Ajali mbaya ya gari na pikipiki, barabara ya Chalinze - Segera

Ajali mbaya ya gari na pikipiki, barabara ya Chalinze - Segera

Ni kweli unachosema,lakini hizo picha hazijavunja maadili yoyote katika jamii.Ni picha za kawaida sana maana miili haijaharibika,haioneshi tupu za marehemu. Inabidi uelewe kuwa picha ni muhimu sana haijalishi zipoje,tatizo linakuja kama zikitumika vibaya kinyume na maadili au ethics za kazi.
Usijali kiongozi hiyo ni general observation kwa kile ambacho huwa kinatokea hapa nyumbani na ndio maana ukaona tukakumbuka na mengine mkuu
 
Hizi bodaboda zimekuja kupunguza idadi ya watu hapa nchini. Walazwe mahali panapostahili marehemu.
 
wawili tumewazika mchana wa leo, mwingine ana hali mbaya hospitali.
Pikipiki waliyotumia haikuwa na breki yoyote. tuwe makini na vyombo vya moto hasa tunapokuwa kwenye highways.

Nina amin fika kama umeenda chuo cha mafunzo ya udereva ukasoma na ukaelewa ulichoelekezwa na wakufunzi wako,hutoweza kuingiza barabarani chombo cha moto kama hakina sifa za kuendeswa,hv pikipiki haina break unategemea ukafunge break zako ktk miguu ya watu?Pikipiki yangu endapo indicator moja haifanyi kazi naitengeneza kwanza kabla ya yote maana walioviunda hv vyombo hawakuweka kama mapambo.
Tufaham sheria na kanuni za barabaran kupunguza ajali zisizo na kisingizio.
 
Ajari haina kinga ila za kwetu nyingi zinazuilika maana ukiangalia vyanzo vya ajali unashangaa maana wengine ana over take kwenye kona tena yupo mafuta mengi, sheria zetu ni nzuri tatizo utekelezaji wa sheria kwa wahusika umekuwa mgumu mwisho wa siku wao wanachojua ni kuwapiga fine tu watu na kutoa leseni bila kufuata kanuni. Kujua kuendesha gari ni zaidi ya kuendesha bali pamoja na kujua sheria za usalama barabarani)
Nakubaliana na wewe mkuu.

Sisi uzembe mkuu, na hata vifo vingi ni uzembe kuanzia hospitalini na kwengineko
 
DSC_0627.JPG


DSC_0630.JPG


Mwendesha pikipiki na abiria (majina hayakutambulika) wakiwa wamelala chini katika barabara ya Chalinze Segera karibu na Kabuku baada ya kugongwa na gari ndogo yenye usajili namba T818 BNS leo mchana.
Inaskitisha sana,barabara zimejengwa kwa ajili ya kusafiria,now ni makaburi ya watanzania,
 
Ulimbukeni wa teknolojia utatumaliza! Badala ya kutoa msaada tunakimbilia kupiga picha ili tuweze ku.apload fasta kwenye blog zetu, poleni and R.I.P wahanga
 
yaan tungekuwa tunaweza kubashiri mambo yatokeayo mbeleni....hakika kusingekuwa na makosa
 
Ulimbukeni wa teknolojia utatumaliza! Badala ya kutoa msaada tunakimbilia kupiga picha ili tuweze ku.apload fasta kwenye blog zetu, poleni and R.I.P wahanga

hawajafa bana
 
Mkuu watu wanaijadili hiyo picha sio mleta uzi / mpiga picha maana hata kama picha imepigwa lakini hakuna hata dalili ya mtu au kivuli cha mtu kinachoonyesha angalau kuna mtu anamsaidia huyo jamaa kumnyanyua na kumsogeza pembeni kwa msaada mwingine sio wa saloon car, mara nyingi huwa tuna deal na watu walioonyesha dalili ya uhai au nafuu kama huyo mwenye Tshirt ya blue (kwa kawaida hutakiwi kumpakia abiria wa ajali kwenye saloon car kwa kuwa anahitaji kubebwa kwa utaratibu maalumu kwa kumlaza ili usiweze kuharibu uti wa mgongo na viungo vingine muhimu). By the way mleta uzi tunamshukuru kwa taarifa

Hapo sawa mkuu nimekubali. U got a point ila ukichunguza sana mpiga picha atakuwa alikuwa ndani ya kori au basi la abiria. Angalia sight mirror hio sasa sijui kama walipata muda wa kutoa msaada au dereva wa bus aliondoka.
 
yani kuna komenti zina ukakasi hapa,,
watu ka si watu.
 
]Ajali kama zimeshazoeleka vile?[/B]Kuna haja ya wadau wa matumizi ya barabara tukajadili tena,tunaangamia jamani
Kweli mkuu maana siku hizi watu 10 au zaidi wakifariki kwenye ajali inaonekana kawaida, miaka ya 90 mwanzoni ilitokea ajali ya bus la Yarabi Salama ikaua watu kadhaa, serikali ikaingilia kati na ndio mpka leo tunasafiri mchana na ajali zilipungua ikaja kutokea nyingine kama sikosei 1997 ya Air Msae nayo ikizua gumzo. Zamani zilikuwa zinachukua interval kubwa lakini siku hizi mwezi unasikia kimenuka, najua kuna ambao watasema magari ni mengi lakini kwenye ajali huwa hatuangalii idadi ya magari kama factor ya kuwa na ajali nyingi maana nyingi tunasababisha wenyewe
 
Sasa kucheka huko inamaana waliopata ajali ni mahayawani ?
Leo kwa mwenzako kesho kwako au kwa familia yako.Sioni sababu ya kucheka

Mkuu hayo maneno yakurudie wewe mwenyewe, sijamcheka mtu, nilimshangaa mchangiaji aliyesema hakuna maiti katika hii ajali na wakati maiti zinaonekana ,..
 
Sasa saloon car yako used na maisha bora nn? Usiwe limbuken ww hivyo ni vyuma chakavu tu vinavyotembea
 
Ajali mbaya inakua hivi ? bodaboda anapiga simu ?

mungu akusamehe na haya maneno yako hakika, usiombe hiki kitu hakuna kidogo, yani umenikera na hii coment yako. tena wewe utakuja kugongwa na baiskeli tu halafu utaona madhara yake. ogopa sana lami tena ukiwa kwenye mwendo hata wa kawaida. kweli kuna watu na viatu, sasa wewe ulitaka achezee viuongo vyake?
 
.....inasikitisha sana kwa kweli.......umasikini si kitu kizuri kwa kweli......tuweke sheria kali juu ya ubebaji abiria kwa kutumia pikipiki.....abiria awe mmoja tu.....tena na yeye pia awe na kofia ngumu......tunapoteza nguvu kazi nyingi sana barabarani.....
 
.....inasikitisha sana kwa kweli.......umasikini si kitu kizuri kwa kweli......tuweke sheria kali juu ya ubebaji abiria kwa kutumia pikipiki.....abiria awe mmoja tu.....tena na yeye pia awe na kofia ngumu......tunapoteza nguvu kazi nyingi sana barabarani.....
Wengi wanazo kofia ngumu, ila hawazitumii hadi akijua kuwa kuna askari trafiki karibu. Ukiangalia picha hii utaonna kofia ngumu ikiwa mbali kidogo na chombo, hapana shaka ilikuwa imening'inizwa tu juu ya chombo.

Ni vizuri kwa abiria nao kutopanda chombo bila ya kuwa na kofia hizo.
 
Back
Top Bottom