Ajali ya moto Msamvu inaleta picha ya udhaifu wa vyombo vya usalama

Rejea mada tajwa hapo juu.Tangu ajali itokee asubuhi Polisi na vyombo vingine vya Usalama walikuwa wapi kufika kunako tukio na kutoa elimu kwa wakaz kuto lisogelea gari hilo.
Niwakati wa serikal pia kuweka vipind katika maredio na TV kuwaelimisha hasa vijana madhara ya uwiz wa mafuta pale magari yanapoanguka na kutiririsha mafuta.....! nawapa pole wale walioguswa kwa namna moja ama nyingine na ajal hio
MAONI
VIJANA tuchape kazi tuachane na tamaa ya vitu vidogovidogo ambavyo vitaleta maafa makubwa kwenye jamii
Kwani hujui hatari kila kitu serikali ikisimamie wewe ujisimamie kujua hatari hii ni kupenda vitu vya cheche
 
Hivi usalama wa taifa kazi yao ni nini ?

Kusikiliza umbeya wa chadema tu kila siku au

Yaani kwamba hiyo ajali hawakupata infos mapema watoe taarifa vyombo vingine viende hapo kuzuia watu

Hizi nyoka zinazosemwa zimesambazwa mtaani za UT znafanya kazi gani sasa ?

UT yeyote naomba anijibu haya maswali yangu
Kati ya matukio magumu kupambana nayo kwa watu wa usalama ni haya ya ghafla na yasiyokuwa na dalili ya kutokea.

Hata kama tunasema wana 6 sense ila ilikuwa ngumu kunusa tukio hilo, pia utayari wa polisi kuwahi kwenye tukio upo mikononi mwao na ni ngumu kuwahi kwenye tukio ambalo hujasikia maafa yametokea. Huwenda taarifa zilifika wakati bado zoezi la uchotaji mafuta likiendelea.

Agent yoyote yule wa UT ananusa mipango ya matukio siyo kuhisi vitu kama hivi. Hata wamarekani ambao wameendelea kwenye mambo ya usalama tunaona siku moja moja yanatokea matukio ambayo hawa wao wanashindwa kuyanusa BEFORE.
 
"Nendeni mkajihulishe na mkatafute ridhiki katika ardhi" wazee wameona sio poaa bora wakaitafute kwa pacha ake jahanam🤣🤣🤣🤣🤣
 
Pole kwa wafiwa,lakini serikali inalakujifunza katika hili. Ugumu wa maisha umekithiri hali ya maisha ni ngumu sana
 
Rejea mada tajwa hapo juu.Tangu ajali itokee asubuhi Polisi na vyombo vingine vya Usalama walikuwa wapi kufika kunako tukio na kutoa elimu kwa wakaz kuto lisogelea gari hilo.
Niwakati wa serikal pia kuweka vipind katika maredio na TV kuwaelimisha hasa vijana madhara ya uwiz wa mafuta pale magari yanapoanguka na kutiririsha mafuta.....! nawapa pole wale walioguswa kwa namna moja ama nyingine na ajal hio
MAONI
VIJANA tuchape kazi tuachane na tamaa ya vitu vidogovidogo ambavyo vitaleta maafa makubwa kwenye jamii
Acheni ujinga wa kutumia matukio kutafuta umaarufu, nani angetoa taarifa polisi au kwa wahusika kuwa kuna ajali ya gari ilihali waliokuwa eneo la tukio walikuwa bize kuchota mafuta. Acha ujinga watu wanaomboleza wamepoteza wapendwa wao. We kama hujaguswa endelea kutafuta umaarufu mitandaoni.
 
Kuchota Mafuta ni Wizi kweli, lakini kazi ya Polisi si kuzuia huo wizi. Watu walichota Mafuta kwa dakika 30 kama hivi, waliitana na kuitana, lakini wao hawapo. Mwisho wamekuja baada ya watu kuanza kuungua. Hawajui kilichitokea zaiidi ya kuwauliza mashuuda na waliochukua video kabla ya mlipuko. Hapo hakuna weledi kwa polisi ya kuzuia athari kwa wakati. Wawajibike na wao sasa.
Adhabu ya wizi siyo lazima uende jela ukafungwe. Hicho kilichowapata ni adhabu vilevile tena ya hapo kwa hapo. Mkiambiwa mfuate sheria bila shuruti hamtaki, haya moto umeamua kuwashurutisha mnabaki mnalialia hapa.
 
Ili polisi wafike mapema kwenye tukio inatakiwa ajali nayo itokee mapema. Ila ikichelewa na wao huchelewa.

Siwezi kueleweka.
Ni jibu zuri sana hili kwa mtu mpumbavu.
Hivi anafikiri polisi watatumia spidi gani kuizidi spidi ya moto wa petrol unapotokea.
Si kila kitu usimamiwe na serikali ukishakuwa na akili zitumie vizuri usisubiri serikali ije ikufundishe kwamba Lori ya mafuta ikianguka usiisogelee.
 
Rejea mada tajwa hapo juu.Tangu ajali itokee asubuhi Polisi na vyombo vingine vya Usalama walikuwa wapi kufika kunako tukio na kutoa elimu kwa wakaz kuto lisogelea gari hilo.
Niwakati wa serikal pia kuweka vipind katika maredio na TV kuwaelimisha hasa vijana madhara ya uwiz wa mafuta pale magari yanapoanguka na kutiririsha mafuta.....! nawapa pole wale walioguswa kwa namna moja ama nyingine na ajal hio
MAONI
VIJANA tuchape kazi tuachane na tamaa ya vitu vidogovidogo ambavyo vitaleta maafa makubwa kwenye jamii
Unajisumbua bure!
Tunafundishwa kila siku wizi ni dhambi.
Hao waliokufa wakiiba mali iliyoharibika baada ya ajali, hata kama ni adhabu kali, wanaistahili ili iwe fundisho
 
Adhabu ya wizi siyo lazima uende jela ukafungwe. Hicho kilichowapata ni adhabu vilevile tena ya hapo kwa hapo. Mkiambiwa mfuate sheria bila shuruti hamtaki, haya moto umeamua kuwashurutisha mnabaki mnalialia hapa.
Mwenye hadhabu hizo za jino kwa jino ni Mungu tu. Sisi Wanadamu tuna weledi na njia za kuzui jambo kabla halijaleta athari. Kama njia ya kuzuia ambayo pia ni kazi ya Polisi ilikuwepo, kwa nini hawakuifanya ?. Kumbuka Serikali ni Mlezi kwa Wananchi wake, kuwa mlezi maana yake ni Kuzuia Raia wako wakae Mbali na Hatari, iwe wanajua hiyo hatari au hawajui.
 
Mnapenda kuongozwa hadi kwenye uhai wenu. Polisi waje wawaambie msichote mafuta kwani hamkujua hata kuchota hayo mafuta ni wizi. Badala ya kuokoa maisha ya waliobanwa kwenye gari nyie mnakimbilia kuiba. Mkome na muache wizi
Ndio hvyo aisee watu hawajielewi kabisa.
Yaani Hadi uhai wako unangojea polisi serikali ije kukufundisha.
Hata huyo kuku wa broiler akiona hatari huwa anakimbia halafu wewe unaisogelea hatari eti unasubiri serikali ije.
 
Mwenye hadhabu hizo za jino kwa jino ni Mungu tu. Sisi Wanadamu tuna weledi na njia za kuzui jambo kabla halijaleta athari. Kama njia ya kuzuia ambayo pia ni kazi ya Polisi ilikuwepo, kwa nini hawakuifanya ?. Kumbuka Serikali ni Mlezi kwa Wananchi wake, kuwa mlezi maana yake ni Kuzuia Raia wako wakae Mbali na Hatari, iwe wanajua hiyo hatari au hawajui.
Kwani wao wananchi hawakujua kama wanachofanya ni hatari kwa maisha yao, ukiacha tu kwamba ni wizi je hata maisha yao hwakuona kama wanayaweka rehani? Yale magari yameandikwa maneno makubwa kila sehemu "DANGER" "HATARI" na alama ya moto imechorwa, je walidhani hayo ni mapambo?
 
Back
Top Bottom