Ajali ya daladala (UDA) Kimara

Ajali ya daladala (UDA) Kimara

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
14,593
Reaction score
5,582
Kuna ajali ya basi la UDA imetokea maeneo ya kimara Suka,ambapo daladala hiyo iliyokuwa inatoka mjini kwenda MBEZI mwisho imeligonga lori (semi-trailer) iliyokuwa imeegeshwa barabaran ambayo ni mbovu,chanzo cha ajali ni kwamba dereva wa UDA amelivaa kwa nyuma lori hilo,hakuna mtu aliyekufa ila watu wamejeruhiwa sana,basi limepondeka kuanzia mbele,upande wa kushoto mpaka kwenye mlango wa kupandia abiria.

Mmoja wa abiria amejeruhiwa vibaya sana hasa mguu ambao umejeruhiwa kiasi cha mifupa kuwa nje kabisaaa kuanzia ugokoni mpaka mapajani.

Mi nimeishuhudia hiyo ajali baadhi ya abiria wanakimbizwa hospitali kwa bajaji.
 
mmh pepo la ajali linaanza tena ee Mungu tunusuru
 
Kuna ajali ya basi la UDA imetokea maeneo ya kimara suka,ambapo daladala hiyo iliyokuwa inatoka mjini kwenda MBEZI mwisho imeligonga lori (semi-trailer) iliyokuwa imeegeshwa barabaran ambayo ni mbovu,chanzo cha ajali ni kwamba dereva wa UDA amelivaa kwa nyuma lori hilo,hakuna mtu aliyekufa ila watu wamejeruhiwa sana,basi limepondeka kuanzia mbele,upande wa kushoto mpaka kwenye mlango wa kupandia abiria,mmoja wa abiria amejeruhiwa vibaya sana hasa mguu ambao umejeruhiwa kiasi cha mifupa kuwa nje kabisaaa kuanzia ugokon mpaka mapajan,
Mi nimeishuhudia hiyo ajali baadh ya abiria wanakimbizwa hospitali kwa bajaji

asubuhi hii,si kuna clear visibility hakuliona hilo lori?? na hio kimara suka sio dual carriageway??
 
Tatizo ni madereva wengi wa public transport wanawaza kufikisha hela ya boss, hawawazi kufikisha abiria salama na ndio maana magari huharibika hovyo
 
mwisho wa mwakaaaaaa da mungu tuepushe na madereva wakosao umakini
 
Jana kuna thread ya madai ya mishahara ya madereva wa UDA ililetwa hapa watu wakamjibu vibaya eti"jf ndio mwajiri wako!" Mawazo ya mshahara yamemfanya dereva aingie uvunguni mwa semi! Na si ajabu miongoni mwa majeruhi yupo memba mwenzetu aliyekuwa akijibu utumbo kwa jambo muhimu kama hilo! Pole sana majeruhi!
 
Madereva wa UDA wanatakiwa wawasilishe hesabu ya Sh 300,000 kwa kutwa! Lazima ajali ziwe nyingi.
 
Habari bila picha sio Habari...mleta mada rudi eneo la tukio ukapige picha....
 
Back
Top Bottom