Ajira za TISS hutangazwa wapi?

Ajira za TISS hutangazwa wapi?

Jasusi Evarist Chahali jana kasema kwa mara ya kwanza TISS wametangaza kazi zao.

Mmeona tangazo?
 
Majeshi ya ulinzi na usalama hutangaza nafasi za kazi kama taasisi nyingine. Mathalani Jeshi la polisi, JWTZ, Kikosi cha zimamoto, Uhamiaji, etc wamekua na kawaida ya kutangaza nafasi za mafunzo na hata ajira. Lakini sijawahi kuona tangazo la kazi kutoka TISS (Tanzania Intelligence Security Services) Wana utaratibu gani katika kutoa ajira?
lumumba
 
Hm. Kwa anaeielewa kiuhalisia,hivyo vigezo ni zero kabisa.
Labda TISS wa mchongo.
Kwanza ukielewa maana ya TISS yenyewe,kuna kitu utaelewa. Baada ya hapo,utagundua nani amekidhi vigezo vya kujiunga.
Hapa nikupe mfano mmoja,jeshini mpaka mtu awe MP(Military Police),inakuwaje? Maana hawaokotwi mtaani na kupewa hicho cheo. Hawatolewi mtaani na kupelekwa course ya uMP. Lakini wapo.
Halafu,ikitokea ukabahatika kujua utendaji kazi wao,ndo utagundua ni watu gani,wana ujuzi gani,missions zao zikoje.
Kila nchi lazima iwe nao,lakini hawafai hata kusikika. Na ukikutana na mtu aliewahi kujikwaa akakutana nao,kwanza ukimuuliza ni kina nani,wanafanya nini,kama mmekaa,atainuka bila jibu. Kwa nini?
Hapo hutotamani hata kufahamiana nao.
Popote ulipo,ujue wapo. Na ndo maana ukipenda,mambo yako yafanye kwa utaratibu.
Mijama kama ina mission,hata zege itakologa na kubeba. Makande itakula kama haina akili. Kibarua cha kuchimba choo,itachimba,hata kwa nusu ya bei.
Sasa waokote mtaani wa msaada gani?
Nijuavyo mimi,hawa hata ikitokea wakagundulika,mpaka anakata upepo utamtesa lakini hakwambii ukweli.
Nimetumwa na furani,yuko sehemu furani,ahhhh wapi. Huyo jambazi tu.
Mtaani mtu haongei,eti yule ni usalama wa taifa. Wengine eti nikivaa miwani yangu,watu wananikimbia wanajua mi usalama wa taifa. Teh teh teh
Ila wale utakaosikia wanasemwa au watu wanawahisi,jua tu hao ni wambea. Wapo watu ambao kazi yao ni kukusanya taarifa na kupeleka kituo cha polisi,hata mia hawapewi,sifa tu kuingia ofisi ya mkuu wa kituo,basi. Na yeye anaambiwa nenda kafatilie hiki na kile.
Hicho ni kitengo kipo,lakini hakinaga ukweli,wahusika,hawajulikanagi,wao wenyewe hawafahamiani,wenyewe kama wanawindana,na siku ukiwajua,basi ujue hicho kitengo kimeshaingiliwa na kuvujisha siri zake. Hapo kinakuwa tayari kimeshakua MOSSAD
Jeshini hakuna cheo cha MP
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom