Ajali mbaya ya ndege kutokea Tanzania soon

Mkuu pole nadhani ni roho ya unabii. Mimi pia nina hali hiyo ila nikipata maono hayo nisipomwambia mtu jambo hilo hutokea. nikisema kwa mtu halitokei.
Bubu Msemaovyo na Kaka Jambazi, najua baadhi ya watu wasiojua mambo haya, watawaona kama machizi fulani, lakini sisi tunaoelewa tunaelewa mnazungumza nini.

Nyinyi wote wawili mna vipaji na vipawa vya kuona mbali, wenzetu wanaita, preamonition na precognition, kama manabii walivyokuwa na uwezo wa kujua yajayo. Ni watu wengi tuu wana vipawa/vipaji hivi ila hawajijua, ila wengine jambo likishatokea, ndipo wanakumbuka kuwa tukio kama hilo, waliwahi kuliona.

Wengine wanaonyeshwa tuu kama 'vissions', maono na wengine wanaonyeshwa ndotoni, ila hiyo ndoto inakuwa inajirudia rudia.

Hizo ni works of powers zinazoitwa "PSI", au "psychic" kila mtu anazaliwa nazo, ila kadri anavyokuwa, zinapotea kidogo kidogo, ila wengine Mungu anakuwa amewajalia kuzimaitain. Wale wanaoligundua hili mapema, wakizishapen, zinafanya wonders!.

Wenzetu wazungu wameshazifanyia research na ukigundulika unazo, wewe ni tajiri!. Haku kwetu wale wanaogundulika kuwa nazo, vibabu na vibibi, vinawawahi na kuwageuza au wachawi, au waganga etc.

Baadhi ya mashirika makubwa ya ndege, likiwemo British Airways, wamewaajiri watu kama hawa, ili kuzui ajali za ndege zake, hutakaa usikie BA imepata ajali!.

Nguvu hizi zinafanya kazi kwa kutumia "power of Mind", au "will Power" zimegawanyika katika makundi mbalimbali namiongoni mwake ni
Faith Healing-Kutibu kwa imani (wengi wakiita miujiza).
Demon Casting -kufukuza mapepo (watu wa dini wakiita kukemea, wasahili wakiita kupunga mashetani)
Telepathy-Kuwasiliana bila kuonana
Telepotation-Kuhamisha kitu bila kukigusa
Levitation- Kupaa juu na kuelea hewani.
Metal Bending-Kupinda vyuma bila kukigusa.
Precognition-Kutambua yajayo kabla hayajatokea.
Preamonition- Kutabiri yajayo
Clayvoyance-Kuzungumza na waliokwisha kufa ili kuuliza ulipo urithi etc (kiafrika kuzungumza na mizimu"
Dowsing-Kutambua mahali ardhini ambapo zimechimbiwa mali, maji au madini (Myahudi Uri Geller" ni tajiri mkubwa kwa kugundua yalipo mafuta au madini, na mkataba wake ni just 1% ya net profit).
Astral Travel- Kutembelea ndugu jamaa na marafiki bila wao kukuona (huku tunawaita wanga)
etc etc.
Etc, etc.
Topic hii ni ndefu, mimi nimesoma for leisure mambo haya na nina hazina kubwa ya vitabu kuhusu mambo haya. Nilipanga nikitulia, nimshauri mode aanzishe jukwaa rasmi la "Mambo Makuu ya Ajabu na Kweli" ili kuwabaini watu hawa na kuwasaidia ku channels hizo powers walizonazo through a good use!.

Angalizo: The deviding line between source ya nguvu hizo kama ni nguvu za Mungu au ni nguvu za giza, is very thin!. Mimi ni Mkatoliki na kuna vitabu nimesoma wanadai Katoliki ni demonics!. Kuna watu wenye nguvu za uoni nimewahi kuzungumza nao, wameniambia wachungaji karibu wote kuanzia Benny Hinn, T.B Joshua, Mwingira, Kakobe, Lusekelo, Rwakatare etc, wote wanatumia nguvu za giza kufanya uponyaji japo wanalitaja jina la Bwana!.

Mtu huyo aliniambia, kile kifungu cha Biblia Takatifu kinasema wazi "Omba Utapewa"!. Amesisitiza Mungu wa ukweli, analo jina lake hali, neno 'Mungu" ni cheo chake tuu ndio maana kuna miungu kibao, ili kufanyiwa miujiza kwa jina la Mungu, wote wanaotibu kwa jina la Mungu, au Bwana, wanatibu kwa kutumia jina la cheo tuu na sio jina halisi!, akasisitiza Shetani ndio amejidisguise na kulitumia jina la cheo cha Mungu, ila uishie hapo hapo kwenye kutaja cheo, bila kulitaja jina halisi la Mungu, hivyo shetani atafanya kila kitu ikiwemo hiyo miujiza ili kumake bilieve kuwa anayefanya ni Mungu!.

Jee tutajuaje kuwa miujiza hii ni ya shetani na sio ya Mungu?. Hii ni topi inayojitegemea!.

Pasco.
 
Kuna kitu kinaclick kwenye akili yangu kila mara kinachoniambia kuwa kunaajali mbaya ya ndege itatokea tz soon, ndani ya miezi sita ijayo.
Nimejaribu kui-deny hii hali lakini nimeshindwa.

Naombeni muendelee kuomba na kukemea nami, ili hali hiyo isitokee kwani utakua msiba mkubwa na wenye gharama kwa taifa.
Sheikh Yahya Husein has been reincarnated!!!
 
Tumekwisha zoea kuzika hata hiyo ajali ya ndege ikitokea watakaokufa tutawazika na hawatakuwa wengi zaidi ya hao waliokufa wakati wa mgomo wa madaktari akiwemo Mwenyekiti wa wazee wa ccm Dodoma!!!
 
kakajambazi hiyo kitu inaclick kivipi?unaota ndoto au unahisi kwa sababu ndege zetu haziaminiki??ukienda kituo cha mabasi ubungo na kuwatangazia wasafiri kuna ajali mbaya itatokea nafikiri wengi wataamini kwa sababu ya uchakavu wa mabasi yetu''
Wewe ni nabii au mchungaji au ni nani??
 
abiria watarajiwa ndo hawa
tanzania-cabinet.jpg
CCM+NEC+NOV1.jpg
 
kakajambazi hiyo kitu inaclick kivipi?unaota ndoto au unahisi kwa sababu ndege zetu haziaminiki??ukienda kituo cha mabasi ubungo na kuwatangazia wasafiri kuna ajali mbaya itatokea nafikiri wengi wataamini kwa sababu ya uchakavu wa mabasi yetu''
Wewe ni nabii au mchungaji au ni nani??

Imetokea mara mbili kwenye ndoto na wakati mwingine nahisi huzuni flani hivi nikiwa relaxed,mara ghafla mawazo ya ajali yananijia, usiku wa leo pia imetokea, baada ya kumaliza kukemea, niliwasha tv, nikakuta matukio ya ajali za ndege mbalimbali miaka 70s KLM, Panama etc, Nikajiuliza what a coincedance!!
 
Pasco uko juu! Nemependa telepotation. Nikawaza mbali. Nakaa karibu na benki. Nikipata nguvu hizo mwanangu si nitakuwa njema?
Ila mleta mada jina lake linajielezea kuwa zile roho alizozitenda kutokana na kazi yake ndo zinamletea mauza uza hayo.
Enenda zako ukatubu kwa Mungu wako. By the way jina huumba..........
 
Pasco uko juu! Nemependa telepotation. Nikawaza mbali. Nakaa karibu na benki. Nikipata nguvu hizo mwanangu si nitakuwa njema?
Ila mleta mada jina lake linajielezea kuwa zile roho alizozitenda kutokana na kazi yake ndo zinamletea mauza uza hayo.
Enenda zako ukatubu kwa Mungu wako. By the way jina huumba..........
Ukiziabuse, zinatoweka!.
 
Unachezea utajiri mlangoni.Fungua ofisi, wenye kuhitaji huduma kama hizo wako wengi..wewe subiria PM muda si mrefu!! Usije kunisahau katika ufalme wako!
 
ndoto zina wigo mpana wa maono,yaweza kuwa ni janga kubwa la kitaifa likifanana na ajali ya ndege inapotokea ni mara chache kuwa na majeruhi
 
kama namuelewa elewa hvi anachomaanisha,.mmmmmh yawezekana haya yakawa kweli,.umesahau kuota kuwa itatokea Mwanza msimu wa mvua au?
 
Mie sijaelewa hapa: Umeota wewe umepata ajali ya ndege ukiwa unasafiri nayo au umeota ukishuhudia ndege inaanguka na kupata ajali? Kama umeota ni wewe umo kwenye ndege na umepata ajali basi jua jinamizi la ajali limekuganda, Funga na Fanya Maombi sanaaa na kwa upande wa shiling fanya vivyo hivyo. Amen
 
Nahisi mtoa mada anajihusisha na shughuli za ugaidi kwa hiyo ameweka mada hii makusudi kupima uhalisia na ugumu/urahisi wa kutekeleza jukumu lake la kulipua ndege tz
 
Hutokea yale ambayo amepanga muumba. Hamna dua la kuku liwezalo kumpata mwewe. Kama ni ajali ya ndege basi basi itakuwa lakini kama haja andika basi hata kama ukulazimisha haiwi.
 
Kuna kitu kinaclick kwenye akili yangu kila mara kinachoniambia kuwa kunaajali mbaya ya ndege itatokea tz soon, ndani ya miezi sita ijayo.
Nimejaribu kui-deny hii hali lakini nimeshindwa.

Naombeni muendelee kuomba na kukemea nami, ili hali hiyo isitokee kwani utakua msiba mkubwa na wenye gharama kwa taifa.
Matatizo ya kichwa huanza poole poole!!
 
Nahisi mtoa mada anajihusisha na shughuli za ugaidi kwa hiyo ameweka mada hii makusudi kupima uhalisia na ugumu/urahisi wa kutekeleza jukumu lake la kulipua ndege tz

Duu,,kaka sikuwai kufikiria hii.
 
Back
Top Bottom