Ajali Tabata, Dar: Mwandishi Mariam Mziwanda wa Gazeti la Uhuru anusurika kifo. Akimbizwa Muhimbili

Jan 4, 2018
22
26
Ni ajari niliyoikuta maeneo ya Tabata majira ya saa sita kasoro usiku huu wa Feb 22, 2018

Majeruhi ni huyo aliyekuwa kwenye gari dogo lililo katikati ya hayo maloli na inasemekana ni mwandishi wa habari wa gazeti mojawapo hapa nchini na alikimbizwa Hospitali ya Muhimbili.

Naona ni Mungu ndo kaepusha kifo chake maana nadhani angekuwa chapati.

f058cfb9ce2c2dd795da60c8cefa6887.jpg

UPDATE:

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku huu baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT.

Kwa mujibu wa dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda.

Lori la mafuta na gari dogo yote yalikuwa upande wa kushoto wa barabara.

Imeelezwa lori hilo baada ya kuanguka lililibana gari dogo lililokuwa katikati.

Shuhuda wa ajali hiyo, Adeodatus Sylivester Charles amesema "Nilimtambua majeruhi kwani namfahamu tangu akiwa mtoto na sasa ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru".

Anasema baada ya ajali kutokea alikuta wasamaria wema tayari wanamtoa majeruhi kwenye gari akiwa ameumia sana.

“Nilikuta ametolewa kwenye gari yake akiwa ameumia sana, nikamsaidia kuvitoa vitu vyake kama simu na pochi na kumpelekea maana alikuwa analalamika simu yangu - simu yangu, na watu walikuwa tayari wameshasogea eneo la ajali wanagombania vitu hivyo.

Madereva wote wa malori walitoka salama bila majeraha ya aina yoyote.

Chanzo: Mwananchi

UPDATE 03:30am:
Baada ya kupimwa kwa kupigwa picha ya C-Ray hospitalini Muhimbili imebainika hajapata madhara makubwa.
 
Ni ajari niliyoikuta maeneo ya Tabata majira ya saa sita kasoro usiku huu wa Feb 22, 2018

Majeruhi ni huyo aliyekuwa kwenye gari dogo lililo katikati ya hayo maloli na inasemekana ni mwandishi wa habari wa gazeti mojawapo hapa nchini na alikimbizwa Hospitali ya Muhimbili.

Naona ni Mungu ndo kaepusha kifo chake maana nadhani angekuwa chapati.

2cf2cb5d343f0b7981b62f5698d5c3c3.jpg
f058cfb9ce2c2dd795da60c8cefa6887.jpg
Duh ashukuru sana uwepo wa hilo Lori la mafuta aisee lasivyo tungempoteza
 
Ni ajari niliyoikuta maeneo ya Tabata majira ya saa sita kasoro usiku huu wa Feb 22, 2018

Majeruhi ni huyo aliyekuwa kwenye gari dogo lililo katikati ya hayo maloli na inasemekana ni mwandishi wa habari wa gazeti mojawapo hapa nchini na alikimbizwa Hospitali ya Muhimbili.

Naona ni Mungu ndo kaepusha kifo chake maana nadhani angekuwa chapati.

2cf2cb5d343f0b7981b62f5698d5c3c3.jpg
f058cfb9ce2c2dd795da60c8cefa6887.jpg
Aisee, inatisha
 
Najaribu kutafakari imekuaje wakutane wote 3 hapo nashindwa kuelewa....huyo mwenye kontena imekuaje akapanda pembezoni huko?
Siku zake zilikuwa hazijafika mkuu. Kama hazijafika hata iweje hufi lakini kama ndo muda umewadia unaweza hata kupaliwa na maji tu ukakohoa mpaka kukata roho. Yote kwa yote Mungu ni mwema ‍♂️
 
Back
Top Bottom