Ajali za kibaologia,nani husababisha?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Unakuta mtu anazaliwa akiwa na ulemavu wa viungo,ama hana kiungo kimojawapo,ama mtu ana jinsia mbili nk.Je nani anahusika na jambo hili?Kama binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu,je ni sehemu gani anayofanana Mungu?Hata mapungufu,yana maana kuwa shetani ana uwezo wa kuingilia uumbaji wa Mungu kama mawimbi ya redio yanavyoweza kuingiliwa?Watu wa dini wanaofunuliwa siri na Mungu,je mmewahi kufunuliwa kuhusu hili?
 
Huenda wao ndio wamekamilika ila sisi tunaojiona wazima ndio walemavu,
So hunda Mungu anatembea kwa mguu mmoja, au labda hana macho,
au labda ni bubu haongei,
Bakiza akiba ya maneno mkuu
Umefika mbali sana
 
Binadamu wote hatufanani, so hakuna mwenye uhakika wa jinsi Mungu alivyo according to his statement tuliumbwa kwa mfano wake
Ni kweli. Lkn vingine ni kumuachia mwenyewe waweza kukufuru bure
 
Ni kweli. Lkn vingine ni kumuachia mwenyewe waweza kukufuru bure
Mkuu acha watu wawe na uhuru wa kujadili mambo kwa mapana bila kuweka mipaka, mambo ya kukufuru ni hadithi zisizo na mashiko kwa ulimwengu wa sasa
 
Unakuta mtu anazaliwa akiwa na ulemavu wa viungo,ama hana kiungo kimojawapo,ama mtu ana jinsia mbili nk.Je nani anahusika na jambo hili?Kama binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu,je ni sehemu gani anayofanana Mungu?Hata mapungufu,yana maana kuwa shetani ana uwezo wa kuingilia uumbaji wa Mungu kama mawimbi ya redio yanavyoweza kuingiliwa?Watu wa dini wanaofunuliwa siri na Mungu,je mmewahi kufunuliwa kuhusu hili?
Ulimwengu ulifanyika kwa Nguvu na Sheria, na kwazo Ulimwengu unaishi na kila kilichomo. Uovu na Ubaya ni Matokeo ya kutotii Sheria, wakati Upendo ni matokeo ya Kutii Sheria. Ulimwengu unaishi kwa Sheria.

Je, ni kiungo kipi utakapokikosa utakuwa umepoteza sifa ya kuwa binadamu? Je, ni miguu? mikono ama macho? Mwili ni sehemu ndogo tu ya Ubinadamu wake mtu. Mwili wako hautoshi kukusemea wewe.

Anaita sasa.
 
Huenda wao ndio wamekamilika ila sisi tunaojiona wazima ndio walemavu,
So hunda Mungu anatembea kwa mguu mmoja, au labda hana macho,
au labda ni bubu haongei,
If God exist, then he is not a physical being...
 
Ni kweli. Lkn vingine ni kumuachia mwenyewe waweza kukufuru bure
Hilo neno kukufuru ni uchochezi... bila shaka watu wote wangelikuwa na mtazamo huo... basi hata hii post yako isingewezekana.
 
Ndio ukweli wenyewe... tunalalamika waafrica nani katuroga lakini aliyeturoga ni huyu aliyetuletea hii ideology. Kwamba nikihoji masuala ya Kimungu basi nakufuru and hence utachomwa na moto wa milele... , je ulikuwa wapi kabla ya mimba???
 
Binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu ni ujinga ambayo wakristo wameutengeneza lakini sio kweli kabisa Mungu hafanani kabisa na alivyoviumba
 
Back
Top Bottom