Ajali mbaya ya daladala kimara-suka

Yesuuuuu...Hivi suca si kuna matuta pale? Kuna nini kimara??????
Jamani haya matuta au speed humps haziondoi ajali bali zinazidisha ajali. Pia ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Think this way, you put more humps and bumps on the highway, you reduce speed during crossing those humps/bumps but someone has to drive faster just after crossing the humps/bumps to catch up with time, then what happens? an accident. Again you spot where the accident happened and you put another bump, etc,etc, how many bumps are you going to put on the road? Some bumps/humps has no warning signs and hence for a new driver to that route can actually lead to another accident if crossed unexptedly at high speed.
If the roads are made with clear signs at correct locations enough to warn, and people (drivers, pedestrians, cyclists,etc) who do not respect signs are fined accordingly, it may reduce the number of accidents on the road but more importantly the education of both drivers and other road users is very important in addressing road accidents.
 
Madereva TZ ni matatizo makubwa, 80% ya madereva wetu hawafuati sheria za usalama barabarani kabisa kitu ambacho ni hatari hata ukiweka mashimo kama mito barabarani ajali zitaendelea kutokea tu. Wewe chakulia mimi huwa natokea mbezi asubuhi foleni inaanzia Temboni mpaka Kimara lakini utakuta gari kibao zinapita pembeni zikiwemo gari ndogo pamoja na daladala tena mwendo mkali wala hamna hata wa kukemea hata magari ya serikali yeneyewe yanapita pembeni bila kujali kabisa, sasa hapa utasingizia nini sasa?. Mimi ningepewa madaraka ningeweka kampuni binafsi kusimamia sheria za usalama barabarani maana polisi wetu kazi imewashinda kabisa. Pia sheria ipewe makali maana Dar kila mtu ni dereva hata kijana wa shule kama kwao kuna gari ni dereva, watu wanaendesha magari wamelewa, wanapiga simu nk. Daladala ndo kero kubwa sijui viongozi wetu hawayaoni haya!, Yaan barabara zetu ni shamba la bibi unaweza pita sehemu yeyote au kukatiza sehemu yeyote kama mtembea kwa mguu hata kama polisi yupo hakufanyi lolote. Mfumo wa usalama barabarani umekufa kabisa na hili litaendelea ku-cost maisha yetu.
 
hizi ajali zitatumaliza jamani....madereva wa daladala muda wote wanajiona wana haraka.....wanazidi kutuua..............
 
jamani serikali ya mkoa dar ilishatangaza kwa tanzania wote wanaoona uozo kama huu wa madereva kuyapiga picha magari hayo yakiwemo yanayokatisha ruti na kuzipeleka kwa jeshi la polisi na zawadi yake walisema ni tsh.5,000/=kwa kila picha.Hili ni jukumu letu sote kuhakikisha maisha yetu hayachezewi kiasi hicho..................

Ajali nyingi karibia 98% zinasababishwa na mwendo kasi. Unaweza ukawa unaendesha kufuata maelekezo ya vibao vya usalama lakini huku nyuma wenye haraka watakuwashia mataa ya kukuelekeza zidisha speed. Sidhani kama hapa Dsm kuna sehemu inaruhusu kuendesha zaidi ya 60 speed, lakini utakuta watu wanaendesha 120 speed.

Pia chunguza kuanzia Kimara hadi Mbezi hakuna vibao vya usalama barabarani, na wala hakuna kiashilio cha kuonyesha hata hayo matuta wanayoyaweka.
 
jamani serikali ya mkoa dar ilishatangaza kwa tanzania wote wanaoona uozo kama huu wa madereva kuyapiga picha magari hayo yakiwemo yanayokatisha ruti na kuzipeleka kwa jeshi la polisi na zawadi yake walisema ni tsh.5,000/=kwa kila picha.Hili ni jukumu letu sote kuhakikisha maisha yetu hayachezewi kiasi hicho..................

Serikali isikwepe jukumu la kusimamia sheria, sasa kwa mtindo huu wa kupiga picha utapiga picha magari mangapi mzee maana pembeni kuna msululu wa magari kama barabarani tu!. Isitoshe kupiga picha ni process ndefu tu ambayo dereva atwambia alikuwa service road anaziba pancha utamfanya nini na sheria inaruhusu kutegeneza gari lako kwenye service road? Dawa ni papo kwa papo wiki mbili keko tu. Kuna nchi kama Singapole wanasimamia sheria hakuna mzaha mfano rushwa adhabu yake miaka 20 jera iwe ya shilingi 1 au zaidi. Sasa sisi tunakuja na solution ya kupiga picha kwa 5,000 ndo nini sheria inasemaje? dawa ni kusimamia sheria tu bila kucheka na mtu. Hata ukipiga picha gari mfumo wa magri ni mbovu utalikamata saa ngapi hilo gari na picha yako si afadhali muda wa kutafuta gari na picha yako mkonononi usimamie sharia tu mzee!
 
Tatizo lingine ni kuwa Askari wa barabarani pamoja na kuwa wengi wao huchukua rushwa lakini pia hawatoshi.

Madereva wengi hasa wa mabasi hupeana taarifa ya kuwepo Askari barabarani, na sehemu korofi kwa ajali kama yupo askari, madereva wengi hupunguza mwendo.

tatizo ni kubwa zaidi ya linavyoonekana!!
 
Madereva wa daladala hata hawafai kuwa mbele yako au nyuma yako. Hata akitanua uwe mwangalifu kupita kiasi asikuzoe. wengi ni wababe, walikoanzia udereva ni upiga debe,--- ukonda---uday waka---udereva. Utadhani sio watu vile. Lakini wapo wachache sana ni madereva kweli na wana busara barabarani. Kuna wengine wala sio daladala lakini saloon, wanashindana na daladala akili zao. Wengi wa madereva wa malori wana busara sana na tena wanajali sana.

Pole sana waliofikwa na ajali hii. Tena wiki la usalama barabarani!!!!!

Leka
 
tatizo siyo madereva, tatizo ni kutokuwa na sheria kali. Nchi jirani Sudan ukimgonga mtu ni lazima umtibie hadi apone na unamlipa dola 5000 na akifa faini ni dola 10000 za marekani. Usipo lipa ni kifungo jera miaka 30, tanzania tunahitaji sheria hizi haraka.
 
Na mtu akigonga gari je? Maana ajali zingine zinasababishwa na pedestrians, ubovu wa barabara, mechanical malfunctions, etc. Tusikimbilie kuiga sheria za kikandamizaji kama hizi kutoka nchi kama Sudan ambayo ina mchanganyiko wa utawala wa kijeshi na kidini (sharia law).
 
People of God, ajali zinatokea si Tanzania tu hata Ulaya na Marekani zinaongoza. Kinachohitajika ni kuelimisha madereva na abiria kuhusu matumizi ya barabara na udereva wa kujikinga (defensive driving). Hii ni muhimu sana na kinachotakiwa kufanywa ni kubadilisha fikra za watu na madereva wawewaangalifu barabarani, wawe na mzigo moyoni kuwa kila mtu anatakiwa arudi na kuiona jamii yake tena baada ya kutoka nyumbani. Inatakiwa kuwepo na mtaala wa usalama barabarani kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Faini kubwa sio suluhisho, labda serikali ifanye ni njia ya kuongeza mapato lakini muhimu ni kuelimisha umma.

Yes, but a proposal sounds more gospel than that of the real world!!!!
 
Pamoja na madereva kutokuwa na nodhamu wawapo kazini ila pia hata miundombinu( Barabara) zetu zinachangia sana kuna haja kwa serikali kuweka zaidi mkazo wa ujenzi wa barabara za kisasa.Sababu nyingine ni pamoja na askari wetu kujali rushwa kuliko uhai wa binadamu na pia sheria bado hazipo strong mtu akiua ni vema asipate tena chance ya kuendesha gari maishani mwake na kutupwa selo for good!
 
Mbona habari ya ajali hii mbaya ya jana asubuhi haipo katika vyombo vya habari hasa magazeti ya leo??
Hata mimi nashangaa kwanini hata vyombo vya habari havijatangaza. Inatupa wasiwasi kama kweli ilitokea au la.

Wakati fulani ajali zingine huwa haziripotiwi, kwa mfano HII HAPA ambayo niliinasa 'live' na kuchukuwa picha papo hapo kama ilivyoonekana
 
Back
Top Bottom