Ajali Tabata, Dar: Mwandishi Mariam Mziwanda wa Gazeti la Uhuru anusurika kifo. Akimbizwa Muhimbili

Mwenyezi Mungu ni mwema.
Pole sana mwandishi wa habari.,.twakuombea upone haraka.

Maana, waandishi wengine huko wanakamatwa hadi na kikosi kazi cha Tanesco kana kwamba Tanesco ina jeshi la polisi.

Waandishi wengine wamepotea kusikojulikana.
Wengine wamuiliwa ...Mwangosi and the likes.

Twakuombea siha njema.
 
Neno la kwanza kutoka mdomoni kwake ilitakiewa " Asante Mungu nimetoka salama" instead analilia simu, c'moon
 
Unaposema mwendo kasi wa lory kwa dar nashindwa kuelewa, au siku hizi hamna foleni?
Vyuma vimekaza magari yamepaki, so hakuna foleni Dar, si jumatatu wala ijumaa, barabara nyeupeee
 
Mungu ni mwema.

Saa nyingine unatoka kwenye ajali halafu ukiangalia huwezi kuamini kama umepona
 
Ni ajari niliyoikuta maeneo ya Tabata majira ya saa sita kasoro usiku huu wa Feb 22, 2018

Majeruhi ni huyo aliyekuwa kwenye gari dogo lililo katikati ya hayo maloli na inasemekana ni mwandishi wa habari wa gazeti mojawapo hapa nchini na alikimbizwa Hospitali ya Muhimbili.

Naona ni Mungu ndo kaepusha kifo chake maana nadhani angekuwa chapati.

2cf2cb5d343f0b7981b62f5698d5c3c3.jpg
f058cfb9ce2c2dd795da60c8cefa6887.jpg

UPDATE:

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku huu baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT.

Kwa mujibu wa dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda.

Lori la mafuta na gari dogo yote yalikuwa upande wa kushoto wa barabara.

Imeelezwa lori hilo baada ya kuanguka lililibana gari dogo lililokuwa katikati.

Shuhuda wa ajali hiyo, Adeodatus Sylivester Charles amesema "Nilimtambua majeruhi kwani namfahamu tangu akiwa mtoto na sasa ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru".

Anasema baada ya ajali kutokea alikuta wasamaria wema tayari wanamtoa majeruhi kwenye gari akiwa ameumia sana.

“Nilikuta ametolewa kwenye gari yake akiwa ameumia sana, nikamsaidia kuvitoa vitu vyake kama simu na pochi na kumpelekea maana alikuwa analalamika simu yangu - simu yangu, na watu walikuwa tayari wameshasogea eneo la ajali wanagombania vitu hivyo.

Madereva wote wa malori walitoka salama bila majeraha ya aina yoyote.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE 03:30am:
Baada ya kupimwa kwa kupigwa picha ya C-Ray hospitalini Muhimbili imebainika hajapata madhara makubwa.
Naliomba Jeshi la polisi wafanye operation ya kuwakagua hawa madereva wa malori yanayotoka bandarini, niliwahi kuletewa mzigo uliokuwa kwenye kontena ya 40ft kutoka port mpaka masaki usiku wa manane (ndio time zao) dereva akawa anahangaika kupaki lori properly ili mzigo ushushwe, kwenda kumuangalia dereva, nakuta chalii wa kama 20years of age kavaa singlet na jeans mlege, yote tisa, kumi cabin nzima inanuka konyagi. Nilitamani kupiga yowe nikifikiria thamani ya mzigo wangu na hayo masaa yote kutoka port mpaka kwa mteja mzigo ulikuwa mikononi mwa huyu chalii ambaye hata kama ana leseni ya kuendesha lori kubwa vile hawezi kuwa na experience (which matters) na malori.
Hadi leo hii nikiona lori usiku limebeba contena huwa nakaa nalo mbali kabisa, hata nikigundua liko nyuma yangu, napaki pembeni apite tu!
 
Wengi wanaotumia majina kama hayo ni wale jamaa zetu wa kule nanilii. Wanapachikana na kupeana kazi kiupendeleo. Chunguza katika taasisi nyingi utagundua mkuu. Mtu anajiita John Michael John, wakati jina lake halisi ni John Michael Migomba. Ili kuficha chimbuko asilia.
Duh, kaazi kweli kweli.
 
HAAA KUNA MWANDISHI MMOJA ALIKUWA RAFIKI YANGU SANA ALIFIA HAPO TABATA RELINI NA KWA AJALI KAMA HII ALIKUWA ANAITWA DAN MWAKITELEKO
 
HAAA KUNA MWANDISHI MMOJA ALIKUWA RAFIKI YANGU SANA ALIFIA HAPO TABATA RELINI NA KWA AJALI KAMA HII ALIKUWA ANAITWA DAN MWAKITELEKO
Pia kuna mwana JF alikuwa anakaribia kufunga ndoa, akiwa anatokea kwenye kikao cha harusi yake alipata ajali na kufia hapo hapo Tabata Relini. Sijui kuna nini pale wallahi.
 
Pia kuna mwana JF alikuwa anakaribia kufunga ndoa, akiwa anatokea kwenye kikao cha harusi yake alipata ajali na kufia hapo hapo Tabata Relini. Sijui kuna nini pale wallahi.

Uendeshaji mbaya tu, hakuna cha nuksi au nguvu za Giza, tukifuata sheria na taratibu ajali kama hizi zitapunguwa
 
Naliomba Jeshi la polisi wafanye operation ya kuwakagua hawa madereva wa malori yanayotoka bandarini, niliwahi kuletewa mzigo uliokuwa kwenye kontena ya 40ft kutoka port mpaka masaki usiku wa manane (ndio time zao) dereva akawa anahangaika kupaki lori properly ili mzigo ushushwe, kwenda kumuangalia dereva, nakuta chalii wa kama 20years of age kavaa singlet na jeans mlege, yote tisa, kumi cabin nzima inanuka konyagi. Nilitamani kupiga yowe nikifikiria thamani ya mzigo wangu na hayo masaa yote kutoka port mpaka kwa mteja mzigo ulikuwa mikononi mwa huyu chalii ambaye hata kama ana leseni ya kuendesha lori kubwa vile hawezi kuwa na experience (which matters) na malori.
Hadi leo hii nikiona lori usiku limebeba contena huwa nakaa nalo mbali kabisa, hata nikigundua liko nyuma yangu, napaki pembeni apite tu!
Trafik wao wako busy na private car tu anajua akiparamia roli anaweza ambulia makofi na uhamisho juu
 
eti nini

simu??? yn mimi ht nisingewaza vilivyomo kwenye gari..ningewaz Uhai wangu na familia yngu...
 
Back
Top Bottom