Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

rostam kawashika pabaya wana JF

Leo CHADEMA wa JAMII FORUMS mnamtetea ROSTAM na kampuni yake ya VODACOM!!!!!


Kweli nimewavulia kofia
 

Hapana aliyesema kwamba watu wote wasifanye kazi, hiyo yako ni kuongeza chumvi. Ila ile 'miss miss' na magoma yake vingeweza kuwekwa pembeni.
 
Nyinyi viongozi acheni kupiga chenga, jibuni mawswali ya wananchi. Haya maswali yako yanahusika vipi na vodacom kama una akili ya kufikiri. Maswali yako yapeleke wizara inayohusika. Vodacom umeshaambiwa walikuwa wadhami tu.

That's my point. Money talks! Kinafanya watu waibane Vodacom ni nguvu ya kipekee waliyonayo kwenye haya mashindano ya ma-miss. Na wangesema wasogeze lingetokea hivyo. Hata hivyo nimesema kufanya kosa sio kosa bali kurudia, kwa nini masaa 24 baada ya blunder wasitoa official statement ya kuomba msamaha.

Watu wanaweza kubeza hizi kelele hapa jamvini lakini nakuhakikishia huko mbele kama litatokea janga kama hili (mungu aepushe mbali) utaona makampuni yatakavyoufyata. CCM wameshikishwa adabu (walau kiasi) na nguvu ya umma, sasa nguvu hiyo hiyo ya umaa inawashikisha adaby makampuni yanayojidai kuwa na kiburi kama cha ccm.

Mwisho, If I had my way mkuu wa TBC angetakiwa aende likizo ya moja kwa moja bila malipo.
 
Leo CHADEMA wa JAMII FORUMS mnamtetea ROSTAM na kampuni yake ya VODACOM!!!!!Kweli nimewavulia kofia
please ondoa siasa hapaina maana kuwa mtanzania mwenye huruma lazima uwe CHADEMA au CCM? Kama kuna mtu anatetea VODA kwa sababu ya masilahi sorry lakini hii wamechemshana VOdafone wakipata taarifa kuna kazi
 
please ondoa siasa hapaina maana kuwa mtanzania mwenye huruma lazima uwe CHADEMA au CCM? Kama kuna mtu anatetea VODA kwa sababu ya masilahi sorry lakini hii wamechemshana VOdafone wakipata taarifa kuna kazi


VODA ni kampuni ya kifisadi na inaongozwa na Fisadi sasa shida yenu ni nini leo kuwatetea hawa afisadi?
 

Mimi naona unaewaza kipuuzi ni wewe hapo. Hebu jaribu kutafakari tena kwa kina wewe mwenyewe.

Unajaribu kujenga hoja za kitoto kabisa!

Na hata hiyo TBC pia imesemwa sana kwa kujiita television ya taifa na wakashindwa hata kutoa breaking news. Na tunavipongeza vituo vya redio na television binafsi vilivyojitahidi sana kutoa taarifa kila baada ya muda na kuonyesha ubinaadamu kwa wenzetu waliopoteza wapendwa wao.

 
Kwakweli Miss Tanzania ingependeza kuahirishwa, walikosea....lakini naona sasa inakua opportunity ya Zantel kujitanua; opportunity ya wachache kukuza movements zao nk.Si mbaya kukataa misaada ya VODACOM lakini haya ya kwenda kwa wadhamini nk. sio kwamba yanavuka mipaka? ni swali tu msinipige mawe
 
ninavyoona mimi hapa tatizo sio kuendelea kwa shindano la umiss wakati msiba umetokea, ila ni kitendo cha star tv kuonyesha lile tukio live! kwa sababu kama ni starehe mbona nyingi ziliendelea wakati ule? TBC1 walikuwa wanapiga mipasho, kumbi zote za starehe zilikuwa zinaendelea kama kawaida, ligi kuu vodacom iliendelea kama kawaida, ufunguzi wa kampeni igunga uliendelea kama kawaida, redio zote ziliendelea kutwanga miziki! kwa hiyo kama tukio la umiss tz lisengeonyeshwa live na star watu wengi wasingejua kinachoendelea hivyo pasingekuwa na manung'uniko.
 

Kwani tatizo nini? si wamekataliwa misaada tu,sasa si warudi na pesa zao tu? au kutoa msaada ni lazima?
 
ROSTAM kiboko na namvulia kofia

99 % hapa mlikuwa mnasema jamaa fisadi leo mko stari wa mbele kuitetea kampuni ya mafisadi!

kweli ROSTAM kawashika pabaya nyie
 
Siku zote Wanzanzibari (serikali) hawajawahi kuunga mkono mashindano ya umiss. Partly for religious factors. Tukio la juzi ni coincidence tu kwa wao kuhalalisha walichokitaka siku zote. Mi nashangaa, badala ya kuzungumza kuwajibisha viongozi wazembe ambao kwa namna moja au nyingine wamepelekea kutokea kwa ajari hiyo public opinion inaelekezwa kwenye vodacam.

Pili ikumbukwe kuwa vodacom ni mshindani wa Zantel, kampuni ya Wazanzibar. Hii pia ni vita ya kibiashara. SINA HISA VODACOM , SINA NDUGU VODACOM WALA SINUFAIKI NAO KWA LOLOTE. WATANZANIA TUBADILIKE
 
Nina wasiwasi na chanzo cha hbri hii kama ni kweli.
Kama kususia basi si Voda tu, tv zilizoonyesha, waliojaza ukumbi, waandaaji na hata wewe uliyeangalia umeshiriki kufanikisha hii kitu.
Sasa msikurupuke kuiponda voda wakati mlikodolea macho mwanzo mwisho.
 

Leo CHADEMA wa JAMII FORUMS mnamtetea ROSTAM na kampuni yake ya VODACOM!!!!!

VODACOM mlikuwa mnalalamika ni kampuni ya FISADI ORIJINO leo imekuwaje?

Kweli FISADI rOSTAM kawashika pabaya
 
Kitu pekee Wazanzibari wanazuiwa kufanya ni kulaumu serikali yao. Wanaaminishwa kuwa tatizo n vodacom na hivyo hasira zao zinaelekezwa huko. Sijui bank atawasaidia.
 



Leo CHADEMA wa JAMII FORUMS mnamtetea ROSTAM na kampuni yake ya VODACOM!!!!!

VODACOM mlikuwa mnalalamika ni kampuni ya FISADI ORIJINO leo imekuwaje?

Kweli FISADI rOSTAM kawashika pabaya
 

Na ZANTEL ilisajiliwa wapi baada ya kukataliwa na TCRA? kuaeni na uhakika kabla ya kutoa hoja.
 

Mkuu naona una hasira tulia kidogo.
 
voda ni kampuni ya kifisadi na inaongozwa na fisadi sasa shida yenu ni nini leo kuwatetea hawa afisadi?

mimi sitetei mafisadi wala sijawahi kuungana nao, swala kwamba vodacom ni kampuni ya mafisadi ni kweli, lakini hoja inayojadiliwa sio kuikatakaa vodacom kwa mahusiano yake na mafisadi. Tunakataa hoja zisizo na kichwa wala miguu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…