Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,035
- 144,387
Baada ya hii ajali ya moto kutokea,Godbless Lema ambae bila shaka ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, jana tarehe 10/08/2019 kupitia mtandao wa twitter, alizitaka Mamlka husika kuwachukulia hatua Polisi/Fire mkoa wa Morogoro kwa uzembe ambapo alipingwa vikali na baadhi ya vijana wa Lumumba ambao walimbeza kuwa anaeleta siasa katka jambo hili.
Nashukuru leo Waziri Mkuu ameamua kuunda tume kuchunguza jambo hili na sasa nasubiri kuona hawa vijana waliombeza Lema watakuja na kauli gani baada ya ripoti kutoka na hatua kuchukuliwa.
Hizi hapa chini ni tweets za Godbless Lema za siku ya jana kuhusiana na ajali hiyo ya moto:
Eneo la ajali ya moto Morogoro ni karibu na Polisi/barabarani.Polisi walipaswa kulinda eneo.Watu wanauliza kwanini watu walienda kuchota mafuta? hakuna jibu linalo ondoa wajibu wa Polisi ktk kulinda uhai wa raia,ni sawa na kumuuliza mtu kwanini amenunua Tv wkt mtaani kuna wizi?
Uzembe mkubwa Polisi/Jeshi la Zimamoto wamefanya,ajali kama hii Polisi walipaswa kuzingira eneo lote ili Zimamoto washugulike,ingekuwa ni kuzuia mikutano ya kisiasa wangefanikiwa,nimetazama picha kuanzia mwanzo watu wanavyo chota mafuta unaona kuwa hili jambo lingeweza kuepukika
Nina toa pole kwa msiba mkubwa uliotokea huko Morogoro kwa ajali na kulipuka kwa gari la mafuta na kusababisha vifo/vilema.Natoa wito kwa Mamlaka za Serikali kuchukua hatua kwa Polisi/Fire Morogoro,kwa uzembe mkubwa ktk kusimamia ajali ya aina hii haswa baada ya kuwa imetokea