Kwa utawal huu tume itakuwa imeishaandaliwa majibu ya kutoa kwa walioiteuaWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtangaza
Jenerali Mstaafu George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza ajali ya
Mv-Nyerere na kutoa mwezi mmoja ili tume hiyo itoe majibu na mapendekezo juu ya hatua ambazo serikali inapaswa kuzichukua.
Akizungumza na wananchi wa Ukara Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea na hatua za awali za kuhakikisha inawachukulia hatua waliosababisha ajali hiyo na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Hatua za awali zilishachukuliwa tulishakamata wale wote ambao waliruhusu watu kujaa, na uchunguzi unaendelea, tumeunda tume iliyojaa wataalamu na vyombo vya dola ilitubaini nani hasa muhusika, tume ina watu saba na inaongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.Nimewapa mwezi mmoja ili kutoa taarifa ya tukio hilo .”
Source: millard ayoView attachment 876235