Hivi hata anachoongea anakijua kweli.
Jamani kwani kutoka Mbeya kwenda Butiama ni mbali kiasi gani? Ajitokeze mtu mmoja hapo Kyela ampatie Mzee nauli aende tuone atakavyomfufua huyo Nyerere kwa hiyo funguo. Kwa nini tujaze server ya JF juu ya kitu kinachoweza kuthibitishwa kuwa ni ukweli au uongo.
Tiba
Anataka akanywe juice Ikulu huyo.
Tiba hapo kuna mtu wa kufika huku butiama kweli
au akifika atakuwa hoi kwenda kulaza tu hosp.
Huwezi jua Bwana huyo Mzee hajawahi kupanda ndege na anajua ili kuwezeshwa kufika Butiama, lazima apate chance ya kukwea pipa. Wazee wengine wajanja sana. Na sijui kufufua mtu kuna uhusiano gani na ufunguo!!!!
Tiba
ilisivyowezekana kumfufua nyerere ndivyo ilivyo ngumu kwa CCM kushinda uchaguzi 2015
Sim'bishii huyo babu anasema kweli kabisa, hivi hamjui kwamba hii nchi inaongozwa na mizimu? 75% ya viongoz wa CCM na serikali yao wote ni mizimu tu, wenyewe walishakufa muda mrefu sana na hii iliyopo sasa ni mizimu yao!
MAAJABU YA MBEYA HEBU SOMA HII KWA MAKINI KABISA.
Huyu mzee alifika katika studio za Kyela FM,
anasema yeye anahitaji Msaada anataka kwenda kumfufua Mwl. Julius Kambarage Nyerere baba wa Taifa aliyefariki Miaka 15 iliyopita,
Na huo ufunguo ameushika mkononi ndiyo wa kumfufulia!
Madai yake mzee huyu anasema anaenda kumfufua na Mwalim ndiye atakuja kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015.
Na pia anaibashiria CCM kuwa mshindi atatoka katika chama cha CCM.
Mimi nitamwamini endapo atafanikiwa kufufua uchumi wake kwanza.Sura yake inaonyesha uchumi wake ulikufa zamani.Hii ni njaa na ni mchawi kama wachawi wengine,namshauri atumie ungo kama anaweza kufufua mtu, badala ya kusubiri kuwezeshwa.