Ajali mbaya ya basi la Meridian

Ajali mbaya ya basi la Meridian

Poleni sana wote mliofikwa na ajali hii, RIP wale waliopoteza maisha!
 
Oooh my Tanzania! Hali hii hadi lini?
Poleni sana wafiwa pamoja na majeruhi.
 
Ameshindwa kumiliki kona na mteremko mkali ukiwa unatoka mbwewe kuelekea lugoba.
Poleni sana wahusika wote,Madreva wanakwenda mwendo kasi sana,na huku waweza kuta anaongea na simu,Hasa magari yanaotoka maeneo ya Arusha na Moshi.poleni sana wa Tanzania wenzetu.Hakika sisi ni Wa Allah,na kwake tutarejea.
 
Poleni sana Majeruhi na Wafiwa wote

Ni nini kimelikata hilo Bus
 
Ee Mungu waguse majeruhi kwa mkono wako wa uponyaji. Wapendwa tuombee kwa ajili ya wasafiri na vyombo vya usafiri! Walitutoka Mungu awapumzishe kwa pema peponi.
 
Poleni sana majeruhi na kw waliofariki Mungu awape neema yake kuingia uzimani. Kwa upande wa Meridian ukweli inakimbia sana ndo inayoongz kuingia ubungo kutoka rombo
 
Ameshindwa kumiliki kona na mteremko mkali ukiwa unatoka mbwewe kuelekea lugoba.
waswahili,wabantu na wataalamu wa lugha nisaidieni hapo,tafadhali ijapokuwa sii jukwaa lake.
Wamefariki wangapi?
 
Mleta taarifa tusaidie kujua hali za majeruhi na vifo kama vipo.natumaini wewe upo eneo la tukio.
 
Nimeshaondoka. Kuna Lori linajaribu kutoa msaada. Watu na watoto wanalia sana. Damu kila mtu. Kama watatu tayari wamepoteza maisha. Mimi naenda Arusha.
 
Namna gari lilivyoharibika linakaribia kufanana na ile ajali ya basi la Air Msae ya mwaka 1999.
 
Hiyo mechanism ya ajali ipoje mpaka basi libakie na sit tuu...dah
 
Mungu tusamehe kwakuwa haya yote yanatokana na dhambi zetu zilizokithiri.....poleni majeruhi, poleni wafiwa, RIP marehemu
 
Mungu awalinde na kuwaponya wote walionusurika, waliopoteza maisha mtangulie kwa amani. Too sad.
 
Back
Top Bottom