Ajira hizi ni kufunga ndoa na ufukara!

Kuna haja ya kuweka msisitizo na umuhimu mkubwa mno kwenye masomo ya ubunifu "creativity" na teknolojia, hivi ndio vina run dunia leo, sasa elimu yetu bado inaakisi miaka ya 60's kipindi tunaandaa wafanyakazi, sio watengeneza kazi.
Infact tangu nimemaliza primary late 90's, sijaona mabadiliko makubwa na muhimu kwenye elimu ya msingi, haswa kwenye upande wa ubunifu na self confidence, what are we expecting then??

Sishangai kuona graduate hapa tz,kwa elimu alionayo anakosa self confidence, hana mawazo mbadala, zaid ya nadharia kibaao alizokariri anzia chekechea hadi umri huu,mbaya zaidi utamaduni wa kusoma vitabu na majarida muhimu yanayoweza kutanua ubongo na uelewa, wengi wao hawana, iko shida, tumeandaliwaje? nothing happens accidentally!
Serikali iangalie na kulipa uzito mkubwa sana suala la elimu na ubora wake, ndio muharubaini wa kwanza kwa tatizo la ajira nchini, otherwise tatizo halitapungua kwa namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni pale graduates wengi wanafunzwa vibaya,kufikiri kipato lazima kitokane na kazi za ofisini,kuniga tai.

Nawashangaa vijana fulani eti wamemaliza chuo kabisa wanalipwa laki tatu. Sasa kuna mwenzao hakufika form four ana toroli lake la matunda. Haki ya Mungu huyu muuza matunda anaweza kuwalisha hao wa chuoni

Kijana wa chuo humwambii achome mahindi, humwambii achome chapati ,kha!

Tungebadilika hapo,huko tunakonyonywa tungepungua.
 
Pamoja na degree yangu ya std 7 ila huwa najiona mfalme mbele ya waajiriwa! Ajira ni upumbavu tu!
 
Pamoja na degree yangu ya std 7 ila huwa najiona mfalme mbele ya waajiriwa! Ajira ni upumbavu tu!

Hahah! Hapa umejumuisha mno.Bado hatuwezi sema ni upumbavu lakini kile kitendo cha kuona kuajiriwa ndiyo kila kitu au hakuna maisha nje ya ajira tunakosea sana.
 
By my side!! Ajira ni utumwa tu,,whether smart or not!

Kwakuwa ni mtazamo wako basi ni sawa. Ila ikumbukwe tu hapa,hatuwezi kuepuka ajira. Lazima kuna kundi litaajiriwa na kundi litaajiri.Maana hata yule asiyetaka kuajiriwa, kuna siku atahitaji kuajiri.
 
Kwaiyo nini ushauri kwa walioko vyuoni wakisomea hizo fani alizozitaja Mkuu?

Wa change mindset. Ajira hazina tija. Wakishamaliza masomo yao wajikite kwenye kilimo au biashara. Watatoka.
 
unasoma ili uajiriwe. elimu ni pesa huwez tumia gharama kwenda shule halafu uje kufanya biashara huo ni ujinga si bora ungeishia la saba tu? bora ufanyekaz
 
Back
Top Bottom