Ajali nyingine mbaya Mohamed Trans

Ajali nyingine mbaya Mohamed Trans

mwanafyale

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2010
Posts
1,641
Reaction score
539
Nimepata taarifa usiku huu kuwa kuna ajali mbaya imetokea barabara ya Moro-Dom iliyohusisha basi la Mohamed Trans. Ajali imetokea eneo la kijiji cha Kiegea. Waliokufa hapo hapo watu 5 na majeruhi ni wengi sana karibu basi zima.
Walioko eneo la tukio watuarifu wana jamvi
 
Let them rest in peace...Mungu awaponye majeruhi!!
 
basi linatoka wapi linakwenda wapi? ajali imetokea saa ngapi?
 
Kama ni kweli RIP waliotangulia
 
Mkuu, Mohamed Trans ya kutoka mkoa gani?
 
Waliokufa hapo hapo watu 5 na majeruhi ni wengi sana karibu basi zima.
Walioko eneo la tukio watuarifu wana jamvi

Nasikia kati ya hao watano, kuna Mhadhiri wa UDOM.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina.
 
Mabasi mengine si ya kupanda ni full ushirikina wa Kutoana damu si waende benki ya damu waanyweeeee
 
Lol! Chanzo ajali ni nini?


Mwenyenzi MUNGU Baba wa rehema awape pumziko la milele marehemu wote shambani mwake!

Na hata majeruhi wote Bwana wape nguvu wapone mapema Baba!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa! Jina lake na lihimidiwe!

Aamen!
 
Jana Kibamba kulikuwa na foleni jioni kuna Mohemed Trans ilipita upande wa pili wa Barabara kwa Mwendo wa kasi kila mtu akishangaa km ndio hyo iliyopata ajali bc dereva alianza fujo Mapema
 
Mungu atuepushe na majanga ya ajali za mara kwa mara. Wahusika wawapime madreva kabla na katikati ya safari kwa usalama wa abiria.

RIP marehemu na GWS majeruhi.
 
Alafu juzi nilifika pale Millenium business compound kumsindikiza mtu, nilichunguza madereva walivyo nimegundua wengi ni vijana alaf mambo ya uswahili ni mwingi....unyonyaji ni wa hali ya juu hasa kwenye mizigo!
 
Jana Kibamba kulikuwa na foleni jioni kuna Mohemed Trans ilipita upande wa pili wa Barabara kwa Mwendo wa kasi kila mtu akishangaa km ndio hyo iliyopata ajali bc dereva alianza fujo Mapema
Hili basi huwa linatoka dodoma saa kumi na mbili asubuhi linafika dar saa 6 au 7 na saa nane na nusu linageuza to dodoma nadhani ndio hili maana si linatembea ni linapaa huo mwendo wake.....
 
Nasikia kati ya hao watano, kuna Mhadhiri wa UDOM.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina.

Ni kweli...
Anaitwa Bernadeta Minja she was my friend and School mate
May her Soul Rest in Peace
 
Back
Top Bottom