Ajira hizi ni kufunga ndoa na ufukara!

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,084
2,000
Jamii sasa imebadilika sana na milango ya ajira imepanuliwa kiasi cha kutosha. Hivi sasa ajira nyingi zilizoitwa uhuni miaka ya nyuma ndizo zinazolipa. Sana.

Ajira rasmi za Serikali heshima yake inazidi kushuka kwani malipo yake ni kiduchu sana. Hatujafikia hatua ya ku legalise ukahaba, lakini kama ungeruhusiwa, nafikiri makahaba wangekuwa na mapato makubwa zaidi kuliko wafanyazi wengi wa umma.

Pamoja na kwamba baadhi wametumia miaka mingi kusoma wafanyazi hasa wa umma hawapati mishahara ya kutosha na hivyo kusoma kwao kuonekana hakuna maana. Badala ya kuboresha maslahi ya wafanyazi, Serikali imekuwa nikipiga blabla kila siku kila mwaka.

Hivi sasa watu waliokuwa wakishika mkia darasani wanapata kipato mara dufu ya wale waliokuwa wakipata A nk.... Ukweli ni kwamba hadhi ya wafanyazi kama walimu, manesi, polisi, mgambo, makarani nk inazidi kushuka? Why? Kipato chao duni. Ndio maana baadhi ya watu wanaojiita kwenye siasa. Si ndiko Serikali imewekeza zaidi!!! ___ Kumbuka the lousy chaguzi za marudio zilivyotumbua mabilioni.

Hii inawavunja sana moyo na ndio maana baadhi wanajiingiza kwenye ubadhilifu. Bila kumpenda mara nyingi!

Kwa kweli siku hizi kukubali kuajiriwa kama polisi, mwalimu, nesi, mwanahabari, mwanajeshi ay karani ni kukubali kufunga pingu za maisha na umaskini. Huwezi kuukwepa umasikini katika nyanja hizi.

Kwa kuwa lazima watu kama walimu na polisi lazima wawepo katika mfumo wa jamii, basi either Serikali iwekeze kwenye maslahi yao seriously au watumishi hawa wachukue 'nadhiri' ya ufukara....!!
 

John_Bravo

Senior Member
Jul 20, 2018
164
500
ila ni kweli kuna jamaaa yangu ana diproma ya Information technolog analipwa laki tano na sitini na tano basic yaan dah

Sent using Jamii Forums mobile app
Broh mbona huo mpunga wakutosha..Watu tunaoenda kazini/poster kila siku kiwango Cha mshahara ni laki tatu tena hiyo ni private sector..Amini mkuu..Wahindi wanautumia sana..Na wafanyakazi wengi ni University graduates..


#Muungwana_John
 

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
568
1,000
Kwaiyo nini ushauri kwa walioko vyuoni wakisomea hizo fani alizozitaja Mkuu?
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,713
2,000
........................Mwenye kusikia na asikie!

Wengi wanajisahau sana wakiwa mavyuoni utakuta huku wanakula pindi huku kichwani zinakatiza ndoto yupo office fulani city center full kiyoyozi juu ghorofa ya saba chini kapaki Klugar au Harrier New Model huku demu wake akimsubiri kwenye ka-restaurant fulani waondoke wote sasa wakija mtaani wakikutana na show la kibabe kazi hakuna pesa hakuna hata kibarua hakuna wanchizika.

Kwa tulipofikia elimu bongo ni kwa ajili ya kukutoa tongotongo tu kwamba 1+1=2 pamoja na kukupa uwezo wa kuwasiliana na watu wa mataifa mengine siyo tofauti na hivyo usitegemee ipo siku ajira yako serikalini itakutoa labda ujitoe muhanga uangalie huku na huku kama hakuna anaekuona upige ndefu ila kama siyo hivyo basi sahau.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 

gunz

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
308
500
Sehemu kubwa japo si zote ktk maisha Unachosoma shuleni au chuo sio kwamba utakuja ku apply katika kazi.ndo maana watu wengi wanafeli wakifika mtaani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom