natoa pole kwa wafiwa, lakini sasa turudi kwenye ukweli, utii wa sheria bila shuruti kwa maana ya kufuata sheria za usalama barabarani, wenzetu wa bodaboda baadhi yao ama hawajui sheria au hawazingatii sheria za usalama barabarani, hili mimi binafsi nimekuwa nikishuhudia mara kwa mara, mimi nafikiri pamoja na kutoa pole kwa mwenzetu lakini tutumie mwanya huu kuwasisitizia wenye pikipiki kuheshimu sheria za usalama barabarani na pale ambapo yupo kwenye sheria lakini akaona gari inamfuata aipishe ili kuokoa maisha yake, mbona hata sisi wenye magari madogo unapoona kuna gari kubwa linakuja upande wako unalipisha kuokoa maisha yako na gari lako kitu ambacho madereva wengi wa bodaboda hawakifanyi.