Ukonga Dar: Ajali mbaya kati ya roli la mchanga na daladala aina ya Coaster

kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,694
2,134
Kuna jamaa imenitaarifu maeneo ya Ukonga Dar e s Salam, kati Magereza na Madafu kumetokea ajali mbaya, daladala aina ya coaster imepigwa ubavuni na roli la mchanga.

Kwa mujibu wa maelezo yake kuna majeruhi wengi na watu kadhaa wanahisiwa kupoteza maisha.

Kama kuna mtu yupo maeneo hayo tunaomba afuatilie tukio hili kwa karibu zaidi na atujuze kwa uzuri zaidi.
FB_IMG_1499143252446.jpg


Watu kadhaa wanahofiwa kujeruhiwa baadhi ikiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria (daladala) kugongana na lori la Taka eneo la Ukonga Madafu jijini Dar es Salaam.

Daladala hilo lifanyalo safari zake kati ya Gongo la Mboto na Makumbusho liligongwa ubavuni kuanzia mlangoni na kusababisha majeruhi hao huku wengine wakihofiwa kufa, wakati daladala hilo likitaka kulipita gari lingine.

Baadhi ya Mashuhuda wamesema dereva wa daladala alikuwa akijaribu kulipita lori lingine ndipo akataka kugongana na lori hilo uso kwa uso na katika harakati za kulikwepa likagongwa ubavuni na kujeruhi watu.

=======

WATU 18 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea saa 10:30 alfajiri katika eneo la Madafu barabara ya Pugu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani alisema ajali hiyo ilihusisha gari namba T 337 BKN Nissan Civilian iliyokuwa inatoka Gongo la Mboto – Mombasa kwenda Kariakoo kupitia Banana.


“Gari hilo liliigonga gari la mchanga namba T 656 DHL Scania 94 lililokuwa likitokea Banana kwenda Gongo la Mboto,.

“Watu 18 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa katika Hospitali ya Amana wakati wengine walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Hali za majeruhi watatu zilikuwa mbaya,” alisema.

Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha hospitali hiyo ilipokea majeruhi tisa na mwili mmoja wa marehemu.

Mwangomo aliwataja majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo kuwa ni Masiku Werema (45), Mohamed Juma (37), Adam Rashid (25) na Joshua Stephen (32).

Wengine ni Said Juma (17), Eliza Chacha (14), Maua Malick (48), Stella Mpahe (35) na Juma Mtally.

“Kati ya majeruhi hao, Adam Rashid alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya hali yake kutengamaa,” alisema.

Mwangomo alisema majeruhi wengine bado wamelazwa wakiendelea kupatiwa matibabu.
 
Asubuhi ya kwenda kutafuta riziki hii daaa wamekutana kila mmoja hawana kujali aina za hao madereva
 
Very sad news! May God rest in peace all those passed as a result of this incident and help those injured recover very soon....Amen
 
lile eneo lina barabara tatu sasa huwa kunakuwa na ushindani wa kutoka upande mmoja kuingia mwingine na nadhani hilo ndio limewatokea, ni hatari kwa madreva wazembe wasiotii kanuni za matumizi ya barabara, atahri zake ni kusababisha ajali
 
Yaani asbuh unawah kusaka Mkate unakumbana na Maswahibu,pole kwa malofa wenzetu
 
lile eneo lina barabara tatu sasa huwa kunakuwa na ushindani wa kutoka upande mmoja kuingia mwingine na nadhani hilo ndio limewatokea, ni hatari kwa madreva wazembe wasiotii kanuni za matumizi ya barabara, atahri zake ni kusababisha ajali
Ni kweli zile bara bara ndiyo chanzo kikuu hii utokana na watu hasa wabongo huwa si wafuataji wa sheria, zile njia zinahitaji busara sana.
 
Hizi barabara tatu serikali ingefanya mpango wa kuzifuta, naona imebaki hiyo tu baada ya hii ya mwenge morroco kujengwa na kuwa nne, nasikia lilikuwa wazo la mamvi
 
Back
Top Bottom