Pole ndugu.
Utawala bora (usalama barabani sawia) hautokani na rais kutangaza adhabu, bali kuwepo sheria na mfumo stahili wa kusimamia utekelezaji wa sheria husika; rais ndiye msimamizi mkuu kuhakikisha sheria zinatekelezwa.
Sasa ni bora kufahamu kuwa rais kutangaza adhabu ni kiashiria cha kushindwa kusimamia utekelezaji wa sheria, period!
Tubadilishe mwelekeo wa mjadala. Tunachoshuhudia kama kuparanganyika katika jamii ya Tanzania ni matokeo ya utawala wa hovyo, usiosimami sheria kwa manufaa ya wananchi wake. Wananchi/madereva hawafuati sheria kwa sababu serikali, kutokana na kughubikwa na rushwa na ufisadi, imeshindwa kusimamia utekelezaji washeria. Sasa hili siyo suala la baranbara kuwekwa au kutowekwa matuta. Aidha siyo tatizo la uslama barabarani peke yake; ni tatizo la usalama wa kila mtanzania kila mahali; mahospitalini, mashuleni, majini na reli, masoko ya mazao ya wakulima, bidhaa za madukani, ujenzi wa barabara, mabwawa na majengo makubwa, uvuvi, mikataba ya rasilimali kama madini na gesi na kadhalika. Ki-msingi, kila kitu nchini Tanzania ni couterfeit!
Mjadala wetu ulekezwe namna wananchi wananvyoweza kuishughulikia serikali na hatimaye waweze kuondoa counterfeit leadership, basi! Tunadhurika kwa sababu tunapenda kuelezwa na kusikia ufumbuzi wa kutumia njia za mkato kushughulikia matatiza makubwa. Kwa mtindo huu hatufiki popote. Tuinue macho na kuangalia/kuona mabli. Licha ya kwamba kuweka matuta kwenye highway kama barabara ya Morgoro ni upuuzi, si ufumbuzi bali ni chanzo cha tatizo lingine, kwa mafano foleni. Ni yale yale ya 'ubunifu' wa Lowasa wa ufumbuzi wa tatizo la foleni kwa 'njia tatu'. Je tatizo liiisha? jibu ni hapana ila lilianzisha tatizo jingine la ajali za barabarani zisizotambuliwa na bima kwa sababu ni kinyume cha sheria za barabarani!
Think loudly.