Ajali mbaya Arusha - Kisongo, takribani watu sita wafa.

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Ajali mbaya imetokea Arusha leo hii, maeneo ya Burka - Redds na kupelekea takribani watu sita kufa. Chanzo cha ajali inasadikiwa ni poor overtaking baada ya dereva wa Hiace No. T706 BFE alipokuwa anajaribu kuovertake gari nyingine na kukutana uso kwa uso na gari Toyota Hilux T509 ATY na kusababisha ajali hiyo mbaya.

Photo0642.jpg


Gari hiyo ilikuwa imetokea Kisongo - Gereza Arusha au Airport kwa mujibu wa mashuhuda walioiona ikitoka eneo hilo, na kwa kuwa leo ni siku ya Jumapili hivyo ni ruksa kuona mahabusu na wafungwa. Wakati ikirudi ndipo ilipobeba baadhi ya watu hao waliotoka kuona ndugu zao na kupata ajali mitaa hiyo.


Photo0647.jpg

Hiace inayosadikiwa kusababisha ajali.

Photo0645.jpg





Photo0643.jpg

Wakuu nilichelewa kupata taarifa na kufika eneo la tukio lakini nilifanya mahojiano na baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa wale watu waliopakizwa katika Hilux waliruka baada ya kugongana na wengine kudondokea kwenye lami na kuumia vibaya licha ya wanaosadikiwa kufa.
 
Asante kwa taarifa iliyo kamilika

Dereva wa gari lilikuwa likipitwa na hiyo Hiace yeye ilibidi kusimama baada ya kuona ile Hilux ipo kasi na ndipo aliposhuhudia ajali hiyo lakini kutokana na hali ilivyo amefichwa ili akili itulie lakini pamoja na hayo maelezo yake hayatofautiani sana na hayo niliyayaweka hapa. Nikipata taarifa nitazidi kutupia tupia jukwaani.
 
Ajali mbaya imetokea majira ya mchana leo iliyohusisha magari matatu kwa wakati moja!
Imeua watu watano hapo hapo,na kujeruhi wengine wengi.

Imehusisha gari aina ya hiace ila ni la binafsi,Hilax pickup mashavu na landrover ya kampuni ya leopard.

Mi nimekuta tukio likiwa limeshatokea ila uhakika kwa watu niowakuta ni kwamba raia hao watano wamepoteza maisha.

MUNGU AWALAZE MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI,na hata walio majeruhi MUNGU watie nguvu wapone mapema!

Ni hayo tu WanaJF na nikaona niwajuze!

Jioni njema wote.
 
Mungu awalaze mahali pema peponi Amina waliojeruhiwa tunawaombea wapona haraka sana...
 
hicho kipande kibaya sana, kisongo, meserani, duka bovu, pana ajali sana..,

rip marehem
 
Very sad, R.I.P marehemu wote! Majeruhi wote mungu awatie nguvu mpate nafuu.
 
Kwa mujibu wa wajeruhi waluopo Mt Meru wanaendelea vizuri na dereva wa Hiace ni miongoni mwa waluovunjika mguu lakini anaendelea vizuri.

R.I.P marehemu wote ambao wengi walikuwa katika Hilux.
 
hili eneo naliheshim sana......kwa macho yangu nilishawahi kushuhudia mtu akizolewa na gari na kufa papo hapo........
ni eneo ambalo nikipita huwa speed inakuwa 10kph.......na inaonekana hiyo Hilux ni zile za samaki kutoka Babati.......huwa zinakimbia sana sana sana.......
R I P marehemu wote.......
 
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wafiwa na wale wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo~AMEN
 
Back
Top Bottom