Bwamdogo anafikiria akipata kazi ndo dharau zitaisha! Dogo wenzio tumemaliza 2012 tukasota wee, tukajiongeza na mtaa, niliamua kuendeleza kipaji changu cha utoto cha ufundi, nikaingia gereji leo mi ni fundi wa umeme wa magari. Yan fresh tuu hakuna mtu anajua nina degree na nimesogea sehemu flani kimaisha. Weka degree pembeni afu tumia ulichonacho "kusavaivu" bwa mdogo. Nilikaa gereji mwaka tuu nikawa nimejifunza kazi kibishi sana, uzuri wa gereji hatubaniani kufundishana kazi madam uwe mtii, kujituma na kuheshimu watu wanaokufundisha. Alhamdulilah degree yao nishaisahau kabatini huko.