Ajira Utumishi - Recruitment portal

Ajira Utumishi - Recruitment portal

kuku wa kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2012
Posts
494
Reaction score
151
Kwanza napendeza kuipa hongera kwenda ajira.go.tz kwa jitihada utumishi wanazozifanya katika kusogeza huduma karibu kwa wateja. Je wewe ni mmoja kati ya watu ambao wameshawahi kufanya maombi ya kazi online kwa kutumia Recruitment portal ?Bila shaka jibu lako ni ndio.

Nataka nikufundishe kidogo utawezaje kujua kama utaitwa kwenye inteview kabla hata majina hayajatoka. Je una kiu hiyo ya kutaka kujua ?Ingia kwenye akaunti yako, click My applications.Zitakuja positions ambazo umesha-apply tayari.Angalia kuna mahala pameandikwa Application Status -Kama umebahatika, utakutana na neno First Interview

HONGERA SANA:

Nyongeza plus~updated 08 May 2015. Napenda kushare na nyie kitu kidogo ambacho kitasave pesa zetu kuhusiana na barua za maombi za kuattach kwenye job application.Je unapoteza pesa nyingi kwenye ku-scan ?Usiende kuscan barua yako hakuna hiyo haja. Type vizuri barua yako ya kazi kwenye Microsoft word then isave.

smallpdf.com/word-to-pdf ina uwezo wa kubadilisha document yako iliyo kwenye word to pdf.

Huna haja ya kuscan barua zako za kazi.

Utumishi wametoa mwongozo kwa watu wanaoomba kazi mtandaoni, pakua faili la PDF hapa: View attachment 277759

Hivi kumbe pakiandikwa hivyo maana'ake utaitwa kwenye interview?
 
Msaada plzz mbona kipengele cha training na work experience najaza zote nikitaka kusave haijisave nifanyeje? Ama nakosea nini? Maana mpka sasa nina 49% tu sijui hizo sabini naFikisha je?
 
Hata me inanzngua, ndio kwanza iko 44%,alafu kitu kingine wakati naandika e-mail yangu kujiregister ikatokea pale yenyewe,asa najiuliza imekuaje inanifahamu?
 
Msaada plzz mbona kipengele cha training na work experience najaza zote nikitaka kusave haijisave nifanyeje? Ama nakosea nini? Maana mpka sasa nina 49% tu sijui hizo sabini naFikisha je?

Hakikisha vibox venye * nyekundu vijazwe. Those are compulsory

Then jaribu tena
 
Tofauti kati ya academic qualifications na professional qualification.
Na kwenye academic qualifications najaza general kwamba mf bachelor tu au naweka detail moko moko kuanzia cheti cha o-level?
 
Tofauti kati ya academic qualifications na professional qualification.
Na kwenye academic qualifications najaza general kwamba mf bachelor tu au naweka detail moko moko kuanzia cheti cha o-level?

Academic qualifications ni hizo bachelor , master, o level Etc

Professional ni CPA(Hii ndo inaehishimika sana duniani), CPB, ACCA, CIA, CIMA, CISA, kuku wa kienyeji, etc

Back to your qn, Onyesha kila kitu, SEPARATELY. Ikiwezekana anzia la saba, o level, A level, degree, master, phd, professor, kuku wa kienyeji etc

Naombeni mnishawishi kugombea,
Wenu Kiongozi,
Kuku wa kienyeji
 
oya mwana mbona mie nimetuma ikanandikia upande wa application status-neno reseived?
 
Mi mbona nikiview my application imeandikwa Application status received ilo neno First Intervie mbona silioni?

Kaka sasa ndo umetoka kutuma. Subiri mpaka ukaguliwe kama uko qualified, ndo utaandikiwa first interview.

Processing bado zinafanywa na watu si computer braza. Huwezi kutuma hapo hapo na kuambiwa tayari for interview
 
oya mwana mbona mie nimetuma ikanandikia upande wa application status-neno reseived?

Mkuu, hilo neno sijalielewa "reseived "

Kama una-maanisha Received -ndo inaonyesha imepokelewa.

Kama una maanisha Reserved - najua unafahamu maana ya reserved nini
 
Received maana yake imefika, kama wataamua kukuita ndipo status itabadilika kuwa interview
 
Kwahyo wote wanaoandikiwa 1st interview wataitwa? Mmh me mbna zote nlizoapply nmeandikiwa 1st interview na nyngne nliapply kujaribu tuu sina hata qualifications ila meandikiwa 1st interview...Is it kweli hilo neno linarefer kuitwa kwa interview?
 
Kaka sasa ndo umetoka kutuma. Subiri mpaka ukaguliwe kama uko qualified, ndo utaandikiwa first interview.

Processing bado zinafanywa na watu si computer braza. Huwezi kutuma hapo hapo na kuambiwa tayari for interview
Nimetuma tangu tarehe 11/04/2015 Kuku wa kienyeji
 
Back
Top Bottom