Ajira za Polisi 2022/2023

Winga dalali

Senior Member
Jul 20, 2021
192
263
Msaada wana JF,

Kuna mdogo wangu,alituma maombi ya kazi polisi, kwa kutumia cheti cha kidato cha nne (IV) waliambiwa wapeleke kwa makamanda wao wa mikoa, tofauti na wale weneye elimu kuanzia certficate hadi degree walituma maombi kwa njia ya mtandao.

Leo tovuti ya jeshi la polisi imetoa orodha ya majina waliofuzu kwenda hatua ya usaili.

Naomba msaada kujua hawa waliotumia cheti cha kidato cha nne majina yao watajuaje kama wamefuzu kwenda usaili? Au jeshi la polisi hutumia njia gani,kuwaita kwenye usaili?

Naomba kuwasilisha! 🙏 kwa anayefahamu tafadhali.
 
Hayo majina ni kwa walioomba moja kwa moja kwa IGP,ni wale wenye Certificate,Diploma na Degree,wale wa Form 4 na 6 walioombea kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa majina yao yatatolewa hukohuko
Huko huko,kupitia njia gani?
 
waliotuma kwenye Email Makao Makuu,walioombea kwa Makamanda mikoani wameanza kutumiwa meseji kwenye simu zao kuitwa kwenye Usaili,kijana wangu ametumiwa,yeye aliombea kwa Kamanda wa Polisi Singida,anatakiwa tarehe 23 saa 2:00 asubuhi kwa Kamanda Singida
 
Asante, kwa ufafanuzi
 
Hizi ajira bado moyo wangu unasta. So mm ndio nakua polisi?
Kwanini,kaka moyo wako unasita? Umeomba? Kama moyo wako hauko na utayari,ni vyema kutokua kabisa,kama umeomba kwa namna au sababu zitokanazo na msukumo wa kimaisha.

KUNYWA MAJI MENGI,FUNGUA MOYO POTI
 
Back
Top Bottom