Madereva wengi arusha wana matatizo makubwa yanayofaa kufuatiliwa sana na askari wa usalama barabarani, Wanapenda sana ku'overtake' tena wakati mwingine katika mazingira yenye utata sana, pia wanapenda kuendesha nje ya barabara (kushoto) kuwapita walioko kwenye foleni ndogo inayotembea bila kujua wanachoenda kufanya huko mbele ni kupiga pini na kusababisha msongamano au foleni kuwa kubwa zaidi, na hii huwafanya walio na subira kukaa katika foleni hiyo ndogo inayotembea kuonekana hawana haraka au ni wajinga. uzembe huu unafunbiwa macho na wana usalama na matokeo yake tunayaona.
pia utumiaji mkubwa wa miraa na viroba wakati wa kazi nalo ni tatizo kwa madereva wengi arusha...
kwa kifupi wanausalama hawajui kazi yao hapa wanachokifanya ni kukamata magari ya private na kuuliza "hii gari ya nani?" wakiacha daladala zikivunja sheria.