Ajutia kugawa namba ya simu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAMKE mmoja [31] mkazi wa Ukonga Madafu, amejikuta akikosa amani ndani ya nyumba yake kutokana na kitendo chake cha kugawa namba yake ya simu ya mkononi kwa mwanaume anayemfahamu mbele ya mume wake.

Mwanamke huyo jina kapuni amejikuta akikosa raha kutokana na kusumbuliwa na mume wake huyo akimshinikiza kuwa mwanaume huyo alikuwa na mahusiano nae.


Alidai kuwa Januari 12 mwaka huu, akiwa maeneo ya Mwenge aliweza kukutana na mwanaume huyo aliyesoma nae chuo cha CBE miaka minne iliyopita na waliweza kuzungumza na baadae kumuomba namba ya simu ya mkononi na kumpatia bila kumuomba ruhusa mume wake huyo.


Hivyo bila kutambua kuwa mume wake kitendo hicho alikuwa hajakiafiki na waliweza kuagana na mwanaume huyo huku kila mmoja akiahidi kuwa wawe wanawasiliana.


Alidai mara baada ya kuachana na mwanaume yule mume wake alibadilika na kila anapomsemesha alikuwa hapati majibu sahihi na alikuwa akimjibu vibaya hali iliyomshangaza na hakutambua mume wake alibadilishwa na nini.


Alidai walipomaliza mizunguko yao waliweza kurudi nyumbani na usiku mume huyo alianza kumuuliza maswali kuhusiana na mwanaume aliyempatia namba yake ya simu.


Hata hivyo juhudi za dada huyo kujielezea kwa mume wake hazikuzaa matunda na huku akishinikizwa kuwa yule alikuwa ni mpenzi wake iweje alikuwa akimsisitiza wafanye mawasiliano.


Mwanamke huyo alidhani huenda yalikuwa yameisha na mume wake alisubiria kukuche haraka na alipotoka kazini alikwenda kuripoti tukio hilo kwa kaka wa mke wake akidai alimvunjia heshima na kuongea na mabwana zake mbele yake huku akimtaka shemeji yake amuite na kufanya kikao cha kumuonya.


Hata hivyo dada huyo alionywa na kaka zake wakiwemo na dada zake hali iliyomfanya akose raha na kuonekana anatoka nje ya ndoa kitu ambacho hakikuwa sahihi.


Hadi kufika jana mwanamke huyo alikuwa hajarudishiwa simu yake ya mkononi na simu hiyo alikuwa akitembea nayo mumewe kwa kufanya uchunguzi zaidi wa uaminifu dhidi ya mkewe.
 
namba ya simu ndo kuwadi maarufu siku hizi..kuna wataalamu ukitoa namba ya simu tu basi mchezo umeisha
 
Huyo mume nae anaonekana hajiamini kweli!Kutoa namba tu tena mara moja tayari imekua kesi ya kuhusisha watu wengine?Hovyo sana!
 
nadhani alitakiwa kumshirikisha mumewe katika hilo bila ya kukurupuka, kila mtu analinda mali yake bwana,bora uitwe haujiamini kuliko ukajifanya unajiamini halafu watu wanakuona b.w.e.g.e.
nimefikiria ingekuwa mimi ingekuaje? bwana ako anaomba namba ya simu au anagawa namba ya simu mbele yako kwa mawasiliano zaidi,bila ya kushirikishwa. huyo mwanaume angekuwa hayupo kipindi wanapeana namba hapo kweli, ila kwasababu alikuwepo alitakiwa kushirikishwa.
 
nadhani alitakiwa kumshirikisha mumewe katika hilo bila ya kukurupuka, kila mtu analinda mali yake bwana,bora uitwe haujiamini kuliko ukajifanya unajiamini halafu watu wanakuona b.w.e.g.e.
nimefikiria ingekuwa mimi ingekuaje? bwana ako anaomba namba ya simu au anagawa namba ya simu mbele yako kwa mawasiliano zaidi,bila ya kushirikishwa.

Tatizo lipo kwenye kushirikisha watu wengine?Kilimshinda nini kukaa na mke wake nyumbani wakayamaliza??Kaniboa kweli kwa hilo!
 
Wanawake wa Tanzania mtajikomboa lini na hivyo vijidume vyenye wivu wa kitoto kiasi hicho? A man shouldnt be a cry baby.That behavior suit better to women.
 
Wanawake wa Tanzania mtajikomboa lini na hivyo vijidume vyenye wivu wa kitoto kiasi hicho? A man shouldnt be a cry baby.That behavior suit better to women.

My point exactly!Huyo mwanaume hajiamini kiasi gani mpaka kutoa namba ya simu iwe issue ya kuwekeana vikao?
 
kuna hoja ilikuwa hapa jana kuwa , wanawake wanaoolewa wakiwa sio mabikira wanaonekana kama walikuwa malaya na hapa ni exactly kinachotokea, huyo jamaa kama angekuwa ndio kavunja yeye mlango wala asingekuwa na wivu wa kihivyo, lakini ukikuta njia ilishafuguliwa basi kila siku unaona waliofungua wanajikumbusha
lakini pia katika maisha ya ndoa watu wanapaswa kuwa makini sana na hizi simu za mkononi, nyumba nyingi zinayumba kutokna na simu hizo,
 
TUsimlaumu sana huyu mwanaume yeye ndo anajua tabia za mkewe jamani!! huenda ana ka tabia kabaya
 
He is insecure! Kuwasiliana na mtu si kukumbushia, mbona wengine tunawasiliana na ma-x wetu na tupo huru tu! Mi naona taizo hawa watu hawapo wazi kuhusu mahusiano yao ya sasa na yaliyopita.
 
haa! Ushamba gani huu. Naona huyo mume mwenzetu hajasoma hata ngumbaru
 
jamani tusilaumu mwanaume sana kuna mazingira unakuta upo na mke gafula anakutana na rafiki yake unashangaa gafula mkeo anamrukia waoo na yule kajiandaa kupokea waoo wanakumbatiana taiti wanazungushana wee kama dk kadhaa we upo pembeni unaangalia 2 gafula yule kijana anahisi kama mpo wote anaomba no yako cm unampa anaondoka mkeo anakufata mwendelee na safari uku kafurai sana anakwambia yan yule alikuwa clac mate wangu ebu niambie hapo ss
 
Kwa mawazo yangu, wanawake ndio wanaleta hii tafurani, hivi nyie mwishakutana na mwanamke hata kuongea na mtu uliyesoma naye hataki, hacha marafiki wa kiume ambao anasema ndio makwadi. The main problem sio kwa mtu binafsi but kwa tabia za watu wote wanaume na wanawake. Wanawake wanatakiwa kujikomboa kwanza na kuacha kufikiri kuwa akiolewa mwanaume anaacha kuwa na marafiki even differenet sex as long they don't have love relationship. Then I think huyo mwanaume asingefikia hapo kama na yeye angekuwa huru to that extent. But the mistake he made was involving other persons in his business, yeye angemalizana na mke wake then yakaisha.
 
Back
Top Bottom