Ajali mbili maeneo ya Ifunda Iringa,trafic busy na kuchota mafuta.

Kisoma

Member
Dec 18, 2011
32
1
Nipo ndani ya basi natokea Mbeya,maeneo ya Ifunda tumeshuhudia gari moja dogo limeanguka na mbele kidogo tumekuta lory la mafuta limeanguka up side down na tenki limetoboka.
jambo la kusikitisha kwenye ajali ya gari dogo hakuna hata polisi mmoja ila kwenye lorry kuna difenda 3 na polisi wako bize kuchota mafuta wakishirikiana na raia wa eneo hilo.
jambo la kusikitisha zaidi dereva wa basi letu anawapa taarifa na kuwaambia kuwa kuna watu wamekufa mita kama 300 hivi nyuma wanampungia mkono na wanaendelea kuhifadhi mafuta wakati kuna watu(majeruhi) wanahitaji huduma yao.
 
Polisi wanaongoza uporaji ukiwaripoti watadai wanalifanyia uchunguzi na si ajabu wakakugeuzia kibao
 
Back
Top Bottom