Ajali mbaya ya basi

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
111
Kuna ajali mbaya ya basi imetokea katikati ya Aljaezira na Mikumi. Basi liliacha njia na kuelekea pembeni ambapo limejigeuza na matairi kuwa juu. Majeruhi ni wengi na nimeshuhudia maiti moja ikiwa imefunikwa pembeni mwa barabara. Polisi bado hawajafika eneo la tukio na hapa nipo na majeruhi wanaenda kituo cha polisi mikumi kupata pf3 kwaajili ya kwenda kutibiwa. Basi linaitwa Al-mu(jina gumu). Source mimi mwenyewe nipo kwenye basi la Alsaedy kutoka Mbeya kwenda Dar.
 
OMG!!!!!! jamani hawa madereva watatumaliza na TBS wasivyojali tena ndio balaa
rip na poleni majeruhi
 
AJ JAZZERA,aL MUM SIJUI AL NINI AJALI ITAKUWA IMESABABISHWA NA AL KAEDA HIYO

tupia maphoto mkuu

POLENI WAASIRIKA
 
Kuna ajali mbaya ya basi imetokea katikati ya Aljaezira na Mikumi. Basi liliacha njia na kuelekea pembeni ambapo limejigeuza na matairi kuwa juu. Majeruhi ni wengi na nimeshuhudia maiti moja ikiwa imefunikwa pembeni mwa barabara. Polisi bado hawajafika eneo la tukio na hapa nipo na majeruhi wanaenda kituo cha polisi mikumi kupata pf3 kwaajili ya kwenda kutibiwa. Basi linaitwa Al-mu(jina gumu). Source mimi mwenyewe nipo kwenye basi la Alsaedy kutoka Mbeya kwenda Dar.
itakuwa ni ALIHUSHOOM daa sijui mda wa sadaka umefika!
 
Poleni mliopata ajali Mungu atawaponya mapema mrudi kuja kuipigania Tz
 
Pole kwa waliowapoteza wapendwa wao.Majeruhi nawaombeni mpone haraka
 
Poleni sana wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine na ajali hiyo!
 
poleni kwa wote waliokutwa na huu mkasa, maeneo kama hayo inahitajika helicopter kuwahaisha majeruhi ktk hospitali kubwa.
 
Poleni sana majeruhi

RIP marehemu wote.

Poleni sana ndugu wa marehemu.

Hawa madereva watatumaliza, inabidi ibadilishwe sheria kwa madereva.

Isiwe tena kifungo, bali wanyongwe hadharani itakuwa fundisho.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Tumewapa lift majeruhi mpaka k2o cha polisi na wameshaenda kutibiwa. Ile sehemu ina mteremko mkali then hakuna netwk.
 
Hizi ajali sasa too much! Tuamini kwamba Mungu kapanga au? Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo tukisafiri, watu walikua wanauliza dereva wa basi husika mtu analosafiri nalo,unakuta ni mzee wa makamo na Kaunda suti yake yake! Siku hizi pale Ubungo ukiulizia dereva unaambiwa 'Dogo flan'..halafu anakuja na chupa ya maji baridiii! Kumbuka saa kumi na mbili hiyo asubuhi! Dereva huyu kaingia jana toka Mwanza saa 4 usiku! Tutegemee nini?
 
kwa watumiaji wa njia kuu ya Iringa - Moro mtakua mnajua hicho kipande alichokitaja mdau jinsi kinavyovutia kufanya makamuzi, nadhani dereva atakuwa alijiachia ile mbaya...
Mungu tusaidie waja wako maana nchi hii kila letu siye baya...lol!
 
Back
Top Bottom