Akamatwa kwa kuchezea mifumo ya vidhibiti mwendo vya mabasi ili madereva waendeshe kwa kasi kubwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Issa Said Mbogo ambaye ni fundi wa vifaa vya umeme anashikiliwa kwa tuhuma za kuchezea vifaa vya kudhibiti mwendo kwenye mabasi (VTS) akidaiwa kuwa anavuruga mifumo hiyo ili madereva wa mabasi waendelee kwenda mwendo kasi.

Mtuhumiwa amekamatiwa Nzega Mkoani Tabora wakati wa oparesheni maalum.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Wilbroad Mutafungwa ameagiza kufunguliwa jalada la uchunguzi baada ya kupata malalamiko mengi kuhusu mtuhumiwa na akibainika anahusika atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: Azam TV
 
Badala ya kumwajiri serikalini ili asaidie kudhibiti mambo kama haya badala yake atapigwa miaka mingi jela mpaka afie huko
 
Issa Said Mbogo ambaye ni fundi wa vifaa vya umeme anashikiliwa kwa tuhuma za kuchezea vifaa vya kudhibiti mwendo kwenye mabasi (VTS) akidaiwa kuwa anavuruga mifumo hiyo ili madereva wa mabasi waendelee kwenda mwendo kasi.

Mtuhumiwa amekamatiwa Nzega Mkoani Tabora wakati wa oparesheni maalum.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Wilbroad Mutafungwa ameagiza kufunguliwa jalada la uchunguzi baada ya kupata malalamiko mengi kuhusu mtuhumiwa na akibainika anahusika atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: Azam TV
fundi bila kazi kazi bure,hapo wachunguzwe na maboc au madereva ndiyo walimpa kazi.Ushauri
 
Back
Top Bottom