Ajira za private sector zina mambo ya ajabu na visa

Ajira za private sector zina mambo ya ajabu na visa

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,473
Reaction score
4,007
Umewahi ajiriwa private sector halafu ukawa kiongozi kwenye idara flan, labda umeajiriwa na mzungu au mwafrika ambaye ni wa nje ya nchi? Kama bado pata story ukae ukijua na haya mara nyingi sana yapo private sector, maana serikalini ukimfitini mtu taratibu za kumuachisha kazi ni ngumu na sio rahisi kiivyo. Utasikia waajiriwa asilimia flan hivi ni washirikina sana na sio wakristo au washika dini haswa wana sababu zao ebu sikiliza hapa story.

Kwanza kwanini sisi wabongo tunapenda sana kuharibiana ili tuchukue nafasi za wengine ni tama au uchu, wengine hawana hata vigezo ila wanalazimisha tu, kwanza tuna tabia ya kuwa na tamaa, kazi aliyonayo mwenzio unaitamani iwe yakwako, je una uwezo, na kwanini usijibidiishe ili upate nafasi hiyo kwa bidii zako na elimu yako, badala yake unaanza kumpiga vita mwenye nafasi hiyo kwa kupeleka umbea kwa boss wake, nilimpenda boss wangu flan hivi kutoka Netherland, ukimletea umbea anamuita mhusika anakwambia useme ulichokuwa unakisema mbele yake jasho linakutoka, tuna wasilisha mengi ya uongo ili boss akuone wewe ni mzuri mwenzio hafai ukiona boss haelekei unaenda kwa Babu eti umtupie mikosi ili yeye achukiwe na boss wewe uonekane ni mzuri, hili limewakuta wengi na limewatesa wengi wasio na hatia.

Mara unaanza kusingiziwa na visa vinaanza. Wanao fanya hivyo watakaa nafasi hizo lakini hawawezi kukaa kwa muda mrefu lazima watatoka na watajuta kwann hawakubakia nafasi zao za chini au kwanini wasingeacha vijembe.

Nilete mfano hai, nimefanya kazi Kenya kwa miaka 4, ukiwa unatokea Namanga Arusha kwenda Kenya ukifika Narok pale kuna Project kama ngapi nimesimamia mimi mfano ujenzi wa Shule kwa jamii za kimasai na water projects nilipewa ofisi kwa kuaminiwa na wazungu, sikupendwa kabisa. Nilipewa administration ya chuo flan maarufu sitaki kulitaja watajua wengine na wakenya waliomo humu maswala ya chakula cha wanafunzi pale campus lazima budget ipitie kwangu ni idhinishe wakanunue vyakula na nina sign check za matumizi, huwezi amini nilipigwa vita sana, ilifikia hatua nikasema sasa narudi nyumbani nimefanya kazi kwa miaka kadhaa nilikuwa mjanja maana walinitafuta juu chini sikupatikana kabisa kuanzia sumu na mengie mnayoyajua. Na ilifikia hatua wakaniwekea mtego wa msichana ili nikamatwe ungoni nikakwema maana sikuwa interested.

Hapa nyumbani nimeshafanya kazi na NGO kama 3 hivi kubwa, ya pili nilifanya kazi ya Engeneering upande wa ICT nilifunga dish za C-Band kwa mawasiliano ya internet na VOI na ku design Network topology kwa ajili ya Korogwe, Bukoba, Shinyanga, Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar… kosa au sijui niseme bahati nililofanya ni pale nilipoomba nipewe kuwa Mkurugenzi wa Afrika mashariki kitengo flan hivi maana yake ningekuwa msimamizi wa miradi iliyopo Rwanda, Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya na Sudan majamaa yalivyosikia hivyo basi vita vikali sana vilianza, hata hivyo nikaambiwa nifanye kazi Dubai kwa ajili ya emergency niwe naangalia nchi za kiarabu na Africa vita vikaibuka tena ni vita kweli sio mchezo vita vikali kweli ile unayosikia mtu anaangukia bafuni au chooni yote yalitumwa, hata siku moja nilitaka kudondoka sokoni maana kizunguzungu cha ghafla na moyo kubanwa ghafla ahaha chezea waroho wa madaraka ww. Mi mkristo namwamini Mungu na sifikirii kuhangaika, niliamua kuachana na kazi zote nikakaa kwanza chini kupumzika nikawa na amani. Sasa niseme hivi mnaofikiria kuwatoa roho wenzenu kisa madaraka je mtaishi milele hapa duniani? Hili ni swali langu kwa wote watumishi wasio jibidiisha na kufikiria kuwafanyia wengine mabaya ili wao wanufaike. STORY HII ITAENDELEA MWEZI MAY 3, 2018. (samahani kwa usumbufu)
--------------------------------------------------------------

MUENDELEZO


Nauliza tena mnaotaka vyeo vya wengine huku mkiwa hata vyakwenu hamfanyi vizuri mkasifiwa kwa kazi nzuri mnataka nini, mnazitaka roho za wenzenu au kuwaharibia maisha kwa uchafu mnao watupia?

Umri wangu ni kati ya 36-41, Kati ya vituko nilivyo kutana navyo ni pamoja na kuwekewa unga usiojulikana ni wa nini unaoekana kwa mbali sana mpaka uwe makini na haujulikani ni wa nini unawekewa kwenye seat ya ofisini, kuwekewa sumu kwenye glasi ya maji nyeupe yani sumu ya maji ni nyeupe huwezi jua, chini ya meza wanamwaga unga flan hivi, naletewa breakfast yenye sumu kwenye omelet na chai…

Maisha ni kupambana si vinginevyo kila mtu ajitahidi apate ajira kwa boss wake kutokana na uwepo wa uwazi wa nafasi hiyo na sio kutafutana.

Nilijipanga sana, hata hivyo ni mtu ambaye huwa najiongeza sana naangalia upepo unapokwenda, niliona kazi ya Engeneering inazehesha haraka sana ni ngumu mno kila nikirudi jioni nachoka mno, sasa walivyoniletea matatizo, nikaamua kubadili fani nikaenda chuoni tena kusomea kitu tofauti namaanisha faculty nyingine ili nifanye kazi ambayo itanifaa tena ila sasa unatakiwa uwe vizuri kichwa kikubali maana kusoma kuna usumbufu wake. Nilipoweka profile yangu UN basi wakawa wana ni shortlist kwa ajili ya interview ila sasa sikufanikiwa kupata nafasi hiyo na sikuomba tena, huko kwenye iyo NGO nyingine sasa nimeacha kazi niko kwenye NGO nyingine ya 3, sasa basi nikagundua kuwa nimemzidi boss wangu elimu wafadhili ndio walinifanyia interview wakaniingiza hapo sasa boss naye akaanza kuhofia kuwa kuna uwezekano wa wafadhili kunipa ile nafasi yake, alihisi hivyo mara zote ila mimi wala siitamani, huyo boss wangu iyo kazi aliipata kwa ki memo kutoka kwa wanasiasa ndugu na marafiki zake, hakuwa na muda wa kujiendeleza alijisahau ila angejiendeleza ki elimu angeweza kuimudu, sasa watu kama sisi kuingia hapo ikawa kikwazo kweli kweli. Ila mi mjanja huwa najituma kweli si mchezo.

Niwaulize ma boss ambao hamtaki kujiendeleza ki elimu na mshahara mnao mzuri mnataka nini sasa mnatufanya sisi tunaotafuta kazi tuanze kuwaogopa kuwa hatuwezi kuajiriwa kisa elimu yangu ni zaidi yakwako na mnatunyima ajira kwa sababu hiyo si nyingine.

Bosi alinijengea hoja eti sifai na sifanyi kazi vizuri mkataba usitishwe, dah mfadhili akasema wanipe assignment au kazi ya kufanya nikishindwa basi mkataba usitishwe, sasa mzungu alivyokuwa mjanja kazi hiyo alimpa na boss wangu aifanye kimya kimya bila ya yeye kujua ila kwenye miradi tofauti inayofanana, ahah kilichotokea kazi hiyo ya vitendo niliifanya kwa ufanisi mkubwa zaidi ya boss wangu kwanza kazi iyo ilikuwa inahusu kuandika brief report ya kumshauri Rais wan chi na waziri husika kuonyesha impact yake na kuwashauri kwa ajili ya maamuzi, pili ilikuwa KUFANYA ANALYSIS YA POLICY (quantitative) Badae kwenda field kufanya Evaluation ili kuja na repoti na mapendekezo kwa hatua zaidi (tools na method niliyotumia ilikuwa ya hali ya juu sana) kama mnasikia mtu ni mshauri wa… huwa lazima ufanye kazi ambayo ukimshauri boss wako akifuata hatajutia maamuzi. Ahaha Boss wangu chali siku hiyo hiyo baada ya kuwasilisha ripoti mfadhili alimshusha cheo na kunipa baruwa nichukue nafasi ile. Sasa sikilizia mziki mama yangu kwanza niliomba off siku 4 ili nijipange vizuri kumbe nimejiloga siku ya kwanza kwa wanaofahamu pale arusha njiro kanisa la SDA kuna mitaro ya maji niliendesha gari karibia kufia kwenye mitaro ya maji nikiwa peke yangu ila Mwenyezi Mungu alikuwa na mimi, siku inayofuata nipo kitandani usiku alikuja mtu mrefu sana mweupeeee kama mzungu ananiambia nakuja kukuchukua tuondoke nikamuuliza kwenda wapi akasema nitajua badae ahaha sasa unataka kujua kilichoendelea baada ya hapo (sehem hii nitaizungumzia siku nyingine maana ni story nyingine)

Siku ya kuripoti niliandika baruwa kwa mzungu sihitaji tena kazi nitaishi bila kazi. STORY HII ITAENDELEA MWEZI APRIL 4, 2018. (samahani kwa usumbufu)
 
waTZ ni problem kwenye ajira binafsi ndio maana katika East Africa nchi ambayo ina waajiriwa wenfi kutoka mataifa mengine ni Tanzania. Wa TZ ni shida tunawaajiri hakuna jinsi lakini ni shida
 
Hayo uliyoyahadithia mbona hayako tu private sector? Hayo oia yako serikalini. Ushirikina haujalishi uko private sector au public sector. Sio hivyo tu, kutotakiana mema ni kila sehemu hata kanisani na misikitini yapo na nina ushahidi. Cha msingi chapa kazi na mtangulize Mungu kwa matendo sio maneno.
 
Ushirikina kila sehemu upo, hilo limewahi kunikumba huko Tunduma, kuna jamaa wawili hivi toka Songea nafikiri hata Malawi wamefika kisa tu kwanini jina langu linaongelewa sana. Nimshukuru Mungu nipo salama salimini na field ya ile kazi nimebadili.
Kiukweli kazi ya engineering inataka moyo, maana ikikukuta wewe ni mvivu utakaa kutembea kwa waganga mara kwa mara, ila huwa Mungu hamtupi mja wake tutapambana hivyo hivyo.

Poleni sana ndg yangu kwa yote yaliyokusibu ila mtegemee Mungu atakunusuru kwa kila baya, mimi walitembea Sumbawanga nzima then wakarudi wakakaa.
 
Hongera saana mkuu, unaonekana uko smart saana, hila ukicheza hao jamaa watakuuwa , mkuu umesomea wapi ?
 
Engineuring? Unaweza ukadhani unapigwa vita ila kumbe unajipiga vita mwenyewe.
 
Back
Top Bottom