Ajali yaua watatu Bunju B, Dar

kwanini uwezi kumsaidia?

Kuna siku jamaa alishuhudia mwendesha boda boda anagongwa na gari ya mbele yake. Ile gari ikakimbia, yeye akasimama kumsaidia, alichokipata Mungu mwenyewe anajua. Waendesha bodaboda wenzake na aliyegongwa walivyofika hawakuuliza kama yeye ndiye kagonga au ni mtoa msaada walianza kutoa kipondo kwa msamaria mwema na gari lake likavunjwa vunjwa vioo..

Twende mbele turudi nyuma, serikali inalichekea hili tatizo la wahuni wanaoendesha boda boda na wasipokuwa makini hii nchi itajenga genge la wahalifu ambao watakuwa wanaendesha nchi kuliko jeshi la polisi huku wakishambulia wananchi bila ya kusemeshwa na mtu. Nimerudia tena hapo juu, mnapoona hawa waendesha boda boda wanafikia kuvamia vituo vya polisi na kumtoa mwenzao na wakaendelea kupeta mitaani, huku ni kuwadekeza na matokeo yake sitaki kuyafikiria.

Kama kuna viongozi humu jamvini hebu lifanyieni kazi hili swala, msisubirie mpaka kiongozi mmoja wa serikali avamiwe au hali iwe mbaya zaidi ndio mu-act.
 

Nina uhakika hakuna ndugu, rafiki au mtu unayemfahamu aliyekutana na hili genge la bodaboda. Nakubaliana na wewe kuwa kuna madereva wazembe ila wanachokifanya kuwapiga madereva, kuharibu magari na kuiba mali sio sahihi hata kidogo. Kuna siku boda boda iliparamia gari la mtu and wakakusanyana kama boda boda sabini hivi walimvamia yule babu wa watu wakati hana makosa na kuvunja gari lake na kumuibia kila kitu wakati kosa ni la mwendesha boda boda. Mzee yule nina uhakika alipata kilema cha kudumu.

Hili ndilo unalotaka tulitetee humu ndani? Hakuna asiyesikitika kwa watu kupoteza maisha na inawezekana kabisa waliokufa sio kati ya wale wahuni ndani ya kikundi cha waendesha boda boda but kitendo cha kuvamia na kutaka kumdhuru na probably kumuua mtu sio sahihi hata kidogo as huyo dereva sidhani kama aliua kwa kukusudia hata kama alikuwa mzembe.. Angekamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola na si vinginevyo..
 

Kwa unavyowafahamu waendesha boda boda, hebu tujibu kiufasaha kabisa, uko pale ubungo au kimara kwa bahati mbaya ukagongana na boda boda (kama ni dereva mzoefu haya mambo yanawezekana kabisa kutokea hasa kwa kuzingatia uendeshwaji wa bodaboda), utasimama na kuanza kuangalia aliyevunjika mkono au aliyekufa..? Ukijibu hili swali kwa uaminifu kabisa ndio uanze kujadili...

Na kama unafahamu kanuni, mtu akishakufa humbebi tu kama inavyokuwa kwa mtu aliyejeruhiwa tu, kuna kanuni zake za kisheria la sivyo kesi inakuwa ngumu zaidi. So, itakulazimu umalize hizo taratibu huku waendesha bodaboda wakiwa wamekuzunguka wakikuimbia nyimbo za krismasi na mwaka mpya....in your dreams..!!
 

Unakurupuka fikiri kwanza! Ni jeshi tarajiwa la uasi kama hawatakuwa controlled. Wanavuta bangi, wanakunywa viroba, hawajui sheria za barabarani, wanaendesha ovyo na mmoja wao akigongwa hata kama ndiye mwenye kosa wenzake watakusanyika na kufanya uharibifu. Wewe cku ukiwa na gari ukamgonga bodaboda ndo utanielewa. Binafsi sijapinga aina hiyo ya ajira but nataka mabadiriko. Serikali iangalie namna ya kuwa-handle. Pili serikali iweke idadi ya bodaboda zinazopaswa kuwa barabarani badala ya kuacha kila mtu ajinunulie bodaboda na kuiingiza barabarani.
Halafu bodaboda sio ajira pekee kwa vijana. Think big!!!
 
GAUTAMA usirukie hoja usizozifahamu. Soma comments za watu. Mwenzako kawa tagged ili ajibu na bado yupo kimya, wewe wakurupuka tu.

Hizo Assumptions ulizokua unazitaka kwa kuniquote mimi ulimaanisha nini? watu wengine bwana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…