Ajiua Kwasababu ya Penzi la Mwanaume Mwenzie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajiua Kwasababu ya Penzi la Mwanaume Mwenzie

Discussion in 'International Forum' started by Mbonea, Oct 9, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Shoga Matt Lucas kushoto akiwa na mume wake wa zamani Kevin McGee ambaye amejiua

  Ndoa za mashoga zimezua jambo nchini Uingereza baada ya mume wa shoga kujiua baada ya ndoa yao kuvunjika na mkewe kuchukuliwa na mwanaume mwingine.


  Ndoa ya jinsia moja imesababisha mwanaume ajiue baada ya kukimbiwa na "Mkewe" (Mwanaume mwenzie, shoga) ambaye baadae alianza mapenzi na mwanaume mwingine.

  Mchekeshaji maarufu wa nchini Uingereza Matt Lucas ambaye ni shoga alifunga ndoa na mpenzi wake Kevin McGee mwaka 2006 katika harusi ya kukata na shoka iliyohudhuriwa na mastaa wengi wakubwa wa Uingereza.

  Lakini ndoa hiyo ya jinsia moja ilivunjika mwaka jana na kuwa ndoa ya kwanza ya watu wa jinsia moja kuvunjika tangia ndoa za watu wa jinsia moja ziliporuhusiwa nchini Uingereza mwaka 2005.

  Sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo ni mchekeshaji Matt Lucas kushindwa kuvumilia matumizi ya madawa ya kulevya ya mumewe.

  Kevin ambaye alikuwa na umri wa miaka 32, alizidisha matumizi ya madawa ya kulevya baada ya kuachana na Lucas na baada ya kuona Lucas amepata mwanaume mwingine Kevin aliamua kujiua.

  "Kifo ni bora kuliko kuendelea kuishi" ndio ujumbe wa Kevin aliouacha kwenye ukurasa wake wa Facebook masaa machache kabla ya kujiua.

  Mwili wa Kevin ulikutwa nyumbani kwake mjini Edinburgh baada ya polisi kutaarifiwa juu ya ujumbe wa Kevin wa kujiua kwenye Facebook.

  Matt Lucas ni maarufu kwa vichekesho vyake hasahasa katika kipindi anachoshiriki cha "Little Britain" wakati Kevin alikuwa mtayarishaji wa vipindi kwenye luninga nchini Uingereza.

   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  The place he has currently gone to, is the best for him. Acha aende huko! Mshahara wa dhambi ni mauti, na huyo aliyemkimbia mwenzie atajinyonga kwasababu penzi atakalopata kwa huyo bibie mpya halitamtosha! lol!
   
Loading...