Ajali ya Morogoro. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya Morogoro.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Azikiwe, Dec 14, 2009.

 1. Azikiwe

  Azikiwe Senior Member

  #1
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazee ni kama nimesikia kuwa kuna gari la lililokuwa kwenye mashindano likaanja njia na kujeruhi watazamaji kandokando ya barabara.
  Kama kuna habari kamili tafadhali.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yeah ni kweli imetokea na wamekufa watu 5 na wengine majeruhi.
  Kwa vile mvivu kupeluzi ngoja nikutafunie wewe umeze tu.
   
 3. s

  smp143 Member

  #3
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kaka..habari kamili hii hapa

  Gari la mashindano laua watoto watano
  WATU watano wamekufa, kati yao wanne papo hapo, baada ya gari la mashindano ya mbio za magari kuacha barabara na kuparamia umati wa watu waliojipanga kando kando ya njia eneo la Mikese Njianne, wilayani Morogoro.

  Ajali hiyo imesababisha pia majeruhi 12 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

  Gari hilo lenye namba za usajili kutoka Kenya KAK 9208 aina ya Subaru likiwa miongoni mwa magari 16 yaliyoshiriki, liliandikishwa namba sita ya katika mashindano ya mbio za umbali wa kilometa 380 yajulikayo kwa jina la Morogoro Pathfinder Rally 2009 na iliendeshwa na dereva Dharam Pandya( 29).

  Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ferdinand Mtui, alithibitisha kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 4:30 asubuhi eneo la Mikese Njianne kwenye barabara ya vumbi.

  Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, watu waliokufa kwenye ajali hiyo ni watoto wenye umri kati ya miaka sita na kuendelea waliokuwa miongoni mwa watazamaji wa mashindano hayo.

  Alisema ajali hiyo katika barabara ya vumbi mara baada ya kufika Mikese Mizani, ambapo magari hayo yalitumia barabara ya kawaida na gari hilo lilipofika eneo lenye kona liliacha njia na kuwaparamia watu na kupinduka na hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao.

  Kati ya maiti hizo nne mmoja ndiye iliyotambuliwa kwa jina la Jacob Mashaka ( 6) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Awali katika Kijiji cha Mikese.

  Naye Ofisa wa zamu katika Hosptitali ya Mkoa wa Morogoro, Judith Kagimbwa, alithibitisha kupokea majeruhi 12 na miili minne.

  Alisema majeruhi mwingine alifariki akiwa wodini saa 7:30 mchana. Naye ni Said Mohamed ( 40) .

  Majeruhi 11 wanaoendelea kupatiwa matibabu ni Pamela Ashumba ( 50), Mgema Deus (16), Mwanaidi Rajab (21), Iddi Hamis ( 40), Hadija Mwarabu (28), Mwamini Said (28), Juma Abdallah (33), Alex Mussa (14) Daniel Masanja (12) na Shukuru Roma (28) ambao baadhi yao ni wakazi wa Mikese na wengine nje ya Mikese.

  Kwa mujibu wa Ofisa wa zamu huyo, majeruhi waliobakia walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu na timu ya madaktari wa hospitali hiyo.

  Akizungumza na HabariLeo, Ofisa Uhusiano wa Mashindano hayo, Pankaj Valambia, alisema kuwa kufuatia kutokea kwa ajali hiyo, wasimamizi wa mashindano hayo waliamua kusitisha mashindano hayo ili kushughulikia watu waliopatwa na ajali hiyo pamoja na taratibu kwa waliofiwa na ndugu zao.

  " Ni kweli ajali imetokea eneo la kona kali Mikese Njianne na kufuatia ajali hiyo utawala na wasimamizi wa mashindano haya wamelazimika kuyasitisha kabisa kwa lengo la kuungana na ndugu na jamaa ambao wamefikwa sambamba na majeruhi," alisema Ofisa Uhusiano huyo.

  Hata hivyo alisema Utawala na wasimamizi wa mashindano hayo wameamua kushirikiana na ndugu hao kwa kila hali ili kuwezesha kufanikisha shughuli mbalimbali zinazohitajika kutokana na ajali hiyo.

  Mashindano hayo yaliyoanza juzi kwa mbio za kilometa 41 na jana kwa kilometa 380 yalishirikisha magari 16 kutoka Mikoa ya Iringa, Der es Salaam, Arusha, Tanga na Morogoro na yalizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu juzi kwenye viwanja vya Gymkana, Morogoro.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
 5. Azikiwe

  Azikiwe Senior Member

  #5
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usijali, tafuna tafuna.
   
Loading...