Ajali ya basi la Upendo

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Ndugu zanguni, Asalaam Aleykum!!

Habari zilizosikika muda huu, Basi la Upendo litokalo Dar es Salaam kuelekea Iringa limepinduka mara mbili. Abiria wengi wamejeruhiwa. Kwa wale wenye ndugu waliosafiri na Basi hio tafadhalini muwasiliane nao kujua hali zao.

Source: Breking News Clouds FM
 
Basi la abiria linaloitwa Upendo lifanyalo safari zake Dar kwenda Iringa limepinduka sasa hivi, na watu kadhaa wamefariki.
 
Hii kali sana lakini naona kuna thread nyingine tena yenye habari hii naomba ziunganishwe tafadhali ili kupata urahisi wa kuchangia na kujua kinachoendelea
 
ooh jamani ajali tena!hivi Tanzania hauwezi kupunguza ajali kwani hawa traffic wanafanya nini huko barabarani?je ni kweli kwamba ajali haina kinga?tutandelea hivi mpaka lini?
 
poleni kwa mliopata ajali, jamani wakati umefika kwa serikali kuanza kukagua leseni za madereva, kwani ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wao, maana wapo walioenda kusomea na walioletewa nyumbani hapo ndo kunakuwa na mkanganyiko barabarani
 
Ndugu zanguni, Asalaam Aleykum!!

Habari zilizosikika muda huu, Basi la Upendo litokalo Dar es Salaam kuelekea Iringa limepinduka mara mbili. Abiria wengi wamejeruhiwa. Kwa wale wenye ndugu waliosafiri na Basi hio tafadhalini muwasiliane nao kujua hali zao.

Source: Breking News Clouds FM

Haya mabasi yanaendelea kutumaliza tu Watanzania. Tanzania ni moja ya nchi duniani ambazi zina ajali nyingi sana za magari. Mwenyezi Mungu azilaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wahusika wote wa misiba iliyotokea.
 
Niliwahi kugombana na dereve wa basi la Buffalo linatoka Arusha kuja Dar baada ya kuumuliza mbona mwendo ni wa kasi kiasi kile jamaa akanitolea macho eti mi mara yangu ya ngapi kupanda hayo mabasi....cha ajabu na baadhi ya abiria walichangia kunikejeli kuwa huyo ndio mnyama ukitaka kuwahi mjini basi ni mafuta kwa sana...baada ya kunusurika kupata ajali kwenye zile kona za Msambiazi kuelekea korogwe abiria wote tulikuwa kitu kimoja...wakati mwingine abiria tunachangia kuwafanya drivers waende mwendo kasi...anyway poleni wote mlioumia....
 
ooh jamani ajali tena!hivi Tanzania hauwezi kupunguza ajali kwani hawa traffic wanafanya nini huko barabarani?je ni kweli kwamba ajali haina kinga?tutandelea hivi mpaka lini?

Swali lako zuri sana, nafikiri KAITABA atatusaidia kufafanua - jana sikuiona hii post.
 
Da!! Poleni sana wenye ndugu yaani hawa Trafic na madereva wazembe kwanini wasihukumiwe kifo speed 160 ya nini hii itakuwa mwendo kasi tu maana sisi madereva wetu wa Ki TZ nilimbukeni na speed pamoja na abiria anatulia tulii hata kama basi lipo speed. POLENI SANA
 
Ooh My God..nyingine tena!!!!

Kwa sababu serikali imeshindwa (kama imejaribu) kutatua tatizo la ajari barabarani hasa hizi za mabasi ya abiria, imefika wakati muafaka kwa viongozi wetu ikiwemo rais wa nchi, mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wote waandamizi wa serikali kuanza kutumia mabasi haya haya ya Ngorika, Hood, n.k. kwenye safari zao za mikoani. Pengine wote tukitumia usafiri huu, watunga sera na wasimamizi wa sheria wanaweza ku feel maumivu tunayoyapata kwa kupoteza ndugu zetu kwa vifo na wengine wengi kupata vilema vya maisha.

Nimemsikia Mkuu wa kikosi cha barabarani jana akiwaamuru wenye mabasi wote kuweka Speed governor, nikajiuliza je kipindi kile speed governor zilipowekwa ajali zilipungua/kumalizika???
 
Poleni wahanga na waliofariki wapunzike kwa amani.
Hivi uchaguzi ukikaribiaga watu wanaendesha kwa rafu nini?
 
jamani ajali zitatumaliza, sijui tufanyaje kutatua hili janga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom