Ajira Zanzibar ni kwa Wazanzibar pekee?

Ajira Zanzibar ni kwa Wazanzibar pekee?

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,438
Nimekuwa nikifatilia matangazo ya ajira kupitia ZBC (TV ya z'bar) cha ajabu nimeona kigezo cha kwanza kutajwa ni lazima mwombaji awe Mnzanzibar.

Nashindwa kuelewa hili limekaaje hasa ukizingatia masuala ya muungano? Ni kwamba mtu wa bara hana haki ya ajira huko visiwani kwa sababu nafaham kuna wazanzibar wengi tu wanaajiriwa bara.
 
umeleta swali zuri kijana, mimi kama mzanzibari ntakujibu hivi, muungano wa tanzania umetokana na serikali mbili nazo ni SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR na SERIKALI YA TANGANYIKA, nin maana yake? ni kwamba kila mtu ana serikal yake na kila serikal ina wananchi wake, ina mipaka yake, ila tatizo linatoka hapa RAIS wa kwanza wa TANGANYIKA, Mwalimu Julius Nyerere hakutaka kuwepo na serikal ya TANGANYIKA, na hili ni tatizo kuu alitaka iwe nchi moja, bahati mbaya ZANZIBAR hawakupenda kusalimisha mamlaka yote, nisifahimke vbaya kuwa 'kila mzanzibari ni mtanzania lakin sio kila mtanzania ni mzanzibar' tufaham mantik kwanza na sio ugomv au madongo.
 
Mtanzania sio mzanzibar ila mzanzibar ni mtanzania so uwezi kupata kazi zanzibar wakati wewe sio mzanzibar
 
Mimi nina rafiki yangu mhasibu na anafanya kazi huko.. acheni chuki zenu dhidi ya wazanzibar,, kama wakenya wanafanya kazi kule na wataliano iweje wa bara asifanye? ila off course kuna posts lazima zihifadhiwe kwa ajili native zanzibarians
 
Tanzania kuna uraia wa aina mbili.

1. Ni raia wa Tanzania ambae ni mtanganyika na mzanzibar.

2. Ni raia wa Zanzibar ambae ni mzanzibar pekee yake mwenye haki ya kuchagua Rais na wajumbe wa baraza la wawakilishi.Mwenye haki ya kununua na kuuza ardhi au kiwanja katika nchi ya Zanzibar amabayo mipaka yake imeainishwa katika katiba ya Zanzibar.Kwakuwa raia wa Zanzibar pia ni raia wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania pia wana haki ya kuchagua Rais wa JMT ,wabunge na madiwani huku Tanganyika iwapo watakuwa wamejiandikisha eneo lolote la nchi ya Tanganyika,hawatakuwa na masharti yoyote ya kuwazuia.Pia watakuwa na haki ya kununua na kuuza ardhi au kiwanja sehemu yoyote ya nchi ya Tanganyika kwakuwa wana uraia wa Tanzania.

3. Hakuna uraia wa Tanganyika kuna uraia wa Tanzania hivyo mtanganyika ana haki ya uraia awapo Tanganyika tu akienda Zanzibar hana haki ya kununua au kumiliki ardhi au kiwanja,hana haki ya kuajiriwa katika nchi ya Zanzibar.

Katiba mpya iliyopendekezwa na Jaji Warioba ilikuwa na majibu ya kuondoa hii kero ya waTanganyika kuonewa wawapo katika nchi ya Zanzibar.

Tafakari chukua hatua ikatae CCM kwakuwa imeshindwa kuwaeleza ukweli waTanzania juu ya kero hii mbaya.
 
umeleta swali zuri kijana, mimi kama mzanzibari ntakujibu hivi, muungano wa tanzania umetokana na serikali mbili nazo ni SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR na SERIKALI YA TANGANYIKA, nin maana yake? ni kwamba kila mtu ana serikal yake na kila serikal ina wananchi wake, ina mipaka yake, ila tatizo linatoka hapa RAIS wa kwanza wa TANGANYIKA, Mwalimu Julius Nyerere hakutaka kuwepo na serikal ya TANGANYIKA, na hili ni tatizo kuu alitaka iwe nchi moja, bahati mbaya ZANZIBAR hawakupenda kusalimisha mamlaka yote, nisifahimke vbaya kuwa 'kila mzanzibari ni mtanzania lakin sio kila mtanzania ni mzanzibar' tufaham mantik kwanza na sio ugomv au madongo.

Uko sawa mno mkuu,mimi ni m bara niko huku Mwanza cha msingi endeleeni kuwanyima ajira kwa sababu huku bara ajira na kazi ni nyingi lakini wanakimbilia visiwani huko ambako hakuna dili lolote.
 
.

Tafakari chukua hatua ikatae CCM kwakuwa imeshindwa kuwaeleza ukweli waTanzania juu ya kero hii mbaya.

CCM hatuitaki lakini Lowassa ndio hatumtaki kabisa!!!!!!Nona UKAWA wametunyima "Option" hapa bora kubaki na Magufuli
 
Kila mzazibar ni mtanzania... Lakin sio kila mtanzania ni mzanzbar..ushanifahamu?? .....mzazibar kupata kazi bara ruksa but sio mbara kujipeleka znz.
 
Nimekuwa nikifatilia matangazo ya ajira kupitia ZBC (TV ya z'bar) cha ajabu nimeona kigezo cha kwanza kutajwa ni lazima mwombaji awe Mnzanzibar.

Nashindwa kuelewa hili limekaaje hasa ukizingatia masuala ya muungano? Ni kwamba mtu wa bara hana haki ya ajira huko visiwani kwa sababu nafaham kuna wazanzibar wengi tu wanaajiriwa bara.

Mkuu hilo umelijua leo? mbona bila kulalamika tulikuwa tunakwenda kwa passport na kuchekiwa/kupekuliwa kama mgeni mwingine yoyote ila wao walikuwa wanakuja bila passport na hata wakati wa kurudi kama umenunua vitu baadhi wanakunyang'anya hii ilimkuta dada yangu alinyang'anywa mpaka sabuni akaja na tutakataka tu.nashukuru siku hizi hakuna bugudha hizo bado ajira tu ndio ngumu kupata.
 
umeleta swali zuri kijana, mimi kama mzanzibari ntakujibu hivi, muungano wa tanzania umetokana na serikali mbili nazo ni SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR na SERIKALI YA TANGANYIKA, nin maana yake? ni kwamba kila mtu ana serikal yake na kila serikal ina wananchi wake, ina mipaka yake, ila tatizo linatoka hapa RAIS wa kwanza wa TANGANYIKA, Mwalimu Julius Nyerere hakutaka kuwepo na serikal ya TANGANYIKA, na hili ni tatizo kuu alitaka iwe nchi moja, bahati mbaya ZANZIBAR hawakupenda kusalimisha mamlaka yote, nisifahimke vbaya kuwa 'kila mzanzibari ni mtanzania lakin sio kila mtanzania ni mzanzibar' tufaham mantik kwanza na sio ugomv au madongo.
Wazanzibar wekeni akiba ya maneno.

Mnaongea sana kiasi cha kushindwa kujua mnaongea nini.

Hii nukuu naomba uihifadhi maana ipo siku utaisoma tena sijui ni kwa namna ipi lakini utaisoma, trust me

Wznz mumesahau mlikuwa vinara wa kuvunja muungano! Leo mna mtima huo tena? Leo kuna mtu anayenyanyua pua kusema muungano uvunnjike. Watanganyika si waliwaambia njia nyeupe, leo mznz gani ana mtima huo

Tanganyika si tuliwaambia harakisheni, mbona leo hamjaondoka

Ngoja tushughulike na mambo ya sasa , hili ni kiporo .

Tunachosema mpime maneno maana ndiyo yaliyojenga hasira na hasara mnayo ninyi.
 
nina mashaka na ufaham wako, unaendeshwa aidha na mihemko au chuki binafsi, bahat mbaya sijaandika lolote lenye kuashiria nataka kuvunja muungano, sijaandika kama nataka muungano uendelee, sijaandika kwa chuki ya mzanzibar au mtanganyika, nlichofanya ni kutoa definition au maana ya muungano ulivo hali yake na hata katiba inasema hivyo, iulize katiba mkuu.
na jengine simo jamiiforum kujibu kila linaloandikwa ila natoa maelezo, pole yako mkuu soma tena au tafuta miwan uangalie ulichonijibu wapi limetoka kwenye comment yangu, " I am responsible for what i have said AND not what you have thought" pole , pole, pole naamin ungeweka hakiba ya maneno na kuifaham comment yangu ungefanya busara lakin haraka imekudhalilisha
 
Zanzibar ni kama taasisi binafsi ambayo ipo ktk hatua za awali tangu kuanzishwa kwake, hivyo haina pesa za kuajiri watu toka tz coz uchmu wao bado sana na fursa za ajira ni chache mno mfano znz hakuna kuteach tuition na hapo awali zilipokuwepo ilikuwa ni kama 4500 kwa masomo 11 ya sec. Kwa mwezi, ni mtz gani yuko tayari kufanya ujinga huu?
 
Na nataka kueleza jambo jengine najua kuna watu watanifaham na wengine hawatanifaham, aidha kwa kuwa hawatakubali kwa kuwa hawataki kukubal au hawajafaham vyema na nipo tayar kuwafafanulia,.
Wakati mwengine tufkirie kwa kutumia akili ilokuwa neutral(haifungaman na sehem yoyote) , nataka kutoa mfano wa EAST AFRICAN COMMUNITY, tunashirikiana mambo mengi km WATANZANIA ila kwenye ajira mbona inakua kasheshe kwasaba hatupo tayar wa TANZANIA kuwaruhusu wa KENYA watachukua ajira zetu ambazo mzawa wa kawaida anaweza kuzifanya, hv leo ikichimbwa gesi mtwara halafu vibarua kama waponda zege, wasafishaji barabara, wasafirishaji mizigo, walinzi wa vitalu, nawengineo waajiriwe watu wa kutoka mikoa mengne wakati mtwara kuna vijana hawana ajira na wako tayar kufanya kazi watajiskiaje? utajijibu mwenyeo.
Je afisa wa uhamiaji wa Tanzania aje aajiriwe mkenya au mtu yoyote ambae si mtanzania itakuaje? na mimi ni mzanzibar naish bara kwa kuja kusoma tu na kwetunimemkodisha mtu wa bara nyumba nzima na anafanya kazi KMKM, na pia ni DAKATARI( kiufup huyu mtu hala ana kazi nying sana na amenivutia na ufanisi wake wa kazi), ninaposihi kuna TV imewekwa nje na watu wanaangalia mipira yote ya ulaya bure na hapo nakutana na watu wengi kutoka bara wanakuja kutazama mpira na tumekuwa kama familia , hapo nishakutana na mchungaji, majeshi, vibarua, wapelelezi, wamachinga, wamasai, kiufup ni watu wengi wa bara wapo na wanfanya kazi, na Zanzibar ipo NSSF, TRA, NIDA, NEC, JWTZ, NBC, CRDB, NMB, hizi ni taasis ambazo wamo wa Zanzibar NA watu wa TANZANIA BARA, namalizia kusema huwezi kumuweka mtu katika wizara ya utamaduni Zanzibar kutoka BARA never haiwezekan kwa sababu utamaduni tofauti, na hutoweza kumuweka mZanzibar katika wizara ya utamaduni ya tanzania( tanzania bara kwasabau hili halipo kwenye muungano) halafu ukategemea ataiendesha vzurofisi haitowezekana.
Nimelizie kusema kuna kazi ni kwa wenyeji na kuna kazi kwa wote.
Nafkir nimefahamika
 
Back
Top Bottom