Ajali ya Precision Air Bukoba: Yawezekana IAMSAR Serikalini haipo au hawaitumii?

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Wana JF

Awali ya yote napenda kuwapa pole wafiwa na majeruhi wa ajali ya ndege Bukoba ya 06/11/2022.
Mengi yamesemwa kuhusu mazingira ya tukio la ajali kabla na baada ya tukio, hasa kuhusu operations za uokoaji na utendaji mbovu wa vyombo husika Serikalini. Na kwa taarifa yenu vyombo husika ni vingi, baadhi yake ni Bukoba Airport yenyewe, Polisi, Zimamoto, National Air Control department, Marine corps, Port Management Bukoba, Wizara husika za Serikali na bila kusahau vyombo vya habari na mawasiliano, na vyombo vya ulinzi na usalama vingine vyote ambavyo sijavitaja hapa.

Na hapa namaanisha katika level ya kitaifa na kimataifa. Hii ni kutokana na kwamba ajali ya ndege ni tukio linalotangazwa ulimwengu mzima.

Na kwakuwa usafiri wa ndege ni nyenzo muhimu ya shughuli na biashara za utalii Tanzania na kimataifa, ajali hii inafuatiliwa kwa karibu na baadhi ya washirika na wadau wetu na hata wengine labda washindani wetu tusiowajua, walio ndani na nje ya nchi.

Maana ya hayo yote hapo juu ni kwamba ni muhimu sana tufanye sasa kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba tunaweka mambo sawa kurudisha hali ya usalama katika masuala yote kuhusu usafiri wa ndege nchini pamoja na kuboresha utendaji, na uendeshaji katika vyombo vya usafiri, pamoja na vya ulinzi na uokoaji kama nilivyainisha hapo juu.

Kama nakumbuka na kumwelewa vizuri Msemaji wa Serikali, Mh. G. Msigwa, alinukuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari kwmfn 'Twitter' akisema kwamba ile ndege 'chopper' (Airbus H255 Super Couger) aliyosafiria PM Mh. M. K. Majaliwa kwenda kwenye ajali ya Bukoba, ilikuwa ya abiria na mzigo tu!

Kama model au jina la ndege hiyo ni: Airbus H255...; Kwa utafitini wangu mdogo ndege hiyo inawezekana kutumika katika masuala ya uokoaji, search and rescue (SAR).

Lakini wakati huo Mh. G. Msigwa aliposema ndege hiyo sio ya uokoaji, hakusema Serikali ina aina gani ya SAR operations aircraft kwa maana ya kwenye vyombo husika vya uokoaji ie. Polisi, zimamoto, nk.!

Nadhani hapo ndipo maswali mengi yanajitokeza! Kwamba hizi chopper nyingi tunazoziona zikiruka za polisi labda na za jeshi kumbe sio SAR vehicles. Na majibu hayo ya Mh. G. Msigwa katika Twitter, 'chombo cha habari' cha kimataifa; kuna faida au madhara gani kwa sifa yetu katika masuala ya usafiri wa anga na biashara za utalii nk?

Kwakuwa lengo kuu la mada yangu siyo kumkosoa mtu au Serikali sasa najielekeza kwenye mambo muhimu ya Sera au miongozo ya kimataifa ya. vyombo vya uokoaji:

International Aeronautical and Marine Search and Rescue (IAMSAR) Operation Manual, ni chapisho au kitabu cha mwongozo kuhusu vyombo, vifaa na shughuli za uokoaji duniani. Kimetungwa na taasisi za UN na IATA.

Kitabu hiki (kinapatikana kupitia Google) kinaelekeza namna ya kuendesha shughuli za uokoaji na jinsi ya kuratibu majukumu ya vyombo husika (kama nilivyoainisha hapo juu) katika matukio ya ajali. Lengo likiwa ni kuwahisha huduma muhimu na fanisi za uokoaji ajalini ili kunusuru maisha ya binadamu.

Vilevile IAMSAR ina miongozo wa aina ya vyombo na vifaa vya uokoaji. Labda ndiyo maana Mh G. Msigwa alisema ndege ya PM ile chopper haikuwa ya uokoaji kwakuwa labda haina vifaa vya uokoaji! Swali ni Je, inahitaji vifaa gani ili ikidhi vigezo vya uokoaji? Naamini hilo ndiyo lingekuwa lengo la kununua chopper ya aina hii.

Ukiona taasisi au watu wanababaisha mambo wakati au baada ajali ujue hawajasoma au hawana mwongozo wa IAMSAR labda na Sheria za uokoaji nchini, kama zipo. Na pengine hawana kabisa vifaa rasmi vya SAR operations. Vinginevyo ungesikia maelezo kwamba: Jamani eh! Sisi tumechukua hatua hii na ile kwa mujibu wa IAMSAR operations manual au/na Sheria namba kadha ya nchi na kufanya tulichotakiwa kufanya. Watu wangeelewa.

Kwahiyo hata pale Rais au PM anapoagiza uchunguzi ufanyike baada matukio mbali mbali ya ajali, (kama moto, meli kuzama, matetemeko nk) kama office yake haina miongozo rasmi kama huu wa IAMSAR ni vigumu kujua terms of reference za uchunguzi, nani achunguze, nani achunguzwe na maeneo gani, scope ya process nzima.

Nimalizie kwa kusema kwamba watu wanalalamikia "utendaji mbovu" wa vyombo husika kwasababu roho na mali za wapendwa wetu kama taifa zimeangamia na wengine ni majeruhi!

Jeshi letu la polisi, na zimamoto inawezekana wanahitaji choppers mpya za uokoaji au kuweka vifaa vya uokoaji kwenye magari na chopper zao ili zikidhi vigezo vya kimataifa vya SAR operation vehicles. Kwanini mlima Kilimanjaro uwake moto kwa siku kadhaa halafu muda huo huo ajali ya ndege inatokea na kutupa simanzi kiasi hiki mbele ya ulimwengu?

NAWASILISHA!
 
Sijaelewa hao wataalam waliokuja kufanya uchunguzi wa kuanguka kwa ndege wakati mawasiliano ya Rubani na Tower ni kwamba kulikuwa na hali ya hewa mbaya/mvua hivyo ikamladhimu akipeleke chombo majini ,sasa hao wataalam wanakuja kufanya nini? au kuja kung'oa blackbox waweze kuretrieve mazungumzo? kwanini tower hawakeep records ya mazungumzo?
 
Wakati umefika wa Tanzania kama nchi na sehemu ya jamii ya dunia ya sasa tujiulize: Je, hizi kamati za ulinzi na usalama kuanzia wilaya, mkoa hadi taifa zinazoongozwa na wanasiasa zina kiwango gani cha ueledi na ufanisi katika masuala ya search and rescue, SAR operations?

Uzoefu unaonyesha wazi kwamba kimuundo na kiutekelezaji ni sawa kusema hivi ni vyombo vya CCM, kwa maana watendaji husika wa Serikali katika masuala ya search and rescue kama RPC, RSO, RAS, RMO na wengine wote wakiwa wataalamu kwenye fani zao, lakini wanaongozwa na wanawajibika kwa wanasiasa! Watu ambao kiuhalisia hawana background knowledge yoyote kuhusu SAR operations au miongozo ya IAMSAR!

Ajali kama ya juzi Bukoba inapotokea, Msemaji Mkuu anakuwa Mkuu wa Mkoa badala ya RPC au mjumbe wa kamati ambaye ni mtaalam katika tukio husika.

Hiki ni chanzo cha madhaifu ya kamati hizi, unaojitokeza wakati wa kufanya maamuzi muhimu na ya haraka ili kufanikisha zoezi la uokoaji, SAR. Yaliyojitokeza katika ajali ya ndege Bukoba ya wavuvi kuwa watu wa kwanza kufika kwenye tukio na kutumia kamba zao kuvuta ndege ni ushahidi kwamba hakukuwa na mrejesho wa haraka (emergency response) kutoka kamati ya ulinzi na usalama kiwilaya, kimkoa na kitaifa!

Picha za ajali mitandaoni zilionyesha dunia jinsi wananchi, hasa wavuvi wakijitolea kutoa msaada wakati baadhi ya watazamaji wakiwa katika uniform za vyombo vya ulinzi! Inabidi tujiulize kama watu hao walikuwa polisi au jwtz walitumwa au walikuja wenyewe hapo kufanya nini?

Kwa upande wa vyombo vya uokoaji kama rescue boats, SAR aircrafts na vifaa vyake kuna wasiwasi kwamba Serikali haina chochote! Na kama wanavyo kwanini hawavitumii ipasavyo wakati wa ajali kama ya juzi Bukoba?

Madhaifu yote haya yangeepukwa kama muundo wa vyombo vya ulinzi na usalama vingeongozwa na wataalamu husika chini ya expert coordinators katika level zote kuanzia wilaya mkoa hadi taifa, badala ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom