Ooh My God..nyingine tena!!!!
Kwa sababu serikali imeshindwa (kama imejaribu) kutatua tatizo la ajari barabarani hasa hizi za mabasi ya abiria, imefika wakati muafaka kwa viongozi wetu ikiwemo rais wa nchi, mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wote waandamizi wa serikali kuanza kutumia mabasi haya haya ya Ngorika, Hood, n.k. kwenye safari zao za mikoani. Pengine wote tukitumia usafiri huu, watunga sera na wasimamizi wa sheria wanaweza ku feel maumivu tunayoyapata kwa kupoteza ndugu zetu kwa vifo na wengine wengi kupata vilema vya maisha.
Nimemsikia Mkuu wa kikosi cha barabarani jana akiwaamuru wenye mabasi wote kuweka Speed governor, nikajiuliza je kipindi kile speed governor zilipowekwa ajali zilipungua/kumalizika???