Ajali mbaya ya gari na pikipiki, barabara ya Chalinze - Segera

Ajali mbaya ya gari na pikipiki, barabara ya Chalinze - Segera

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,714
DSC_0627.JPG

DSC_0630.JPG

Mwendesha pikipiki na abiria (majina hayakutambulika) wakiwa wamelala chini katika barabara ya Chalinze Segera karibu na Kabuku baada ya kugongwa na gari ndogo yenye usajili namba T818 BNS leo mchana.
 
nikweli watu watatu ktk pikipiki wamefariki.
mmoja alikufa palepale na wa pili alikufa hospital ys magunga na watatu alifia njiani akiwahishwa kcmc moshi.

aliyekuwa mmojawapo ni mtoto wa omari wa samsasu. @ omari mchinja mbuzi wa kabuku.
 
Hiyo barabara huwa hawa watu wa pikipiki wanariski sana wanaendesha kama wapo peke yao
Sasa inapotokea unapishana na gari upande wa pili na barabara ni nyembamba lazima umpe upaja mwenye pikipiki la sivyo uende kwenye fuso
Ni hatari sana
 
nikweli watu watatu ktk pikipiki wamefariki.
mmoja alikufa palepale na wa pili alikufa hospital ys magunga na watatu alifia njiani akiwahishwa kcmc moshi.

aliyekuwa mmojawapo ni mtoto wa omari wa samsasu. @ omari mchinja mbuzi wa kabuku.

Aisee kwani bodaboda inapakia watu wangapi. Mbona unataja maiti 3 na mmoja kapona! Hio ni saloon car basi.
 
Poleni sana wafiwa. Barabarani ni heri kutii sheria bila shuruti ingawa siku yako ya kufa ikifika sio bodaboda wala nini utakwenda tu! Mungu awarehemu waliokufa.
 
Sio kuchukulia poa sababu waliokumbwa na ajali huwafahamu/huwajui kwa kweli inasikitisha sana
Ila na wengine wapo faster kupiga picha kuliko kuokoa maana nilitegemea picha ingeenda sambamba na zoezi kufanya uokoaji hasa kwa huyo jamaa mwenye Tshirt ya blue kidogo ameonekana na nafuu (angalau kumbeba akiwa kalala ili kuweza kuviweka viuongo vyake vizuri hasa uti wa mgongo badala ya kumwacha aamke mwenyewe kumbe ndio anavi-disturb viungo vyake)
 
Vifo hivi vinatokea mara nyingi sana katika mataifa maskini. Poleni sana majeruhi Sir God awalaze mahala pema walotangulia mbele za haki.
 
Aisee kwani bodaboda inapakia watu wangapi. Mbona unataja maiti 3 na mmoja kapona! Hio ni saloon car basi.

Poleni ndugu.huyu bodaboda aliibukia wapi?mbona yupo target kabisa upande usiostahili.ingekuwa DSD wenye gari wlishamalizwa maskini
 
Mtu atakae mlaumu mwenzie kwenye ajali za barabarani lazima awe hajui barabarani kukoje yaani hana gari na hajawahi endesha gari.
Hivi vitu hutokea ghafla sana kiasi kwamba sometime huna option zaidi ya kusababisha maumivu kama hayo.
Silaumu bodaboda au mwenye gari hapo inategemea tu je situation iliruhusu kuwakwepa?
Siwezi kujipeleka mvunguni mwa lori kisa boda boda kachomekea so nitaua lazima nimpe body tu kesi badae!
Kuna ndugu zangu 2 walikufa pale pale karibu na chainze ndani ya Rav 4. Boda boda kachomeka anamkwepa upande wa pili uso kwa uso na basi. Sasa nani mjanja hapo?
We learn through mistakes.
 
Ila na wengine wapo faster kupiga picha kuliko kuokoa maana nilitegemea picha ingeenda sambamba na zoezi kufanya uokoaji hasa kwa huyo jamaa mwenye Tshirt ya blue kidogo ameonekana na nafuu (angalau kumbeba akiwa kalala ili kuweza kuviweka viuongo vyake vizuri hasa uti wa mgongo badala ya kumwacha aamke mwenyewe kumbe ndio anavi-disturb viungo vyake)
Ni kweli mkuu huu utandawazi unachangia huduma ya kwanza ishuke siku hadi siku badale yake wanachojali kupiga picha na ukiangalia hapo kuna gari kubwa(BASI) kama sijakosea angalia kioo cha upande wa dereva kikubwa, na BASI nina uhakika lina abiria kwahiyo uwezekano wa kutoa msaada upo.

Majeruhi anajisaidia mwenyewe kwa kuomba msaada kwa simu kwa watu walio mbali kuwafahamisha nimepatwa na ajali, wakati alihitajika aliye karibu kufanya hivyo huku wakiendelea na kuwapa huduma ya kwanza na zoezi la uokoaji kwa ujumla
 
sasa mpiga picha amejali kupiga picha kwanza kuliko kuokoa kweli zama za mwisho hizi za kujipenda wenyewe.
 
Hizi ajali zitatumaliza tusipokuwa makini na kuzingatia sheria za barabarani.Nidhamu ya barabarani unapokuwa na chombo cha moto ni muhimu sana.Tatizo lingine kwa waendesha bodaboda wanaotumia hizi barabara kuu za mikoani wanapenda sana kuzidisha abiria na hata mizigo.Nadhani adhabu kali itolewe kwa bodaboda anayekiuka sheria hizi.Tumechoka sana na hizi ajali khaa!!
 
Back
Top Bottom