Kwa kweli amenisikitisha sana, ila bado sijatambua nguvu ya namba 3 na maisha ya mwanadamu.
Kila kitu kinakwenda mara tatu. Tukianza na Utatu Mtakatifu, Alianguka Mara Tatu, Walisulubiwa watu watatu, Akafufuka siku ya tatu, Tuna Mafiga Matatu, Dakika Tatu, Kutwa Mara Tatu, ghrrr! Tatu Jamani Tatu, nini maana yako.
Laiti angelipata mtu mzoefu wa kumshauri kuwa kufeli mtihani sio kufeli maisha. Kuna watu wengi waliofeli mtihani / hawakusoma lakini wana maisha mazuri kuliko hao waliosoma.