Poleni sana wafiwa kwa kuwa inaonekana vifo ni vingi kuliko idadi tuliyoambiwa.
Inasemekana bus lilikuwa limejaa kwa maana ya abiria 60, lakini tumeambiwa vifo ni 13 na majeruhi 25 kwa maana kwamba idadi ya abiria walioripotiwa ni 37 tu.
Tunawaombea wote waliojeruhiwa wapone upesi.
Bila kumumunya maneno, nikiri wazi ajali hii imetokana na uzembe mkubwa wa dereva wa basi.Hakufuata sheria za barabarani. Alitembea mwendo kasi mkubwa bila kujali anapita kwenye kivuko cha treni.Hakuchukua tahadhari.Alijiachia kama vile yuko peke yake barabarani.
Mamlaka zinazodhibiti vyombo hivi,wamewaamuru wafunge VTS.Pamoja na kuwa mabasi yamefunga vifaa hivyo,bado wanavunja sheria kila siku kwa kutembea mwendokasi usioruhusiwa kisheria na wachache tu ndio hupewa adhabu.
Jamii tumejaa ujinga mwingi kwa sababu tuliaminishwa ajali haina kinga.Kutokana na huu msemo,uzembe unaruhusiwa na kuonekana ni kitu cha kawaida. Hata dereva wa train alipaswa kujua eneo hilo anapaswa kupiga honi tangu mbali kutoa tahadhari kwa madereva wazembe wa mabasi. Hata kichwa cha train kilipaswa kuwa na taa zenye mwanga mkali ili kutoa ishara ya tahadhari. hata hivyo unaweza kuta hata dereva wa train naye alikuwa amelala usingizi wa pono.
Mungu atusaidie waja wake
Soma:
- Bus la Ally's lagonga Kichwa cha Treni Manyoni Singida, Watu 13 wafariki Dunia, 25 wajeruhiwa