''ni nani katika kamati hiyo ana utaalamu kunipita mimi?''
hakya mungu nchi hii!!!!!?
we acha tu.
Hizi tabia za kukatakata maneno ilikupata tafsiri tofauti ni tabia za kishetani!
''ni nani katika kamati hiyo ana utaalamu kunipita mimi?''
hakya mungu nchi hii!!!!!?
we acha tu.
Naomba kama kuna mwenye namba ya simu au e mail ya Dk. Mwakyembe anipatie. Natanguliza shukrani.
Ukweli plain truth ni short, simple na clear na direct to the point, kama Masia alivyosulubishwa bila kosa lolote
Hakuwa na maelezo mengi zaidi ya kusema 'wewe wasema'.
Dr ambaye yu mgonjwa, hakuhitaji kujisafisha kwa maelezo yote hayo na kuingia kwenye technicalities
Za kisheria kwa andiko safi la kiuandishi wa habari.
Angetulia tuu kwanza apone ndipo alonge.
Mengi alipowatukana mafisadi papa, kuna wenye busara walimuona ni mjinga fulani, Rostam alipomjibibisha na kumuita fisadi nyangumi, wale wenye busara wanamuona RA ndio mjinga wa wajinga. Jeethu pamoja na ufisadi wake, hajajibu, hajaitisha press conference, hajatoa statement yoyote na hatajibu chochote, huyo ndio wakumuogopa.
Ili Dr alinde heshima yake, hana haja ya kusema saana na andiko refu. Yeye tayari ni mheshimiwa na anaheshimiwa hata akikaa kimya.
Pamoja na kwamba bado naumwa na niko nyumbani nikipumzika kwa ushauri wa madaktari, nimelazimika kuvunja ukimya na kutoa taarifa hii fupi kuzuia upotoshaji wa makusudi unaofanywa na magazeti, hususan gazeti la Tanzania Daima, na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi kwa sababu wanazozijua wenyewe kuhusu suala hili.
''ni nani katika kamati hiyo ana utaalamu kunipita mimi?''
hakya mungu nchi hii!!!!!?
we acha tu.
Hizi tabia za kukatakata maneno ilikupata tafsiri tofauti ni tabia za kishetani!
Baadhi yetu tunashiriki kikamilifu kuwalewesha sifa viongozi wetu wazuri tu. Matokeo yake wakishalewa sifa hizi wanakuwa watu wa kulialia tu, kujitetea tu, kudhani wana maadui wengi tu, kuamini kuwa baya lolote kwao lina mkono wa mtu....Matokeo yake tunawapoteza kwenye uongozi wanabaki kukimbizana na vivuli vyao tu.
Ajali ya kujitakia hii .... Mwakyembe, siku nyingine awe makini, na amuache dereva afanye kazi yake na siyo kumlazimisha kuvunja taratibu za barabarani ... yeye ni abiria tu!!
Swali: Mbona Chenge alipogonga na kuuwa watu wawili alitokea kwenye TV na magazeti yakaandika na ni mwaka huu huu akielezea ilivyokuwa na tena akisindikizwa na polisi wengi. Au sheria na makatazo hayo ya polisi yamepitishwa lini au polisi wamesahau. Chenge ni Mbunge na Mwanasheria kama mwakyembe? Polisi wakitoa ufafanuzi na tofauti ya matukio haya mawili iatakuwa vizuri
Shangazi,
Usipotoshe ukweli hapa; case ya Chenge na mwakyembe ni tofauti. Ajali ilipotokea polisi na Mwakyembe walitoa taarifa zilizokuwa zinapingana. Moja ikisema waligongwa kwa nyuma na polisi wakisema hawakugongwa na badala yake ilikuwa makosa ya dereva.
Pia Mwakyembe alionyesha kama kulikuwa na uwezekano wa kutokuwa ajali ya kawaida.
Kwenye mazingira kama hayo ilikuwa vizuri kwa polisi kuunda tume ili kuhakikisha ukweli unapatikana. Kibaya zaidi hii ajali imetokea wakati Mwakyembe yuko kwenye malumbano na baadhi ya watu (mafisadi).
Kama ilivyo Tanzania, polisi hawakuwa makini kwenye uchunguzi wao; wameacha mapengo mengi ambayo sasa Mwakyembe anayatumia kuonyesha mapungufu kwenye taarifa yao.
Kwa ujumla hii case na ya Chenge ni tofauti. Chenge hakusema kwamba kunaweza kuwa na mkono wa mtu. Polisi wamefanya uchunguzi na case ya Chenge iko mahakamani. Hata uchunguzi wa case ya Chenge ulikuwa wa haraka, labda case ndio itachukua muda mrefu kusikilizwa.
Ninamheshimu sana Dr Mwakyembe lakini kwa kauli zake za kutatanisha naanza kuwa na mashaka na uwezo wake kiuongozi he looks like mtu wa mitaani.Please sir acha kubishana bishana.Utajiongezea heshima kwa sisi tunaokuheshimu.Hivi Mwakyembea mbona muongo hivi huyu Mbunge? Leo anadai alisema toka awali hii ni ajali, na hiki nini:
Mimi binafsi nilistushwa sana na taarifa ya ajali ya Mh Mwakyembe lakini baada ya maelezo kupatikana kutoka kwake na dereva wake na baadae Polisi nimepata ninashawishika kabisa kusema kuwa ni ajali ya kawaida ina kwa sehemu kubwa imesababishwa na uzembe wa dereva wa Mh Mbunge. Nikirejea maelezo ya awali kuwa lorry ndiyo lilikuwa linataka kuipita gari ya mheshimiwa na wakati huohuo mbele kwa upande mwingine kulikuwa kuna kuja basi la abiria, badala ya dereva wa mheshimiwa kupunguza mwenndo ili lorry litangulie, yeye akafanya maamuzi ambayo hayakuwa sahihi kwa kuongeza mwendo wa gari lake. Hali hiyo ilikuwa ni hatari kwa wale waliokuwa katika lorry na basi la abiria pia. Laiti kama asingeliongeza mwendo ni wazi angeweza kulimiki gari lake vizuri na kuondoa hofu aliyokuwa nayo kwa wakati ule.
Sasa nikirejea katika hayo maelezo ya Mh Mwakyembe, nadhani amekosea kabisa kufanya hivyo kwani nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria ambazo wao ndiyo watungaji. Hakupashwa kulalamika wakati huu ambapo tayari mamlaka husika zimesha sema kuwa tatizo alikuwa ni dereva wake na atafikishwa katika mahakama kujibu mashtaka. Haya ambayo Mwakyembe anayoyaongea alitakiwa akayatoe mahakama kama shahidi wa dereva wake na si vinginevyo. tafsiri inayojitokeza ni kuwa Mh anataka kupindisha shauri zima kwa ajili ya 'kumsaidia' dereva wake. Hayo ya kuanza kusema hii ajali inaweza kuwa na mkono wa mtu ni mawazo finyu sana kuongelewa na mtu kama mbunge kwenye hadhara.
Hofstede,Nakubaliana na wewe kabisa kuwa hizi case ni tofauti, moja iliua wawili na ilikuwa dar na nyingine hakuua na ilifanyikia Iringa
Ila kuna ukaribu wa hali ya juu hasa katika uundani wa kamati
Kamati iliyoundwa kwa ajili ya Chenge ilimchukua mpaka eneo la tukio na kumhojihoji kidogo kisha kufungua kesi ambayo mpaka leo haijulikani inaendelea vipi
Kamati ya ajali ya Mwakyembe ilitoa taarifa ikiwa ina ushahidi tosha kuwa Dereva wa Lorry hana makosa na wao walijua kila kitu kilichotendeka wakati wa ajali bila hata ya kumhoji Mwakyembe na Dereva wake. Sasa hapa ndipo tunajiuliza kuwa kuna nini?, iweje kamati itoe taarifa siku tatu tu wakati ile ya Chenge mpaka leo Ipo kimya?.
Ukweli ni kwamba wanasiasa wa bongo wanavipa wakati mgumu sana vyombo vya dola kufanya kazi kitaalam. Kila kitu ni maagizo tu fanyeni hivi fanyeni vile. Yaani mwanasiasa huyohuyo, hakimu huyo huyo, polisi huyo huyo and everything.
Wao wanaona wanalinda maslahi yao lakini kwa undani zaidi wanaiangamiza nchi kwa kiasi kikubwa. Huwezi kuwa na double standards katika kushughulikia mambo ni kinyume kabisa na utawala wa sheria ni kama tunatawaliwa kiimla.
Yaani ili uwe salama jipendekeze kwa aliyeshika dola vinginevyo huna haki hivi, siku akishika dola mwingine aliyenyimwa haki leo unatarajia na yeye afanye nini?. tunakoenda si kuzuri kama tutaendelea kuwa na viongozi wabovu wa fikra kiasi hiki.
Kwa nini Tume iwe na kiherehere cha kutoa taarifa bila kuwa na all facts on the table?, huku ni kuua professionalism. Ninaamini kabisa kuwa kuna undue influence towards all conclusion reached in Mwakenyembe's accident.
Tubadilike muda bado tunao tuache kutumia vyombo vya dola kwa manufaa ya wachache tutalipeleka taifa pabaya.