Ajira kwa wageni iangaliwe upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira kwa wageni iangaliwe upya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Jun 21, 2011.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kasumba ya kuajiri wageni hasa kutoka kenya naomba iangaliwe kwa makini,
  tukumbuke tuna wasomi wanagraduate kila mwaka,kama muungano wa africa mashariki unakuja na hasara
  kwa watanzania kiasi hiki basi tumekwisha,
  ukitembelea makampuni makubwa hasa ya kutoka nje na mengine ya ndugu zetu watanzania
  wanapendelea kuajiri wakenya eti kwa sababu wanajua kiingereza
  nina imani kila mahali kuna mkuu wa wilaya na watendaji wao lakini wanapuuza hili jambo,
  kama watanzania hatuna ujuzi tuna haki ya kufunzwa ili tupate ujuzi unaotakiwa,
  kwa watanzania wenzetu wanaofanya hivyo naomba waache hiyo kasumba kwani sio uzalendo,
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ofisi jirani kuna kampuni ya ujenzi wote wachina wameomba working permitt as Civil engeener ila cha kushangaza ni wapishi, cleaners and office attendants wanazunguka huku na kule kununua chapati za wafanyakazi tena wabongo walioko ndani
   
 3. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kuwa na Agenda nyingi sana zitatushinda kuziaccomplish.
  tufocus kwenye Agenda ya kuwaondoa CCM madarakani sababu
  ndio chanzo cha matatizo yote haya.

  Hizi kero zote zinazotusononesha wameshindwa kuzitatua
  na sasa ndio tunazidi kuwafahamu zaidi kwamba wamekwisha poteza
  dhamira ya kuziondoa.

  tuzitumie sababu hizi kuwaondoa marakani hata sasa.
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  nashangazwa sana na wakenya kuwazidi kete watanzania
  mbona mna university nyingi sana hapo?ina maana wote mnaomaliza mnapata kazi?
  inakuwaje wageni wapewe kazi ndani ya nchi yenu na nyie hamna kazi?
  kama vipi fanyeni kama south africa kuwakimbiza wageni,
  nafikiri hiyo itakuwa ujumbe tosha kwa serikali yenu
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,285
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  hiki ndicho kilico baki, nchi za ulaya wanaua wageni
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama tunategemea baada ya miaka mitano watakuwa wameisha komaa. Ukiwagusa kuwaondoa watakuwa wameweka mizizi. Agenda hii ni muhimu kwa sasa ili kuwazuia wasiingie na kuota mizizi isije ikawa ngumu kuwang'oa.
   
 7. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Siyo hiyo tuu! Wakenya baada ya uhuru waliendeleza ubepari wa kizungu uliokuwepo. Kwa hilo tu wakawa kipenzi chao! Hivyo usishangae hao wageni kutoka Ulaya kuwapendelea Wakenya. Hao kwao ndiyo Yes Sir wao. Sisi tukiulizwa swali tunajibu kwa kuwauliza swali! Hapo ndiyo mzungu nguvu zinamwisha kabisa! Kwake bora mkenya anatii kwanza. Potelea hata kama hana taaluma nzuri bora awe msikivu na mzungumzaji wa kiingereza basi!
   
 8. v

  vivimama Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si hao tuu, migodini huku kuna makaburu kibao wanajiita ma-expat wakati hawajui lolote wanakuja kulala na kupewa mishahara mikubwa wakati kazi zote wanapiga wabongo.
  mapenzi yangu
   
 9. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kuna kitu iitwayo professionalism, and thats what most employers look for. Watanzania wengi wame qualify kwenye nyanja tofauti, kijana ana ka degree kake kutoka UDSM, lakini pale unapomwita kwenye interview aketi chini na panell ianze kumuuliza maswali, una realise ya kuwa hana chochote anachojua na confidence yake si kitu cha kutamanisha. on the other hand, Wakenya waliopo huku wako kikazi zaidi, wanajua wanachotaka na wanafanya bidii kukipata, tusiwe tu watu wakuongea bila ya kuchunguza zaidi ili kuelewa kwa nini makampuni fulani yanaandika wakenya.

  Kucomplain hapa kwenye Blogs haitasaidia, ndugu yangu Thabo Mbeki hapo juu anasema waTz wafukuze foreigners kama vile ammbavyo wale illiterate goons walivyofanya kule SA, he tends to forget that he lives and works in SA. Vijana wa Kibongo wanafaa kusoma sana, dunia ya saa hii sikama ile ya zamani, this is a global village na hizi borders hazimsaidii yeyote, zina ongeza uvivu na uswahili kwa kuwa hakuna competition na kila mtu yuko comfortable.

  Kenyans are not the problem, the uneducated Tanzanian youth is.
   
 10. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jamani siku hizi hata walimu wa day-care wanatoka Kenya.............
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu nimekuelewa vizuri sana
  kumbe nyie watanzania mnasoma theory?kumbe mnakaa darasani na kukariri peke yake?
  ndio maana ridwan kikwete alisema anaishi kimjinimjini wakati ana degree ya law?
  ndugu zangu kwa south africa mwenye degree kama ya ridwan ni mtu anaheshimika sana,
  kama ndio tabia yenu ya uvivu na maneno mengi mitaani,
  sidhani kama mtaweza kukimbizana na wakenya,na kwa bahati mbaya mna chuki binafsi za kidini ambazo zinawapotezea muda mwingi.
  sidhani kama skill ni jambo la muhimi sana hapo tanzania,
  hapa kila siku mtu anawaza jinsi ya kuendeleza skill aliyo nayo,nafikiri kwa hilo mtaona rangi zote!
   
Loading...