SaidAlly
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 2,386
- 2,339
Kila siku tunasikia taarifa za ajali zinazopoteza maisha na kuacha familia zikiwa na majonzi. 😔 Hamna mtanzania ambaye yupo salama ambaye anatoka asubuhi kwenda kutafuta. Polis wa usalama barabarani fanyeni kazi kwa weledi ajali zinaepukika.
Tuwe makini barabarani:
🚗 Epuka mwendo kasi.
📵 Usitumie simu ukiendesha.
🍺 Usiongoze gari ukiwa umelewa.
🚦 Heshimu alama na sheria za barabarani.
🛵 Wapanda pikipiki na abiria watumie helmeti.
🚌 Madereva wapumzike wanapochoka.
Dakika chache za uzembe zinaweza kubadilisha maisha ya familia nzima. Kuna watoto wanateseka siku ya leo kwa kuondokewa na wazazi/mzazi sababu ya ajali.
🙏 Tanzania salama inaanza na mimi na wewe. Tuendeshe kwa tahadhari, tuokoe maisha.
Unajitahidi kufanya yote hayo, safari ndefu toka mwanza kuja dar, unafika mlandizi anakuja traffic anakulazimishia kosa ili utoe chochote na ukiwa umeanza kuchoka unafanyaje hapo? Kosa eti ume overtake lori wakati lilikua limesimama na mbele kulikua clear......??!!