Ajali Nyingine Iramba Ndani ya Masaa Mawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali Nyingine Iramba Ndani ya Masaa Mawili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by S2dak_Jr, Sep 8, 2012.

 1. S2dak_Jr

  S2dak_Jr Senior Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi,

  Nadhani mtakumbuka nilikuja na thread ya Ajali Mbaya ya Hiace Jimboni kwa Mwigulu Nchemba masaa mawili yaliyopita.

  Muda huu kuna taarifa ya kuwa mtu mmoja amefariki baada ya kuanguka kutoka juu ya gari la Mnada mpaka chini kwenye lami.

  Ajali hii imetokea maeneo ya Kiomboi ambapo leo Mh. Mwigulu Nchemba amemaliza kikao cha siku mbili na wanaCCM wenzake.

  Kwa wale wanaofahamu magari ya Mnadani huwa yanajaza mizigo mingi na wenye mizigo kukaa juu ya hiyo mizigo.

  Hiki ni kifo cha nne ndani ya masaa mawili, ukiacha vile vifo vitatu vya Hiace nilivyoripoti hapa jamvini.

  My take: Mpaka sasa sijajua leo kuna balaa gani kwenye barabara hii.

  Source: Duru za Kipolisi.
   
 2. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,348
  Likes Received: 6,698
  Trophy Points: 280
  vipi kiongozi nasikia pia treni imeanguka huko saranda!!hebu wapigie jamaa wa huko utuletee habari kamili!
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Tuliambiwa Dr.Mwakyembe, Dr. Nchimbi, IGP Mwema wamepata Mwarubaini wa ajari za barabarani nchini. Je huyo dawa bado haijaanza kufanya kazi au haina nguvu kupambana na ugonjwa?
   
 4. m

  markj JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  mwarobaini ni sisi raia kumrudia mungu kwani ajali nyingi sasa ni kutokana na watu kusahau mungu yu wapi! watu wanatoana makafara tu barabarani tena sana, asilimia 95 za ajali kwa sasa ni watu kujumlishia na ushirikina, sasa si dhani kama hawa wakina mwema hapa watakuwa na uo mwarubaini, watz tumekuwa na roho maya ni kuuana tu sikuizi kishirikina hasa kwenye haya maajali ya barabarani na ukitafuta sababu ya ajali unaweza ukashangaa kama kweli ndio ilo sababisha yote hayo, sasa wengine wanaomiliki mabus ya usafiri ni lazima anaamini atoe kafara watu, sasa hapa wakina wakyembe wanafanyaje? au waanzishe kila bus na vyombo vingine vya usafiri viwe na watu wa ibada na nyenzo mablimbali za ibada kwa dini zote umo ndani, labda itasaidia
   
Loading...