Wana njia kuu 3 wanazotumia ..
( 1. )Wanachukua vijana kutoka Vyuo vikuu, JKT na hata mitaani kwa vigezo wanavyovitaka wao na kwa mahitaji maalum ya kazi ila huwa wanachukuliwa Kimya Kimya na vijana wanaochukuliwa hufanyiwa vetting kisha huchukuliwa. Lakini pia kwenye majeshi ya askari polisi, magereza, JWTZ n.k huchukuliwa yaani hapa mtu utakuta ni polisi lakini hapohapo ni TISS au ni JWTZ hapohapo ni TISS anakuwa anafanya simultaneously role Ila role kubwa inakuwa ni base on TISS.
(2). Kupitia vyama vya siasa jiunge CCM au Vyama vya upinzani na ukiwa huko usibweteke toa hoja kwelikweli, Hoja ziwe za maana you have to be a man of logic na uwe na ushawishi wa kutetea hoja zako watakutafuta for political reasons.
(3). Kupitia connection, Kama una ndugu yako mwenye nafasi kubwa ni rahisi kuchukuliwa, Ni mwendo wa vi-memo tu.
Note: Kama unataka kuwa TISS na hauna connection wala hutaki jihusisha na mambo ya siasa Basi njia ya kwanza ndio option iliyobaki, Jitahidi kufanya vitu ambavyo vita wa attract wao wakutafute njia rahisi ingia kwenye majeshi ya ulinzi na usalama iwe ni polisi,magereza, JWTZ n.k then fanya vitu extraordinary Huko usiwe mzembe fanya vitu vya kiintelijensia kweli onyesha kuwa una kitu extra basi unaweza chukuliwa.
Kama upo mtaani basi fanya vitu extraordinary jihusishe na mambo ya gunduzi, teknolojia, jifunze teknolojia mpya tafuta ujuzi wa kushawishi wakutafute kama kuwa expert wa computer mambo ya IT soma sana mambo ya networking etc alafu kuwa na project zako then zi launch kwa society wazione unaweza kuchukuliwa. Kwa nyongeza labda uwe mnaaa ukiona uhalifu,uuzaji wa madawa kama mirungi, bangi n.k Katoe taarifa polisi yaani uwe unachomea wananchi wenzako ila njia hii sio nzuri na salama do at your own risk.
N.B. Njia zote hizo hazina guarantee ya 100% so unaweza kuwa na sifa zote na ukakosa kazi kitengo na sio kitengo tu ata polisi yenyewe unaweza kosa.