Ajali ya Morogoro ni kafara?

Ajali ya Morogoro ni kafara?

Umeambiwa alikuwa anamkwepa mwendesha boda boda wewe unasema kafara. Akiongeacho mtu ndicho kiujazacho moyo wake
 
Kaa mbali mzee
tapatalk_1565525696166.jpeg
 
Zipo taarifa za miaka nenda rudi kuhusu ajali ya ma bus ya Abood kwa mfano. Mara nyingi hutokea maeneo ya Bwawani.

Yalisenwa mambo ya kafara kuhusu ajali ya MV Kagera.

Here we are again. Kafara kuhusu ajali ya Morogoro. Tumwachie Mungu. Anajua kilichomo na kisichokuwemo.
 
unaujua moto wa mlipuko lakini mkuu? Usiufananishe na moto unaoutumiaga ule unasambaa pande zote pindi tu kilipuzi kinapulipuka na moto unaweza kukukuta kokote pale mita chache toka kilipuzi kilipo.
Chukulia mfano mdogo tu wa bomu. Linapilipuka hata ukiwa mita labda tano toka eneo hilo lazima chamoto ukione. Vimbi la moto linatembea mkuu. Hakuna cha kafara wala nini. Waafrika tunaendekeza ujinga sana.
 
Tunayo safari ndefu sana watanzania. Kama kufikiri kwa baadhi yetu ndiyo kunakomea hapo basi , binafsi naona tunazo maili nyingi sana kule tuendako. Ndugu zangu kwanini tusijenge utamaduni wa kuuliza kwa lugha ya kawaida tu kwa kile usichokijua?
 
Hafu kuna watu wanawatetea wale wezi wa mafuta

Wamepata wanachostahili RIP KWA dereva konda na mama abiria pia na wapita njia wote

Anyway sipendagi unafiki najua ntakufa ila vifo vingine vya kujitakia sitaki nife kifo cha kujitakia nature circumstance sio ya kujitakia
Huu ni ujinga !
umeona uwe muwazi.
Marehemu huwa hawawasemi vibaya...
Ila nadhani Hawa majeruhi hawatarudia Tena huu ujinga.
 
Salama JF members,

Pole kwa wale waliopata msiba na majeruhi katika ajali ya Morogoro.

Mola awajalie marehemu wote Pumziko la Amani AMINA.

Naomba niende kwenye Mada husika,

Binafsi najiuliza kama ajali ya Morogoro ni KAFARA au SIYO KAFARA. Naomba kuainisha sababu zangu Kuu 2.

1. Eneo la Tukio, nimeangalia Leo asubuhi wakati PM akiwa eneo la tukio. Mazingira niliyo yaona ni kama vile Janga ni dogo ukilinganisha na idadi ya vifo na majeruhi.

2. Pikipiki zilizokuwa eneo la tukio zimeungua. Ila cha kushangaza Mipira ya Magurudumu ya Pikipiki ambayo ni PLASTIC haijaungua au kuungua kidogo.

Logic hizo mbili zinanifanya nijiulize kuwa ajali ya Morogoro ya Tarehe 10/8/2019 ni KAFARA au SIYO KAFARA

Nimeambatanisha picha ya eneo husika

Ahsanteni.
View attachment 1178331
Nichangie kwenye #2; iko hivi, tairi ikiwa imejaa upepo huwaga haiungui ikaisha yan. Ko ndo hivo jamaayangu!
 
Back
Top Bottom