Ajali mbaya ya ndege kutokea Tanzania soon

Kakajambazi:

Ni jambo zuri ulilofanya kushikisha watu jambo hili. lakini naomba Forum imejaa mizaha sana. Naomba kukuuliza:
  1. Je wewe ni mlokole?
  2. Je, umeshawahi kusikia huduma kama vile New Life in Christ, Prayer action Tanzania, Vikundi mbali mbali vya maombi? au hata kanisani kwako. Could you please share this vision with your local pastor. Anaweza kukupa ushauri wa kufanya au hata kuomba pamoja naye, ili Mungu aonyeshe dhahiri nini kiko mbele ya nchi ama Taifa.
Ubarikiwe.

Mkuu mimi kwa sasa nimeokoka.
 
Kuna kijana mmoja alikuwa anafanya kazi nyumbani kwetu; siku moja nikamuona ameshika gazeti na akaanza kucheka sana, nilipomuuliza unacheka nini aliniita na kunionyesha picha ya Mugabe na kudai huyo ni kaka yake (alisisitiza sana). Siku ya pili asubuhi hakutokea na tukaletea taarifa UCHIZI umeshampata. Kule kusini wanasema CHALUVA....!!!!
 
binafsi nimewahi kuwa trained to ''sense danger''........haya mambo yapo...wewe kakajambazi hilo unalosema lipo na inaonekana una kipawa kikubwa sana.....hebu ni pm yawezekana ukatufaa wewe
 
Sina ndugu anayepanda ndege, ianguke ili yule mwenye uchafu wa mawingu auumbuke japokuwa kajitahidi kucheza fair play kwenye mswada wa katiba
 
Tapeli wa kimataifa, TB Josghua katangaza, Mugabe hana zaidi ya siku 60, nadhani zimebaki 55 sasa, wewe unakuja na ajali ya ndege ndani ya miezi 6. Kongo ndani ya wiki mbili zimeanguka mbili, tanzani ikianguka hatushangai, kwani kitambo tangu ile ya mbeya
 
binafsi nimewahi kuwa trained to ''sense danger''........haya mambo yapo...wewe kakajambazi hilo unalosema lipo na inaonekana una kipawa kikubwa sana.....hebu ni pm yawezekana ukatufaa wewe

kwani wewe huwezi ku pm? wacha kumfariji
 
Tabia yako a kuibia majeruhi ndo inakupa mawazo haya, umeona siku hizi watu kwenye mabasi hawatembei na pesa unaanza kuwaza ndege. Acha tabia ya kuibia majeruhi mkuu, siku nyingine utawaza nyumba yako iungue ili ujiibie

Kuna kitu kinaclick kwenye akili yangu kila mara kinachoniambia kuwa kunaajali mbaya ya ndege itatokea tz soon, ndani ya miezi sita ijayo.
Nimejaribu kui-deny hii hali lakini nimeshindwa.

Naombeni muendelee kuomba na kukemea nami, ili hali hiyo isitokee kwani utakua msiba mkubwa na wenye gharama kwa taifa.
 
Kwa hiyo Pasco, Na wanaoponya kwa Jina la Yesu (in the name of Jesus Christ) nao wanaponya kwa nguvu za giza?

Hii imekaaje lakini?je, shetani anaweza kuufitini ufalme wake mwenyewe?

Ni kweli ukisoma Biblia Mathayo 24 ile sura yote inazungumzia huo mwisho utakuwaje, Yesu aliwaonya wanafunzi wake kwamba watakuja manabii wengi wauongo, nao watafanya miujiza na ishara kubwa kwa jina lake,

Tatizo ni jinsi gani unatofautisha?

Can you assist? hasa hapa kwenye utabiri, maana wengine wanatabiri vinatokea vyote (e.g T.B. Joshua) mfano anapoombea wanandoa wasiopata mtoto zaidi ya miaka 10, in a year time wale wanandoa wanarudi kutoa ushuhuda na watoto mikononi au mimba, ni nini ile, ni nguvu ya nani ile jamani natamani nijue
Si lazima kila anayeponya, kufukuza pepo au kutoa unabii awe anafanya hivyo kwa mamlaka ya Yesu kwani hata Yesu mwenyewe alishatuonya kwamba watatokea watu watakaodai kutenda hayo na mengi mengineyo kwa jina lake ingawa kiukweli watakuwa wakitumia nguvu za yule aliye mwovu. Siku ya mwisho atawakana na kuwafukuzilia mbali na kuwaambia waziwazi"Ondkeni ninyi mfanyao maovu maana sikuwatuma". Kwa hiyo utitiri wa hawa vibwetere wanaojinadi kama manabii, mitume, wachungaji na takataka nyinginezo kwa matendo yao wanathibitisha ndiyo walewale waliotabiriwa. Mwenye masikio na asikie.
 
Mimi nimeoteshwa aina ya ndege ni gulf sijui nini vile kwani jina lake nileona gulf na kama mkondo wa maji vile ilikuwa inachangnya kidogo ile ulikuwa msiba wa aina yake kwani hata bendera zilipeperuka nusu mlingoti kwa muda, watu wakawa hawaelweki?? jeshi likawa kama lina asi vile in short was my worse dream ever
 
Tapeli wa kimataifa, TB Josghua katangaza, Mugabe hana zaidi ya siku 60, nadhani zimebaki 55 sasa, wewe unakuja na ajali ya ndege ndani ya miezi 6. Kongo ndani ya wiki mbili zimeanguka mbili, tanzani ikianguka hatushangai, kwani kitambo tangu ile ya mbeya

Ndugu, please hold on your lips! Uwe na ushahidi wa utapeli anaofanya, otherwise NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK!
 
Avatar ya mtoa mada na maono yake vinafanana,huenda anapanga kufanya kitu mbaya kwenye kale kandege ketu ka bei mbaya,hakyanani baba M akiiona hii...
 
Hapo kwenye bold mi simo! nakushauri subiri hizo siku zikiisha ndipo utamka ulivyotamka,sometimes mihemko ina matatizo sana!
Tapeli wa kimataifa, TB Josghua katangaza, Mugabe hana zaidi ya siku 60, nadhani zimebaki 55 sasa, wewe unakuja na ajali ya ndege ndani ya miezi 6. Kongo ndani ya wiki mbili zimeanguka mbili, tanzani ikianguka hatushangai, kwani kitambo tangu ile ya mbeya
 
Mimi pia nimeshwahi kujiwa na mawazo haya lakini sio ndoto, ninachofanya nikipata mwazo haya ni kumuomba Mungu-(Yahwe, Yehoha na Mkuu wa kila kilichopo duniani )aepushe mbali mawazo hayo na anipatie amani nafsini...,!!

ila pia angalia ndoto hzo unaota wakati gani...ujue ukishiba sana nako waweza jikuta unaota ndoto za ajabiu ajabu, pia ukiwaza kitu sana wakati unapolala uwezekano wa kukiota ni mkubwa! So sio kila unabii ni unabii, zipimeni hizo roho ili muone kama zinatoka kwa Mungu wa mbinguni au ni roho za kishetani au ni shibe tu ilipelekea kuota ndoto za namna hiyo....
 
Hata mimi nimekuwa na kitu kiclick kuwa kakajambazi atakufa muda si mrefu. Nimejarib kukipinga bila mafanikio. Hata hivyo Yesu aliwahi kututahadharisha kuwaogopa waota ndoto kama ukoma. Au kakajambawazi unajenga mazingira ya kutaka kuchukua ukanda wa shehe tapeli yahaya? si useme tu.
 
Back
Top Bottom