa upande wa IPTL alisaini aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Datuk Baharuden Majid na upande wa BoT, alisaini aliyekuwa Gavana Mkuu, marehemu Daudi Balali kama wakala wa kuhifadhi fedha hizo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ikiwa ni maelekezo ya mahakama, ilielezwa kuwa mgogoro utakapoisha kati ya wabia, BoT itatoa fedha zote ilizokuwa inazihifadhi katika akaunti hiyo kwa mujibu wa hati husika ya makubaliano kwa ajili ya malipo ya uuzaji wa umeme kwa TANESCO.

Kwa upande wake, mbunge mwingine kutoka mkoani Tabora, ambaye alikuwa na mbunge mwenzake kutoka Mkoa wa Pwani, alisema ukilitazama Bunge kwa umakini limeanza kugawanyika.

“Kuna wafanyabiashara waliokosa vitalu vya gesi wamekuja na yao ndani ya Bunge ili wamwajibishe Waziri wa Nishati na madini kwa maslahi yao na wengine walikuwa wanatoa ushauri wa kisheria katika suala hili,” alisema mbunge huyo.

Aliongeza kuwa, Serikali inapaswa kuwa makini na kuhakikisha inasimama imara kuelezwa ukweli wa jambo hilo kwani anaamini kinachofanyika ndani ya bunge ni hasira za watu.

Chanzo:Majira
majira gazeti la mafisadi. ucrudie kuweka hilo gazeti hapa. onyoooooooooo
 
cha msingi wasiishie kujiuzulu tu bali wanatakiwa washitakiwe na kisha wanyongwe, maana tumezoea kuona ccm kila uchaguzi unapokaribia lazima kutokee wizi mkubwa wa mali ya mali umma, na kisha walioba huishia kujiuzulu tu, huku wakibeba mamilioni ya fedha, jamani viongozi wa ccm ifike hatua muwe na huruma hospitali hazina dawa, hakuna maabara hata za kupima tezi dume kama ugojwa wa mh,,,,,k,,,,,lakini mnadiliki kula mamilion ya fedha bila from no reason?? duh,,,navumilia kuwa mtanzania lakini sijivunii kuwa mtanzania
 
watanzania tunajazwa chuki ya ajabu ni hatari kilichoandikwa na majira ni sahihi kabisa kama inafikia fitina kwa ajiri ya kukosa kitu ni hatari au kwa kuwa kuna mtu anataka kugombea urais huyo anayefanya vitina hiyo ni kumuogopa kama ukoma huyo aliokosa gass ndie alieifirisi bank ya NBC mpaka ikauzwa chee.
kwanini mtu huyo asijadiliwe bungeni? nawaombeni wabunge msipandikizwe chuki ni hatari

Mzee mengi na Mkono pia wahindi wenye mgongano wa kimasilahi na sings singasinga wa IPTL ndiyo walichanga Pesa wakampa Kafulila na Zito wapaze Sauti wakiamini Maswi na Prof mugongo watang'oka Wizara ya Nishati ili Mengi akajimegee Vitalu vya Gesi huku Mkono akirejeshewa Tenda za kisheria ambazo amenyang'anywa na kujenga Chuki na waziri, Bunge wanapaswa wajadili ni kwa nini NBC Bank iliyumba? Huyo mengi alikopa mapesa mengi huko kisha akaanzisha viwanda vya Levola na komesha nk, hakurejesha hizo Pesa bali alikupa njama na wafanyakazi wa NBC wasio waaminifu wakaziiba nyaraka za kumbukumbu za mikono kisha zikachomwa moto hadi Leo NBC inayumba hivi kwa nini Bunge hakijafika hiki?
 
Wapo watu wenye Uchungu na hizo pesa na hasa wananchi , Likini Zito na Kafulila wao wapo after money Kwani sasa wanafanya kazi kwa maelekezo ya Mkono na Mengi ambaye anamchukia sana waziri baada ya kumnyima Vitalu vya Gesi,huku Mkono akiwa na hasira naye kwa kunyang'anywa Tenda zote za kisheria , huu mgongano wa masibani , mengi anatumia hii fursa ili Wananchi na wabunge Wamsaidie kumng'oa Prof Mhongo haraka kisha yy atawahi Mtwara akajimegee Ardhi kiulaini na kujimilikisha Vitalu vya Gesi kiulaini, mengi Hana Uchungu na pesa hizo yy anausongo na Vitalu vya Gesi tu.
 
Acha chuki za kichadema dhidi ya mh zitto wewe, kile ni kichwa an huw hakikosei. Subiri uone matokeo ndo utajua yeye ni nani

Vipi kuhusu MABILIONI YA USWISS alipatia na ile issue imeishia wapi? na tangu ameanza kuzalisha hoja Bungeni ni ipi iliishawahi kumature na kuleta Product yenye manufaa kwa taifa
 
Vipi kuhusu MABILIONI YA USWISS alipatia na ile issue imeishia wapi? na tangu ameanza kuzalisha hoja Bungeni ni ipi iliishawahi kumature na kuleta Product yenye manufaa kwa taifa

Wewe ni ZOMBI aisee nakufananisha na MCHAWI anayewanga mchana
Sis tunaongelea maslahi mapana ya nchi ww unaleta Ushabiki wa kichadema hapa SHETAN mkubwa na ulaaniwe .mbona VIDEO ya mbowe kule Soweto ujamuuliza iko wapi wakati alisema anao ushahidi
 
magazeti ya udaku bhana,eti mbunge mmoja ambae hakupenda jina litajwe! mwaga hadharani tujue nani ni nani na ana mwelekeo gani ili tumhukum ktk sanduku la kura,upole wa pinda usitufanye tumwonee huruma apigwe tu na ajiuzulu,hapana taka jitu oga hivi na nafiki likipewa nchi tutauzwa
 
Back
Top Bottom