TUACHE SIASA KWENYE TAALUMA
Nimepokea kwa masikitiko makubwa majibu aliyoyatoa leo bungeni naibu waziri anayehusika na TAMISEMI ndugu JAFFO,kwa ujasiri mkubwa mheshimiwa JAFO aliyesimama February wakati wa bunge na kudai serikali imejiandaa kutoa ajira 71,000 zikiwemo za walimu 40,000 leo ameibuka na kihoja kingine ambacho kwa wanataaluma haswa walimu inatakiwa kuungana kwa pamoja kupinga huu ugumashi kwenye sekta ya elimu.
Tumetoka kuwaondoa vijana waliokuwa wakisoma special program pale UDOM kwa kile kilichoitwa walimu vilaza na kwa pamoja tukaona ni mwendelezo mzuri wa serikali yetu ya awamu ya tano kuendeleza sekta hii ya elimu licha ya mbinu iliyobuniwa na Rais wa awamu ya nne na serikali yake.
Sijajua kama mawazo na majibu ya JAFFO niyaserikali au mawazo yake binafsi ,kama ni ya serikali KWA HERI NYERERE KWA HERI ELIMU kama ni ya JAFFO anapaswa kuhakikiwa cheti chake cha elimu kuanzia ngazi ya msingi mpaka chuo kikuu, hatuwezi kuwa na mawaziri wanaoshindwa kutambua kua UALIMU NI TAALUMA INAYOSOMEWA KWA MUDA HUSIKA.
Unapata wapi ujasiri wa kutamka mbele ya halaiki ya watanzania kuwa uwachukue watu waliosoma sayansi na kuwapiga brush ya wiki mbili wakawe walimu na bado ukashangiliwa lazima waziri ajue kuwa kunatofauti kubwa kati ya uelewa na ufundishaji.
Kwanini wanasiasa mnaidharau taaluma ya elimu, kwanini mnataka kuendelea kulitengeneza taifa la watoto wenu( wenye nacho) waendele kutawala watoto wetu (tusionacho). Kipindi masomo ya sayansi mnayafanya kuwa ya lazima mnaleta walimu wa mwendokasi wa sayansi hivi JAFFO ni kweli haujui ualimu ni Taaluma? Ualimu si siasa ambayo mtu yeyote anawezakujaribu. Wiki mbili zinatosha kumfanya mtu awe mwalimu?
Hivi unafikiri kushika chaki ndo kujua kufundisha? Sasa ni wakati wa kugeukia vyeti vya wanasiasa ili kupima uelewa wao kitaaluma lasivyo tunakolipeleka taifa ni kwenye giza tororo………taifa lenye walimu -magumashi kama anaowataka Jaffo aliwezi likapiga hatua na kuifikia Tanzania ya viwanda.
Taifa litaendelea kushuhudia ustawi washule binafsi na kufa kwa shule za jamii huku watoto wa matajiri na mawaziri wakisoma kwenye shule binafsi na watoto wa wasionacho wakiendelea kufundishwa na walimu wa sayansi wa mwendokasi.
Jambo lingine ambalo serikali inapaswa kulitambua ni kutofikiria walimu wa sanaa ni wajinga sana , 1958 mwalimu nyerere alijiuzulu ualimu pale BUGU akiwa anafundisha masomo ya sanaa, maraisi wote waliofuata walikuwa ni wanasanaa(waalimu wa sanaa)kasoro wa awamu hii ya tano, na mawaziri wengi ni wanasanaa tunatoa wapi ujasiri wa kuwadhalilisha hawa walimu wa masomo ya sanaa wenye shahada ambao wangeamua kusomea ualimu wa cheti tayari wangekua kwenye system toka 2012 na kama ni diploma tangu 2015 wangekuwa kwenye system.
Tulitake sasa bunge linaloendelea Dodoma kuitaka serikali itokekauli yake kama ajira zitafunguliwa ama la! Ili vijana wengi wakitanzania tuliokuwa tukizisubiri tujue moja kwamba azipo au zipo ili tuangalie mambo mengine ya kufanya tusikae kusibiri jambo ambalo bado lipo kwenye michakato ambayo mimi niliamini imekufa na serikali ya awamu ya nne. AMA KWELI ALIYESHIBA HAMKUMBUKI MWENYE NJAA.
Na Mwalimu asiye na Ajira
Rucho.
0756231744.